Wednesday, 29 July 2015

Re: [wanabidii] CHADEMA lazima ijiandae kukabiliana na mambo yafuatayo...

CHADEMA ininusurika itakuwa chama kikubwa cha upinzani. Haiwezi tena kuvuka mstari huo. Acha maumivu ndani ya chama ila pia imewaumiza watanzania waliokiona kama chama tawala kitarajiwa. Kitendo cha kukiri kuwa hakikuwa na mgombea urais bali kilisubiri atakayetemwa na CCM basi watanzania watataka kuiona CHADEMA mpya isiyoongozwa na waliotamka upuuzi jana. Itapatikana wakijiuzulu au wakifukuzwa. Nimesema Ikinusulika. Uwezekano wa kupolomoka kama NCCR Mageuzi au TLP ni mkubwa. Wakiweza kubadili na kumpata mgombea urais wa ndani majeraha yatapungua.
--------------------------------------------
On Wed, 7/29/15, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] CHADEMA lazima ijiandae kukabiliana na mambo yafuatayo...
To: "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, July 29, 2015, 9:53 AM



CHADEMA lazima ijiandae
kukabiliana na mambo yafuatayo...


Hata kabla ya kuja kwa
Lowasa ndani ya CHADEMA kulikuwa kumeanza
kuonyesha dalili mbaya sana;



Mosi, katika kura za maoni; kuna malalamiko mengi sana ya
kujihusisha na rushwa
kwa baadhi ya wagombea wa ubunge. Changamoto kubwa ni kwamba
ushahidi wa rushwa
ni mgumu mno kuuthibitisha. Ikumbukwe kuwa hata ndani ya CCM
kulianza na
minong'ono ya rushwa kutoka kwa watu wa kawaida lakini
viongozi wakawa wanaziba
masikio kwa pamba leo hii rushwa inakitesa chama cha
mapinduzi.



Pili, kuna baadhi ya makada waliotoka CCM na hata wale
waliokuwepo ndani ya
chama wamebadili kabisa njia ya ushindini, kwani kwa sasa
njia wanayoiamini
sana ni kutoa rushwa, wengi wao wameshinda kura za maoni
ndani ya CHADEMA, na
wengine ndani ya Chadema wanaamini katika ushindani wa hoja
tu na si rushwa
hawa ni wachache sana na nafasi yao kwa sasa ndani ya chama
inafifia sana tena
mno kwa sababu nguvu ya PESA kwa sasa ndani ya CHADEMA
imeingia kwa kasi.



Tatu, Hatari nyingine ninayoiona ndani ya chama ni kupenda
mno vitu vya
Uliberali kuliko vya Kijamaa. CHADEMA inaamini katika Mrengo
wa kati yaani mazuri
ya Ujamaaa na ya Uliberali. Mimi naona chama kimeegemea sana
kwa sasa kwenye
Uliberali wakati kimefika hapa kilimo leo kwa sababu ya
kuegemea sana kwenye
Ujamaa wa Kisasa. Bila kurudi kwenye Ujamaa wa kisasa naona
hatari sana ndani
ya chama.



Nne, Ujio wa Lowasa una faida na hasara. Mosi, endapo kundi
la Lowasa litaanza
kuwanyang'anya makada wa CHADEMA nafasi walizonazo kwa
kisingizio kuwa hawana
hela za kufanya siasa ndani ya chama, kuna hatari sana ya
CHADEMA kukabiliana
na upinzani mkubwa ndani ya chama kuliko wakati wowote ule.
Pili, Kuna kundi
kubwa bado lina mini katika Dr. Slaa nalo linatakiwa baadae
lipewe maelezo ya
kutosha kabisa kuwa kwa nini Dr. Slaa asigombee URAIS.
Hasara yake nayo iko
kwenye kuaminisha Watanzania kuwa ni fisadi na kwa sasa
kuwashawishi kuwa
Lowasa si fisadi hili jambo litaitesa sana CHADEMA.



Tano, shutuma za ufisadi kama silaha kubwa ya CHADEMA lazima
wataalam wa siasa
ndani ya chama wajiandae kuja na hoja zenye mashiko ili
kuendeleza neno hili
ambalo limeonekana kwa muda mrefu kama nguzo ya CHADEMA.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment