Thursday 30 July 2015

Re: [wanabidii] Lowassa ni mzigo, Slaa angekuwa chaguo sahihi!

Email moja humu imekuwa hacked???
--------------------------------------------
On Fri, 7/31/15, 'Lesian Mollel' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Lowassa ni mzigo, Slaa angekuwa chaguo sahihi!
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, July 31, 2015, 1:59 AM

Ndio maana wana habar wkt mwingine
mnachukiwa na watu mnaandika as if iko hvyo kumbe
umepelekewa na maono yako,better u write bila kujichukulia
kama wewe,analysis nayojua mimi, ni ile ambayo ni research
based,i did journalism for 8 years nikaacha,mbwambo was my
editor kasuku newspaper pale jet,sikudhani kama angeandika
hv,kachemka kweli.ametumwa na fikra zake.
Anyway tunaheshim mawazo yake na ionekane ni mawazo yake sio
ndivyo ilivyo
Lesian

Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:

Umeona, eeh? Naheshimu maandiko ya Mbwambo lakini
katika hili amebugi.em
Sent from my iPhone
On Jul 30, 2015, at 8:48 AM, Telesphor Magobe <tmagobe@gmail.com>
wrote:

Mhu! Naona
roho ya CCM ndani ya makala hii na hivyo inaegemea upande
fulani na siyo uchambuzi huru.

2015-07-30 15:21
GMT+03:00 fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com>:


Johnson Mbwambo
Lowassa ni mzigo, Slaa
angekuwa chaguo sahihi!


WAKATI naandika makala
hii, habari zilikuwa zimezagaa ya
kuwa Umoja wa Vyama vya Upinzani nchini (Ukawa), na hasa
Chadema walikuwa
wamekubaliana kumpokea Edward Lowassa na kumfanya kuwa
mgombea urais wao kwenye
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Nathubutu kueleza wazi kwamba hilo
ni kosa ambalo
watalijutia kwa miaka mingi.


Sijui nini kilikuwa
kinaendelea katika vichwa vya viongozi
wa Ukawa wakati wakifanya maamuzi ya mwisho ya kumpokea
Edward Lowassa na hata
kumfikiria kuwa ndiye anayestahili kupeperusha bendera yao
kumkabili Dk. John
Magufuli wa chama tawala, CCM, kwenye patashika ya Oktoba ya
kuwania kukamata
dola.


Najua ya kwamba
'siasa ni mchezo mchafu', lakini bado
najiuliza maswali kibao kichwani mwangu ya ni hoja zipi
Chadema ilizizingatia
katika kumkubali Lowassa – mtu ambaye chama hicho
kilimuorodhesha katika ile
orodha ya Mwembe Yanga ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini
– List of shame
(orodha ya aibu).

Chadema haikupata
kumuondoa Lowassa katika orodha hiyo. Na
ndiyo sababu wengi wetu tumepigwa na butwaa kwa hatua yake
ya ghafla ya
kumkubali mtu huyo kuwa anakifaa chama hicho kubeba bendera
yao ya kuwania
urais.


Je, ni kwa sababu labda
ana maono (vision) ya namna ya
kuikomboa nchi hii au ni kwa sababu tu ya mapesa yake? Au
tuseme ni kwa sababu
ya 'umaarufu' wake? Au labda ni kwa sababu ya uwezo wake
kiutendaji? Au ni kwa
sababu ya marafiki zake matajiri atakaohama nao? Vyovyote
vile, umma unawadai
viongozi wa Chadema na Ukawa majibu ya maswali haya.


Hivi Chadema (achilia
mbali CUF) inawezaje kusimama jukwaani
na kumnadi urais (au hata kuwa naye tu jukwaani) mtu ambaye
yumo katika orodha
yao ya mafisadi papa nchini? Wataanzia wapi na wataficha
wapi nyuso zao? Au
labda ni kwa kuwa IQ ya Watanzania ni ya kiwango cha chini,
na ndiyo maana
wanaamini watasahau ya jana kuhusu mgombea urais huyo?


Hivi nani asiyejua ya
kuwa Lowassa anahamia Chadema si kwa
sababu ya kukipenda chama hicho na sera zake, lakini ni kwa
sababu ya kuikomoa
CCM iliyomtosa? Hivi kweli mtu anayeingia chama kulipa
visasi au kukikomoa
chama chake cha zamani anaweza kuwa na faida yoyote kubwa na
endelevu kwa chama
hicho alichohamia na kwa Watanzania kwa ujumla? Tangu lini
visasi binafsi na
kukomoana vikachukua nafasi ya mustakabali wa taifa?


Vyovyote vile, Chadema
na Ukawa yao itabidi, kwenye kampeni
ya urais waanze kwanza na kumsafisha Lowassa (sijui kwa
sabuni gani) ndipo
waeleze sera zao kwa wapiga kuwa. Itabidi kwanza wazifute
hadharani kauli zote
za nyuma ambazo ziko kwenye kumbukumbu walizozitamka dhidi
ya Lowassa
kumhusisha na ufisadi, na ndipo waanze kumnadi au hata
kuhalalisha tu kuwa naye
kwenye jukwaa wakati wa kampeni.


Baba wa Taifa, Mwalimu
Nyerere, alipata kusema ya kuwa mtu
akishakuwa tu na tuhuma kubwa za ufisadi hafai kufikiriwa
urais, na naamini ni
kwa hoja hiyo hiyo CCM iliamua kumtosa Lowassa hata bila ya
kufikisha jina lake
kwenye vikao vya juu kabisa vya maamuzi – Kamati Kuu, NEC
na Mkutano Mkuu.


Sasa, ni 'maajabu'
kwamba Chadema, badala ya kujisifu
kwamba, kimechangia kuifanya CCM imtose urais mtu aliyekuwa
kwenye orodha yao
ya 'list of shame', ndicho hicho kinachompokea kwa
mbwembwe – yaani mtu yule
yule kiliyempiga vita kuwa ni fisadi!!! Jamani, ni kwa
sababu ya mapesa yake tu
au ni kwa sababu ya maslahi binafsi na si maslahi mapana ya
chama na
Watanzania?


Nimedadisidadisi ni vipi
Chadema na Ukawa walikubali
kumpokea mtu ambaye chama tawala CCM kilimtosa kwa sababu ya
tuhuma za ufisadi
- mtu ambaye Chadema kilishiriki kueneza habari nchini nzima
kuwa ni fisadi.

Jibu nililopewa na
ninalopewa ni kwamba eti Lowassa ni 'mwathirika' tu wa
mfumo
(system) wa kifisadi wa Serikali ya CCM. Eti sasa wanadai ya
kuwa Lowassa ni
msafi ila mfumo wa kifisadi ndiyo tatizo kuu linalopaswa
kupigiwa kelele! Mbona
haya hawakutueleza tangu mwanzo? Au ndo wameyajua baada ya
yeye kutoswa na CCM?


Lakini hapa kuna swali
jingine. Huo mfumo (mimi nauita
mtandao) uliwekwa na unaendeshwa na kina nani? Si kweli
kwamba nyuma ya mfumo
huo kuna watu na Lowassa, kama mmoja wa watu walioshika
nafasi za juu za
uongozi nchini, ni sehemu ya mfumo huo? Kweli

Watanzania tumepoteza
uwezo wa
kufikiri (we have gone crazy)!

Ndugu zangu, nasisitiza
tena ya kwamba Chadema na Ukawa
wamefanya kosa ambalo watalijutia. Nadiriki kusema ya kuwa
kama kweli
watamsimamisha Lowassa kuwa mgombea urais wao, basi
wameshindwa uchaguzi wa
Oktoba hata kabla hawajaingia kwenye kampeni zenyewe.

Kama wamesahau,
waulize
kilichomkumba Augustine Mrema kwenye uchaguzi wa mwaka 1995
baada ya kutoka CCM
akiwa na huo unaoitwa 'umaarufu' ambao leo tunaaminishwa
Lowassa anao hivi sasa
nchini!

Binafsi, sioni namna
yoyote ambayo Rais Kikwete na CCM yake
ataukabidhi urais kwa Lowassa Novemba mwaka huu.
Ninachokiona ni kwamba sasa
Kikwete na CCM yake watafanya kazi usiku na mchana
kuhakikisha Lowassa hakamati
Ikulu.
CCM watapindua kila
jiwe kuhakikisha Lowassa hawi rais wa nchi hata kama
atasimama kwa tiketi ya Ukawa. Kama mnabisha, subirini
Oktoba muone matokeo!

Kwa mtazamo wangu,
niliamini, na bado naamini ya kuwa 'The
Chosen

One' kutoka Ukawa
alistahili kuwa Dk. Slaa wa Chadema. Takwimu za
uchaguzi wa mwisho wa mwaka 2010 zinaonyesha ya kwamba
walijiandikisha wapiga
kura 20,137,303 lakini waliopiga kura ni 8,626,283. Kati ya
kura hizo
zilizopigwa Rais Kikwete alipata kura 5,276,827, Dk. Slaa
kura 2,271,941 na Lipumba
kura 695,667.


Kwa takwimu hizo, na
kwa kigezo cha lojiki, Slaa anampiku
Lipumba kwa mbali. Ingawa katika siasa kuna mambo mengi ya
kuzingatia kabla
chama husika hakijateua mgombea urais wake, lakini utahitaji
maelezo ya
kuridhisha kumtosa mtu ambaye uchaguzi uliopita alipata kura
2,271,941 na
badala yake kumteua mtu ambaye aliambulia kura 695,667 tu.
Kwa hiyo, kwangu
mimi, uteuzi wa Dk. Slaa ungekuwa ni uteuzi sahihi awepo
Lowassa au kwenye
Upinzani au asiwepo.


Kiupambanaji, Dk. Slaa
ni zaidi ya Lowassa. Ana ujasiri. Kumbukumbu
zinaonyesha kwamba damu yake na ya mkewe Josephine (sijui
kama wameshaoana)
iliwahi kumwagika akipambana na dola kuwatetea wanyonge.
Aidha, ni mwadilifu,
mweledi, ana busara, na hana maamuzi ya jazba kama Lowassa
(rejea skandali ya
Richmond) au Magufuli.


Katika kipindi cha
miaka 15 iliyopita, Dk. Slaa amewaongoza
Watanzania (wakiwemo wabunge) kubadilisha kabisa mwelekeo wa
uwajibikaji wa
watawala wetu Tanzania. Aidha, amehangaika huku na kule
nchini kuwaamsha wapiga
kura usingizini ili wawatathmini watawala wao (siwaiti
viongozi) wakiwa na upeo
mkubwa wa ufahamu.


Ninadiriki kusema kuwa
hata kufungwa jela kwa hivi karibuni
kwa mawaziri wawili wa zamani – Daniel Yona na Basil
Mramba, ni matunda ya kazi
ya muda mrefu ya kupambana na ufisadi ya Dk. Slaa na wenzake
kadhaa pamoja na
vyombo vya habari.


Tofauti na wagombea
urais wengine ambao wangeweza kuteuliwa
kutoka Upinzani – Lowassa, Lipumba, Mbowe nk, Dk. Slaa
yeye anaingia katika
kinyang'anyiro hicho akiwa na rekodi safi ya nyuma ya
utendaji jimboni na hata
alipokuwa ndani ya Bunge. Hadi leo rekodi hiyo haijapata
kuchafuliwa na kashfa
yoyote ya ufisadi au nyingine yoyote kubwa.


Kama, mpaka sasa,
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaendelea
kuwa mfano wa kuigwa nchini wa halmashauri zinazochacharika
kuwaletea wananchi
wake maendeleo makubwa, ni kwa sababu ya msingi mkubwa wa
Dk. Willbroad Slaa
aliouweka akiwa mbunge wa jimbo hilo.


Ndugu zangu, kama
bunge sasa linachangamka na linasimama
kidete kupambana na ufisadi nchini (mfano Escrow), ni kwa
sababu huko nyuma
kulikuwa na kina Slaa ndani ya bunge hilo waliojitolea
"kufa kidogo" kutetea
wanyonge na ambao walionyesha ujasiri wa kutoiogopa serikali
kwa kuibana kweli
kweli. Hawa wa sasa wanafuata tu njia iliyoanzishwa na hao
waliowatangulia –
yaani Dk. Slaa na wenzake.


Ndugu zangu,
nihitimishe kwa kusisitiza mambo mawili. La
kwanza ni
kwamba Dk. Slaa ndiye
aliyestahili kuwa chaguo sahihi la kumkabili
Dk.
Magufuli, na si
Lowassa, Lipumba, Mbowe au Mbatia. La pili ni kwamba kwa
kumkubali Lowassa kuwa mmojawao, Chadema na Ukawa
'wameipoteza' kabisa agenda
ya ufisadi. Itabidi sasa wafunge midomo yao kuzungumzia vita
ya ufisadi, kwa
sababu sasa Watanzania wanaamini kuwa walikuwa wakibwabwaja
tu maneno lakini si
waumin wa kweli wa vita hiyo!


Niambieni; ni wapi
ambako kuna ushahidi kuwa Lowassa alipata
kukubali "kufa kidogo" kuwatetea wanyonge na masikini wa
nchi hii. Ni mjinga tu
ndiye asiyejua kwamba Lowassa ndiye chaguo la urais la
mabilionea wa Tanzania
ambao wengi wao mapesa yao hawakuyapata kihalali.


Hakuna namna yoyote
ambayo Lowassa anaweza kudai kuwa katika
patashika zake za kuusaka urais anawakilisha maslahi ya
masikini waliozagaa
vijijini! Tiketi yake ni ya mabilionea wenzake na ndiyo
atakaowawakilisha
kwenye kampeni. Mtu wa namna hiyo akiingia Ikulu, kamwe
hawezi kuwakumbuka
masikini wala wanyonge bali atawakumbuka mabilionea wenzake
waliomwingiza
Ikulu.


Rejeeni ile hafla yake
ya Arusha ya kutangaza nia ya kuwania
urais ilivyokuwa ya mapesa mengi ndo utaelewa
ninachomaanisha ninaposema ya
kuwa si mwakilishi wa masikini na wanyonge. Na ndiyo maana,
kwangu mimi, bado
nitaendelea kuamini ya kuwa The Chosen One kutoka Upinzani
wa kumkabili Dk.
Magufuli alistahili kuwa Dk. Slaa.


Ni bora CCM, ambayo
sasa inaanza kujirudi na kujisafisha kwa
kuwatosa watuhumiwa wa ufisadi miongoni mwao kuliko Chadema
na Ukawa ambao sasa
wanapokea makapi ya CCM yanayokimbia tuhuma za ufisadi.
Lowassa, kama
alivyokuwa mzigo kwa CCM, atakuwa tu mzigo kwa Chadema na
Ukawa yao! Time will
tell! Tafakari.


Raia Mwema

Toleo la 416

29 Jul 2015-





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment