Thursday 30 July 2015

[wanabidii] Ama kweli SHETANI akizeeka hujifanya malaika

Ama kweli SHETANI akizeeka hujifanya malaika

Napata tabu,napata tabu sana kuwaelewa viongozi wangu wangu wa chama cha watu,chama pendwa kwa sasa.chama cha demokrasia na maendeleo..

Chama kilichojinadi kwa muda mrefu kuwa KINAPINGA UFISADI.
Chama kilichojitangaza KUCHUKIA RUSHWA.
Chama kilichojinadi kupiga vita UKIRITIMBA.
Chama kilichojinadi kuwa kina WATU MAKINI.
na mengine mengi.........

Watu tukakiamini,tukakipenda.
Masikini ya Mungu..
Yule mtu waliyemponda wao wenyewe kuwa ni FISADI,ANAJIMIRIKISHA ARDHI KINYUME NA SHERIA(wakati wafugaji na wakulima wakihangaika hawana ardhi ya kulima na kulishia).
Mtu ambaye AMEVUNJA WAZI WAZI KANUNI za chama chake cha zamani; usifanye kampeni..KAFANYA. Usitoe rushwa,KATOA.
Kati ya watu 40 yeye na wachache ndo hawajaridhika,JE,HII NDIO DEMOKRASIA?

kanuni za CHADEMA MTU KUGOMBEA UONGOZI ZINASEMAJE?
Mtu hata wiki kwenye chama hana wanampa URAIS..
NI HALALI KWELI?
kuna watu wana miaka zaidi ya mingi wanataka kugombea urais kwenye chama.KWA NINI MSIWAPE HAO? au hakukua na watu?

Wasomi,wazoefu... Mtu ALIJIUZURU mnamwita MSTAAFU.du! hivi kujiuzuru ni kustaafu?

Eti ametueleza vizuri kuhusu Richmond.
Alikuwa wapi kueleza miaka yote?
VIPI KAMA CCM INGEMPITISHA,ANGEYASEMA HAYO.

Anasema anayesema ye ni fisadi kama ana ushahidi.aende Mahakamani.
Nani aliyekuwa akisema yeye ni fisadi kama si CHADEMA?
anamaanisha chadema waende mahakamani?
Mgh! Haeleweki..

Pesa pesa pesa pesa.....

Yesu na utume wake wote alnunuliwa kwa pesa..

Viongozi wa juu wa CHADEMA wamenunuliwa na pesa za mafisadi.

Chademaaaa!!!!! Nilikiamini sana chama changu.. SIAMINI LEO KIMEKUWA NDIO KIMBILIO,TETEO NA TAKASO LA MAFASIDI,WATOA RUSHWA,WAKIRITIMBA NA WATU WANAOTAKA KUWA JUU YA SHERIA.WATU WASIOKUBALI MATOKEO(madikteta).


We mungu tulindie tu amani ya nchi yetu,
Wewe ndio kiongozi wetu wa kweli,
Viongozi wetu wa dunia hawaeleweki WANA NDIMI MBILI MBILI.
TENA VIGEUGEU...
Wanalazimisha mambo..

Ee mungu tuonyeshe haki ILIYO WAZI NA KWELI tuifate,na utuoneshe BATILI tuiache.

Mungu tupe kiongozi bora.
MUNGU IBARIKI TANZANIA

0 comments:

Post a Comment