Tuesday, 21 July 2015

Re: [wanabidii] wapinzani hawajajipanga tangu 1992, watanzania watawaamini kuwapa dola?

Brother Muhingo Wasalaam.
Ni vema tukajifunza kwamba mabadiliko yeyote katika jamii yeyote ni lazima yaambatane na vizingiti kedekede.Hivyo basi katika mazingira wanayokutana nayo kama chama cha upinzani wa kweli ni dhahiri kwamba kila mmoja anaona jinsi CDM kilivyoweza kujipambanua kuwa ni chama cha upinzani wa kweli tofauti na watangulizi wake waloweza kuwa na nguvu mathalan NCCR -Mageuzi wakati wa Mrema -1995 na baadaye CUF miaka ya 2000 na tangu mfumo wa vyama vingi ulipoingia Tanzania Zanzibar.CDM kimeweza kuhimili mikiki mukiki ya nguvu na ya kutosha na kifanya yasotarajiwa, kupambana kisheria na hila za CCM hatimaye haki ikaonekana ikitendeka mchana wa adhuhuri.
Naomba tuwaunge mkono badala ya kuwakatisha tamaa makamanda

PBK


From: 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, July 21, 2015 5:23 AM
Subject: [wanabidii] wapinzani hawajajipanga tangu 1992, watanzania watawaamini kuwapa dola?

•  Hadi sasa hawajafanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya viongozi wao kuongoza dola, wamekurupuka na kuacha maswali mengi ikiwa kuwa na wagombea wenye dosari ambazo zinaepukika!

•  Ikulu sio mahala pa mchezo, utani wala pa kuhadaa Watanzania kwa kuuza sera zisizotekelezeka!

•  Halikadhalika wapinzani wameshindwa kujitandaza barabara nchi nzima tokea 1992 mfumo wa vyama vingi ulipoanza!

•  Lakini pia hawajaonyesha ukomavu wakuwa na mtandao wa umoja miongoni mwao dhidi ya CCM!

•  Uchu wa madaraka umezidi uwezo wao wa kudhibiti nchi jambo la hatari sana, hata kama baadhi ya taasisi za habari na wasomi zinajaribu kuwafagilia ili wakamate dola kwa njia za mkato!

•  CCM bado ni chama makini chenye mtandao wa uhakika unaofika vijijini japokuwa kinaendeshwa na binadamu ambao sio malaika!

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment