Wednesday, 29 July 2015

Re: [wanabidii] Msimamo: Nitasimama na Majemedari Ninaowajua, Tuliopigana Vita Pamoja Nao.

Mtalinganisha sana na vitu ambavyo kwa namna nyingi wala havina uwiano wala havifanani. 



On Wednesday, 29 July 2015, 7:33, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:




(Pichani Mwalimu Nyerere akiwa na Majemedari Wake wakati wa Vita ya Kagera)

 Na Mwanakijiji
.
Neno la Leo: Unapoenda vitani unaenda na makamanda wapiganaji wako, makamanda wako na majemedari wako. Wapiganaji wako wanapoanguka hurudi nyuma unaendelea kusimama, makamanda wakijeruhiwa unawasaidia wanainuka mnaendelea mapambano, na majemedari wenu wakiumizwa mnaendelea kusimama nyuma yao na kuendelea kusonga mbele (charge).

Jemedari wa upinzani anapoamua kubadili kambi na kuja upande wenu hata akiwa maarufu kiasi gani KAMWE hamuwaondoi majemedari wenu na kumpa yeye ukumbi ati aongoze vita kwa sababu mnataka ushindi tu! Zaidi mtamtumia mtu huyo kwa ushauri zaidi, msaada wa maono kutokana na ujuzi wa kule anakotoka.

Ni kweli inawezekana mnautaka ushindi lakini ushindi hauji kwa "gharama yoyote"! Jamani hata vita ina kanuni zake - Rules of Engagement. Kuna baadhi ya mambo hata kama yanaweza kusaidia vita hayaruhusiwi vitani na yakifanyika matokeo yake yanaweza kuwa ni ya hatari sana na ndio maana kuna vitu kama Geneva Convention kusimamia kanuni hizi za vita.

Huwezi kusema ati unataka kushinda vita kwa gharama yoyote hata kama utaua wanawake, watoto na wazee, raia n.k Kusema "tunataka ushindi kwa gharama au namna yoyote" ni kufungua milango ya hatari sana kwani unaweza kujikuta unamkaribisha jemedari wa adui na kumuingiza hadi kwenye mipango yenu ya vita na akawashauri vizuri... na wenyewe mkafurahia hadi mtakapojikuta mmeingia kwenye mtego usioachia.

Ni kwa sababu hiyo, wakati vita tunasimama na makamanda na majemedari wetu tuliokuwa nao, tuliopigana vita pamoja, tuliojeruhiwa pamoja. We DO NOT LEAVE A MAN BEHIND! Tunaweza kuweka imani yetu kwa majemedari tunaowajua hata maisha yetu lakini tutakuwa tayari kufa kwa jemedari tusiyemjua ambaye tulisikia umahiri wake alipokuwa upande wa adui na jinsi alivyowatenda askari wetu walipoangukia mikononi mwake?

Tutakuwa na imani na jemedari aliyehamia kwetu wakati alipokuwa upande ule hakuzuia majeshi yake kuwatenda vibaya askari wetu na raia wetu? Wakati watoto wetu, mabinti na dada zetu, wake zetu na mama zetu wanapigwa na kuuawa na waandishi wetu wanaumizwa hakusimama upande ule kupinga au kuonesha kujali lakini leo aje upande wetu tumkumbatie ati kwa vile tunataka kushinda?

Lakini itakuwaje kama jemedari huyo anakuja na maafisa wake nawapiganaji wake ambao nao wanataka kuchukua nafasi za mbele. Watakuwa kweli wanapigania jeshi letu au wanapigania maslahi yao na nafasi zao? Na ikitokea tukashinda huyu jemedari mahili atakuwa kweli chini ya jeshi letu au itabidi tumfuate anakotaka yeye sasa? Na tukishindwa kweli tutaweza kumlaumu yeye kwa kushindwa kwetu wakati ni sisi wenyewe tulimfuata aje atuongoze vita ambayo tayari tulikuwa tunashinda chini ya majemedari wetu tuliotoka nao mbali?

Ukiniuliza mimi... nitasimama na majemedari ninaowajua hata kama hatutashinda vita lakini najua pamoja nao tumepigana hadi dakika ya mwisho. Jemedari mgeni akija na akatusaidia kushinda vita nyuma ya majemedari yetu mchango wake hautasahaulika. Jemedari mgeni akisimama nyuma ya makamanda wetu na kuunga mkono mapambano kwa kadiri ya uwezo wake tutakubali na kushukuru. Siyo kinyume cha hivyo.

NB: Iangalie hiyo picha juu halafu jiulize; kweli Watanzania wangemwelewa Nyerere na uongozi wa Taifa kumchukua Generali wa Idi Amin (amekosana na Idi Amin au vipi) halafu aje huku achukue nafasi za kina Mwita Marwa, Musuguli na wengine? Kwamba ati huyo Generali kwa vile alikuwa karibu sana na Idi Amin na maarufu sana akiwa Uganda basi atafaa kuongoza majeshi ya Tanzania? Tungeshangilia kweli kweli... kina Musuguli, Kyaro, Kiwelu, n.k wangemwelewa Nyerere ati kwa vile tulitaka kushinda vita "by any means necessary"? Siyo kwamba, pamoja na hela, vifaa n.k alivyokuwa navyo Idi Amin majenerali wetu wenye uzoefu na tulioawamini ndio waliotupatia ushindi?
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment