Thursday 30 July 2015

[wanabidii] BVR Registration - Kimenuka Kinyerezi NSSF

Niko kwenye zoezi la uandikishaji BVR Kinyerezi. Zoezi limeingia dosari nyingi ikiwemo kuisha karatasi za kuandikisha na baya zaidi ni pale afisa magereza aliyepewa fursa ya kujiandikisha na baadaye akajaribu kumleta ndugu yake kimabavu bila kufuata utaratibu.

Raia ambao wengi wao wamekuwepo kituoni tangu saa 9 alfajiri walikosa uvumilivu na kuzusha rabsha ambayo imepelekea zoezi kuhairishwa kwa muda.
Hadi ninapoandika haya zoezi limesimama na hatima yake haijulikani. Bado Tuko kwenye mstari na hatujui kama tutafanikiwa kupata usajiri. Mimi nimepewa namba tangu jumamosi ya wiki iliyopita.

Kuna mapungufu mengi sana ukiwa ni pamoja askari aliyepo kituoni kutotimiza wajibu wake sawasawa kwani hadi muda wote vurugu zinafanyika alikuwa pembeni tu anashuhudia.

Hii Ndiyo Tanzania!

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment