Friday 31 July 2015

Re: [wanabidii] Lowassa ni mzigo, Slaa angekuwa chaguo sahihi!

Mm nadhani sisi wana-CCM wa kweli hatutakiwi kuendelea kuzungumzia hbr za EL na CDM kama wamefanya blunders au la. Tungehangaika na kupata wanachama wengine na kuachana wapinzani. Uchambuzi wwt wa kwenye mitandao hautujengei chama chetu. Siasa za Afrika zinafanana zote.
Kama mtakumbuka miaka ya hivi karibuni William Ruto alijiuzulu ukatibu mkuu wa KANU kwa sababu Mzee Moi alimpendekeza kijana Uhuru Kenyatta kuwa mgombea urais kupitia KANU. Matokeo chama Uhuru akashindwa na the same people 2007 walikuwa maadui wakubwa kiasi cha kusababisha vita vya ukabila huko kwao. Now the same people wanaongoza Kenya. Hata akina Amama Mbabazi na Daktari Byesigye walikuwa na Mu7 huko msituni now ni wapinzani. Bado kina Pierre Nkurunzinza na Agaton Rwasa wa Burundi ni hivyo hivyo. EL na CDM waliitana majina lkn kama tujuavyo wote ni wanasiasa na sio vigumu kufanya kazi pamoja.
Sioni cha kugombanisha watu kwenye mitandao. Ni afadhali kutumia muda kuzungumzia issues muhimu kitaifa badala ya kuzungumzia watu.
Kwanza hakuna mbaya absolutely au mtu mzuri bila kasoro.
CDM wameona potential ya EL wamemchukua naye pia ameona anaweza kufaidika kwa kuwa ukawa. Kwa hiyo kwao wao ni win win situation.
Sisi tuliopoteza ndio tutafute namna ya kukabiliana nao sio kuwapa faida kwa kusema mapungufu yao mtandaoni. Je wakiyaona wakarekebisha si watatushinda!!! Tuwe makini wapendwa

Sent from My Ipad

On 31 Jul 2015 13:14, "Ireneus Kakuru Mushongi" <ireneuskakurumushongi@gmail.com> wrote:
Moja ya makosa ambayo wanasiasa wa kiafrika wanafanya ni kutokuwa na washauri wa kisaikolojia. Wengi wanakuwa na washauri wa kiuchumi zaidi. (ni mawazo yangu binafsi) kuwa baada ya shughuli ya Dodoma, ENL alikuwa somehow stressed, aliathirika sana kisaikolojia. Kama angelipata vacation ya mwezi mzima huko Hawaii au popote mbali; akarefresh kabisa nje ya upepo huu wa Bongo na akawa yuko peke yake kwa muda, NA asintaentertain hizi "Pole Mzee lakini never give up"; baada ya mwezi mmoja, usingem-approach na habari au hadithi za UKAWA au ndugu zake na UKAWA akakuelewa; hapa wamecheza na wakati na akili yake ikiwa haijakaa sawasawa! Unless uniambie ENL ni comedian.

Yeye anadhani anautumia UKAWA kuachieve political ambition zake, but wao wana agenda zaidi ya kumtumia yeye kujitengeneza kisiasa zaidi. kupitia yeye watavuna wanachama, watapandisha status yao kisiasa; they know that he might not make it kwa urais; but watakuwa wamegain zaidi kuliko wangemsimamisha Dr au Proffessor kwenye mbio hizi. Next move itakuwa ya kuunganisha nguvu na kuunda chama kimoja kikubwa cha siasa after the expected popularity. In politics watapretend kumpenda; watamsifia sana (but kinafiki) but with hidden agendas...Huyu Bwana Mkubwa akija kustuka tayari wako mbali. Kwani Mrema ilikuwaje baada ya kuondoka CCM? Watu walikuwa wanasukuma gari kila pahali huku akiitwa Rais Rais but where did it end? Alikuwa despaired, akaanza kupelekwa mahakamani, and guess what... hadi alipobend tena, sasa ana kaposition ka ubunge at least kumkeep alive kisiasa; but is a pro-CCM. Siamini kwamba ENL sio mwanaCCM kwa ghafla hivi kwani pia si wa kwanza kufanya haya....but tusubiri tuone..


Omukunirwa Ireneus 


 

2015-07-31 2:26 GMT+03:00 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Email moja humu imekuwa hacked???
--------------------------------------------
On Fri, 7/31/15, 'Lesian Mollel' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

 Subject: Re: [wanabidii] Lowassa ni mzigo, Slaa angekuwa chaguo sahihi!
 To: wanabidii@googlegroups.com
 Date: Friday, July 31, 2015, 1:59 AM

 Ndio maana wana habar wkt mwingine
 mnachukiwa na watu mnaandika as if iko hvyo kumbe
 umepelekewa na maono yako,better u write bila kujichukulia
 kama wewe,analysis nayojua mimi, ni ile ambayo ni research
 based,i did journalism for 8 years nikaacha,mbwambo was my
 editor kasuku newspaper pale jet,sikudhani kama angeandika
 hv,kachemka kweli.ametumwa na fikra zake.
 Anyway tunaheshim mawazo yake na ionekane ni mawazo yake sio
 ndivyo ilivyo
 Lesian

 Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:

 Umeona, eeh? Naheshimu maandiko ya Mbwambo lakini
 katika hili amebugi.em
 Sent from my iPhone
 On Jul 30, 2015, at 8:48 AM, Telesphor Magobe <tmagobe@gmail.com>
 wrote:

 Mhu! Naona
 roho ya CCM ndani ya makala hii na hivyo inaegemea upande
 fulani na siyo uchambuzi huru.

 2015-07-30 15:21
 GMT+03:00 fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com>:


 Johnson Mbwambo
 Lowassa ni mzigo, Slaa
 angekuwa chaguo sahihi!


 WAKATI naandika makala
 hii, habari zilikuwa zimezagaa ya
 kuwa Umoja wa Vyama vya Upinzani nchini (Ukawa), na hasa
 Chadema walikuwa
 wamekubaliana kumpokea Edward Lowassa na kumfanya kuwa
 mgombea urais wao kwenye
 Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Nathubutu kueleza wazi kwamba hilo
 ni kosa ambalo
 watalijutia kwa miaka mingi.


 Sijui nini kilikuwa
 kinaendelea katika vichwa vya viongozi
 wa Ukawa wakati wakifanya maamuzi ya mwisho ya kumpokea
 Edward Lowassa na hata
 kumfikiria kuwa ndiye anayestahili kupeperusha bendera yao
 kumkabili Dk. John
 Magufuli wa chama tawala, CCM, kwenye patashika ya Oktoba ya
 kuwania kukamata
 dola.


 Najua ya kwamba
 'siasa ni mchezo mchafu', lakini bado
 najiuliza maswali kibao kichwani mwangu ya ni hoja zipi
 Chadema ilizizingatia
 katika kumkubali Lowassa – mtu ambaye chama hicho
 kilimuorodhesha katika ile
 orodha ya Mwembe Yanga ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini
 – List of shame
 (orodha ya aibu).

 Chadema haikupata
 kumuondoa Lowassa katika orodha hiyo. Na
 ndiyo sababu wengi wetu tumepigwa na butwaa kwa hatua yake
 ya ghafla ya
 kumkubali mtu huyo kuwa anakifaa chama hicho kubeba bendera
 yao ya kuwania
 urais.


 Je, ni kwa sababu labda
 ana maono (vision) ya namna ya
 kuikomboa nchi hii au ni kwa sababu tu ya mapesa yake? Au
 tuseme ni kwa sababu
 ya 'umaarufu' wake? Au labda ni kwa sababu ya uwezo wake
 kiutendaji? Au ni kwa
 sababu ya marafiki zake matajiri atakaohama nao? Vyovyote
 vile, umma unawadai
 viongozi wa Chadema na Ukawa majibu ya maswali haya.


 Hivi Chadema (achilia
 mbali CUF) inawezaje kusimama jukwaani
 na kumnadi urais (au hata kuwa naye tu jukwaani) mtu ambaye
 yumo katika orodha
 yao ya mafisadi papa nchini? Wataanzia wapi na wataficha
 wapi nyuso zao? Au
 labda ni kwa kuwa IQ ya Watanzania ni ya kiwango cha chini,
 na ndiyo maana
 wanaamini watasahau ya jana kuhusu mgombea urais huyo?


 Hivi nani asiyejua ya
 kuwa Lowassa anahamia Chadema si kwa
 sababu ya kukipenda chama hicho na sera zake, lakini ni kwa
 sababu ya kuikomoa
 CCM iliyomtosa? Hivi kweli mtu anayeingia chama kulipa
 visasi au kukikomoa
 chama chake cha zamani anaweza kuwa na faida yoyote kubwa na
 endelevu kwa chama
 hicho alichohamia na kwa Watanzania kwa ujumla? Tangu lini
 visasi binafsi na
 kukomoana vikachukua nafasi ya mustakabali wa taifa?


 Vyovyote vile, Chadema
 na Ukawa yao itabidi, kwenye kampeni
 ya urais waanze kwanza na kumsafisha Lowassa (sijui kwa
 sabuni gani) ndipo
 waeleze sera zao kwa wapiga kuwa. Itabidi kwanza wazifute
 hadharani kauli zote
 za nyuma ambazo ziko kwenye kumbukumbu walizozitamka dhidi
 ya Lowassa
 kumhusisha na ufisadi, na ndipo waanze kumnadi au hata
 kuhalalisha tu kuwa naye
 kwenye jukwaa wakati wa kampeni.


 Baba wa Taifa, Mwalimu
 Nyerere, alipata kusema ya kuwa mtu
 akishakuwa tu na tuhuma kubwa za ufisadi hafai kufikiriwa
 urais, na naamini ni
 kwa hoja hiyo hiyo CCM iliamua kumtosa Lowassa hata bila ya
 kufikisha jina lake
 kwenye vikao vya juu kabisa vya maamuzi – Kamati Kuu, NEC
 na Mkutano Mkuu.


 Sasa, ni 'maajabu'
 kwamba Chadema, badala ya kujisifu
 kwamba, kimechangia kuifanya CCM imtose urais mtu aliyekuwa
 kwenye orodha yao
 ya 'list of shame', ndicho hicho kinachompokea kwa
 mbwembwe – yaani mtu yule
 yule kiliyempiga vita kuwa ni fisadi!!! Jamani, ni kwa
 sababu ya mapesa yake tu
 au ni kwa sababu ya maslahi binafsi na si maslahi mapana ya
 chama na
 Watanzania?


 Nimedadisidadisi ni vipi
 Chadema na Ukawa walikubali
 kumpokea mtu ambaye chama tawala CCM kilimtosa kwa sababu ya
 tuhuma za ufisadi
 - mtu ambaye Chadema kilishiriki kueneza habari nchini nzima
 kuwa ni fisadi.

 Jibu nililopewa na
 ninalopewa ni kwamba eti Lowassa ni 'mwathirika' tu wa
 mfumo
 (system) wa kifisadi wa Serikali ya CCM. Eti sasa wanadai ya
 kuwa Lowassa ni
 msafi ila mfumo wa kifisadi ndiyo tatizo kuu linalopaswa
 kupigiwa kelele! Mbona
 haya hawakutueleza tangu mwanzo? Au ndo wameyajua baada ya
 yeye kutoswa na CCM?


 Lakini hapa kuna swali
 jingine. Huo mfumo (mimi nauita
 mtandao) uliwekwa na unaendeshwa na kina nani? Si kweli
 kwamba nyuma ya mfumo
 huo kuna watu na Lowassa, kama mmoja wa watu walioshika
 nafasi za juu za
 uongozi nchini, ni sehemu ya mfumo huo? Kweli

 Watanzania tumepoteza
 uwezo wa
 kufikiri (we have gone crazy)!

 Ndugu zangu, nasisitiza
 tena ya kwamba Chadema na Ukawa
 wamefanya kosa ambalo watalijutia. Nadiriki kusema ya kuwa
 kama kweli
 watamsimamisha Lowassa kuwa mgombea urais wao, basi
 wameshindwa uchaguzi wa
 Oktoba hata kabla hawajaingia kwenye kampeni zenyewe.

 Kama wamesahau,
 waulize
 kilichomkumba Augustine Mrema kwenye uchaguzi wa mwaka 1995
 baada ya kutoka CCM
 akiwa na huo unaoitwa 'umaarufu' ambao leo tunaaminishwa
 Lowassa anao hivi sasa
 nchini!

 Binafsi, sioni namna
 yoyote ambayo Rais Kikwete na CCM yake
 ataukabidhi urais kwa Lowassa Novemba mwaka huu.
 Ninachokiona ni kwamba sasa
 Kikwete na CCM yake watafanya kazi usiku na mchana
 kuhakikisha Lowassa hakamati
 Ikulu.
  CCM watapindua kila
 jiwe kuhakikisha Lowassa hawi rais wa nchi hata kama
 atasimama kwa tiketi ya Ukawa. Kama mnabisha, subirini
 Oktoba muone matokeo!

 Kwa mtazamo wangu,
 niliamini, na bado naamini ya kuwa 'The
 Chosen

 One' kutoka Ukawa
 alistahili kuwa Dk. Slaa wa Chadema. Takwimu za
 uchaguzi wa mwisho wa mwaka 2010 zinaonyesha ya kwamba
 walijiandikisha wapiga
 kura 20,137,303 lakini waliopiga kura ni 8,626,283. Kati ya
 kura hizo
 zilizopigwa Rais Kikwete alipata kura 5,276,827, Dk. Slaa
 kura 2,271,941 na Lipumba
 kura 695,667.


 Kwa takwimu hizo, na
 kwa kigezo cha lojiki, Slaa anampiku
 Lipumba kwa mbali. Ingawa katika siasa kuna mambo mengi ya
 kuzingatia kabla
 chama husika hakijateua mgombea urais wake, lakini utahitaji
 maelezo ya
 kuridhisha kumtosa mtu ambaye uchaguzi uliopita alipata kura
 2,271,941 na
 badala yake kumteua mtu ambaye aliambulia kura 695,667 tu.
 Kwa hiyo, kwangu
 mimi, uteuzi wa Dk. Slaa ungekuwa ni uteuzi sahihi awepo
 Lowassa au kwenye
 Upinzani au asiwepo.


 Kiupambanaji, Dk. Slaa
 ni zaidi ya Lowassa. Ana ujasiri. Kumbukumbu
 zinaonyesha kwamba damu yake na ya mkewe Josephine (sijui
 kama wameshaoana)
 iliwahi kumwagika akipambana na dola kuwatetea wanyonge.
 Aidha, ni mwadilifu,
 mweledi, ana busara, na hana maamuzi ya jazba kama Lowassa
 (rejea skandali ya
 Richmond) au Magufuli.


 Katika kipindi cha
 miaka 15 iliyopita, Dk. Slaa amewaongoza
 Watanzania (wakiwemo wabunge) kubadilisha kabisa mwelekeo wa
 uwajibikaji wa
 watawala wetu Tanzania. Aidha, amehangaika huku na kule
 nchini kuwaamsha wapiga
 kura usingizini ili wawatathmini watawala wao (siwaiti
 viongozi) wakiwa na upeo
 mkubwa wa ufahamu.


 Ninadiriki kusema kuwa
 hata kufungwa jela kwa hivi karibuni
 kwa mawaziri wawili wa zamani – Daniel Yona na Basil
 Mramba, ni matunda ya kazi
 ya muda mrefu ya kupambana na ufisadi ya Dk. Slaa na wenzake
 kadhaa pamoja na
 vyombo vya habari.


 Tofauti na wagombea
 urais wengine ambao wangeweza kuteuliwa
 kutoka Upinzani – Lowassa, Lipumba, Mbowe nk, Dk. Slaa
 yeye anaingia katika
 kinyang'anyiro hicho akiwa na rekodi safi ya nyuma ya
 utendaji jimboni na hata
 alipokuwa ndani ya Bunge. Hadi leo rekodi hiyo haijapata
 kuchafuliwa na kashfa
 yoyote ya ufisadi au nyingine yoyote kubwa.


 Kama, mpaka sasa,
 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaendelea
 kuwa mfano wa kuigwa nchini wa halmashauri zinazochacharika
 kuwaletea wananchi
 wake maendeleo makubwa, ni kwa sababu ya msingi mkubwa wa
 Dk. Willbroad Slaa
 aliouweka akiwa mbunge wa jimbo hilo.


 Ndugu zangu, kama
 bunge sasa linachangamka na linasimama
 kidete kupambana na ufisadi nchini (mfano Escrow), ni kwa
 sababu huko nyuma
 kulikuwa na kina Slaa ndani ya bunge hilo waliojitolea
 "kufa kidogo" kutetea
 wanyonge na ambao walionyesha ujasiri wa kutoiogopa serikali
 kwa kuibana kweli
 kweli. Hawa wa sasa wanafuata tu njia iliyoanzishwa na hao
 waliowatangulia –
 yaani Dk. Slaa na wenzake.


 Ndugu zangu,
 nihitimishe kwa kusisitiza mambo mawili. La
 kwanza ni
 kwamba Dk. Slaa ndiye
 aliyestahili kuwa chaguo sahihi la kumkabili
 Dk.
 Magufuli, na si
 Lowassa, Lipumba, Mbowe au Mbatia. La pili ni kwamba kwa
 kumkubali Lowassa kuwa mmojawao, Chadema na Ukawa
 'wameipoteza' kabisa agenda
 ya ufisadi. Itabidi sasa wafunge midomo yao kuzungumzia vita
 ya ufisadi, kwa
 sababu sasa Watanzania wanaamini kuwa walikuwa wakibwabwaja
 tu maneno lakini si
 waumin wa kweli wa vita hiyo!


 Niambieni; ni wapi
 ambako kuna ushahidi kuwa Lowassa alipata
 kukubali "kufa kidogo" kuwatetea wanyonge na masikini wa
 nchi hii. Ni mjinga tu
 ndiye asiyejua kwamba Lowassa ndiye chaguo la urais la
 mabilionea wa Tanzania
 ambao wengi wao mapesa yao hawakuyapata kihalali.


 Hakuna namna yoyote
 ambayo Lowassa anaweza kudai kuwa katika
 patashika zake za kuusaka urais anawakilisha maslahi ya
 masikini waliozagaa
 vijijini! Tiketi yake ni ya mabilionea wenzake na ndiyo
 atakaowawakilisha
 kwenye kampeni. Mtu wa namna hiyo akiingia Ikulu, kamwe
 hawezi kuwakumbuka
 masikini wala wanyonge bali atawakumbuka mabilionea wenzake
 waliomwingiza
 Ikulu.


 Rejeeni ile hafla yake
 ya Arusha ya kutangaza nia ya kuwania
 urais ilivyokuwa ya mapesa mengi ndo utaelewa
 ninachomaanisha ninaposema ya
 kuwa si mwakilishi wa masikini na wanyonge. Na ndiyo maana,
 kwangu mimi, bado
 nitaendelea kuamini ya kuwa The Chosen One kutoka Upinzani
 wa kumkabili Dk.
 Magufuli alistahili kuwa Dk. Slaa.


 Ni bora CCM, ambayo
 sasa inaanza kujirudi na kujisafisha kwa
 kuwatosa watuhumiwa wa ufisadi miongoni mwao kuliko Chadema
 na Ukawa ambao sasa
 wanapokea makapi ya CCM yanayokimbia tuhuma za ufisadi.
 Lowassa, kama
 alivyokuwa mzigo kwa CCM, atakuwa tu mzigo kwa Chadema na
 Ukawa yao! Time will
 tell! Tafakari.


 Raia Mwema

 Toleo la 416

 29 Jul 2015-





 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment