Wapendwa WaTanzania na Marafiki zetu popote mlipo,
Kwa niaba ya uongozi wa Tanzania Global Prayer Movement (TGPM), nachukua nafasi hii kuwashukuru wote walioungana nasi kuombea Kiti cha Uraisi na Ikulu siku ya Jumapili Julai 26 kwa kujiunga nasi kwa simu au kwa namna yoyote ile ingine. Maombi ya Jumapili kwenye simu yalikuwa mazito sana na uwepo wa Roho Mtakatifu ulionekana. Bwana apewe sifa sana.
Mafunuo yanayoendelea kujitokeza ni mazito na tunahitaji kuongeza bidii ya maombi. Wale wote walioguswa dunia nzima kuombea nchi yetu ya Tanzania inabidi wote kwa pamoja tuombe Mungu atupe mzigo wa maombi … YES, Mungu atupe mzigo wa maombi.
Kipindi hiki hadi Oktoba 25, siku ya uchaguzi, panahitajika maombi mazito ili nchi yetu tunayoipenda iweze kukombolewa. Mambo mengi ya kusambaratisha yako mbele yetu. Every prayer counts! Recruit as many as you to join the movement. Wapendwa tuombe bila kukoma. Huyu tunayemwomba ni Yesu Mungu aliye hai, Mungu asiyeshindwa, Mungu anayejibu kwa moto. Mpaka hapa tumefika amejihirisha kuwa nothing is impossible with God.
Naomba nitoe tahadhari. Kama kweli wewe Mungu amekugusa kuombea nchi yako, basi itabidi umpe Mungu wako a blank sheet yeye mwenyewe ajaze anachokusudia kwa nchi yetu ya Tanzania. Huwezi ukawa shabaki wa CCM or UKAWA halafu unaomba Mungu ampitishe mgombea wa chama fulani. We're serving a big God who knows what He is doing. We MUST pray with faith and according to God's will for our prayers to be answered. Ndiyo sababu TGPM tunaomba Mungu atupe viongozi wa ngazi zote (Raisi, wabunge na madiwani) walio na hofu ya Mungu bila kujali wanatoka chama gani na bila kujadili dini zao. Ila siku ya uchaguzi kila mmoja wetu kwa wale walio Tanzania watapiga kura kutokana na dhamiri yao.
Kuanzia Jumapili Julai 26 mpaka Jumapili Agosti 9 kila siku endelea kuombea maswala yafuatayo:
1) Omba Mungu akupe mzigo wa kuombea nchi yako ya Tanzania.
2) Ombea amani nchini wakati vyama vinakamilisha uchaguzi wa wagombea wao wa nafasi ya Raisi.
3) Ombea utakaso wa Kiti cha Uraisi wa Tanzania.
4) Ombea utakaso wa Ikulu ikiwa ni mahali anapofanyia kazi Raisi wa Tanzania.
5) Ombea utakaso wa viti vya wabunge na madiwani nchi nzima.
6) Ombea mgombea Uraisi wa UKAWA kama jina litakuwa limetoka. Kama bado, tutaendelea kuombea amani huku mchakachuo ukiendelea.
To join the conference call every Sunday, please dial (218) 895 9661 and passcode is 222555. The prayer starts at 9pm Eastern, 8pm central, 7pm Mountain or 6pm Pacific time.
For more information about Tanzania Global Prayer Movement (TGPM), please visit our website at:
Tafadhali sambaza huu ujumbe kwa watu wote unaowafahamu.
May the good Lord richly bless you!
Frank Mwakasisi, Ph.D.
Founder
Evangelist, Pastor, Teacher, and Preacher
Tanzania Global Prayer Movement - "Praying for the Power of the Resurrected Jesus Christ, our Lord to Transform Tanzania and spring forth Personal Renewal and Community Revival."
Chicago, Illinois
USA
Website: http://www.tgpm.org
Email: info@tgpm.org
From: Dr. Frank Mwakasisi [mailto:mwakasisi@tgpm.org]
Sent: Friday, July 24, 2015 6:53 PM
To: 'Tanzania Global Prayer Movement'
Subject: Maombi ya Utakaso wa Ikulu na Kiti cha Uraisi
Wapendwa WaTanzania na Marafiki zetu popote mlipo,
Kwa niaba ya uongozi wa Tanzania Global Prayer Movement (TGPM), natoa shukrani za dhati kwa wale wote walioungana nasi kupitia simu kwenye maombi ya Jumapili iliyopita. Tunawashukuru pia wale walioomba kwa wakati wao popote pale duniani. Jumapili iliyopita tuliombea:
1) Usalama wa mgombea Uraisi kupitia chama cha CCM.
2) Amani katika UKAWA huku wakiendelea kuchakanua mgombea wao wa Uraisi.
3) Tamko la Raisi Obama kuhusiana na Uhamiaji hapa Marekani.
Tuendelee kuombea hayo mambo matatu kwani yote bado ni nyeti. Endelea kuombea usalama wa Dr. Magufuli.
Kuanzia Jumapili ijayo yaani kesho kutwa Mungu ametupa mzigo wa maombi kulenga vitu vikubwa vitatu:
1) Utakaso wa Kiti cha Uraisi wa Tanzania
2) Utakaso wa Ikulu ikiwa ni mahali anapofanyia kazi Raisi wa Tanzania
3) Mgombea Uraisi wa UKAWA kama jina litakuwa limetoka. Kama bado, tutaendelea kuombea amani huku mchakachuo ukiendelea.
Bila kwenda ndani zaidi, maono yaliyotolewa yanaonyesha kafara nyingi zilizotolewa kwenye nguvu ya giza na kuchafua kiti cha Urahisi na eneo analofanyia kazi yaani Ikulu. Wapendwa tumepewa mzigo wa kuombea nchi yetu ili Mungu ajiinulie mtu wake mwenye hofu ya Mungu atakayeongoza Tanzania. Maono yanaonyesha kuwa huyo mtu hata akawa na hofu ya Mungu, atapata shida sana kufanya kazi yake kama hatutaomba utakaso wa hayo mambo mawili. Mpendwa haya ni maswala nyeti na yanahitaji msukumo mzito wa kiroho wa maombi kuweza kuisukuma hiyo giza inayozunguka hayo maeneo mawili. Maombi ya haya maswala si lelemama. Omba Mungu akupe mzigo wa kuyaombea.
Hizi dondoo mpya za maombi tutaanza kuombea siku ya Jumapili Julai 26. Vile vile nitaomba kila mtu kuendelea kuombea kwa wakati wako kila siku mpaka Jumapili Agosti 2.
To join the conference call, please dial (218) 895 9661 and passcode is 222555. The prayer starts at 9pm Eastern, 8pm central, 7pm Mountain or 6pm Pacific time.
For more information about Tanzania Global Prayer Movement (TGPM), please visit our website at:
Tafadhali sambaza huu ujumbe kwa watu wote unaowafahamu.
Neema ya Bwana ikufunike na kukushindia daima.
Frank Mwakasisi, Ph.D.
Founder
Evangelist, Pastor, Teacher, and Preacher
Tanzania Global Prayer Movement - "Praying for the Power of the Resurrected Jesus Christ, our Lord to Transform Tanzania and spring forth Personal Renewal and Community Revival."
Chicago, Illinois
USA
Website: http://www.tgpm.org
Email: info@tgpm.org
_______________________________________________
Prayers mailing list
Prayers@tgpm.org
http://tgpm.org/mailman/listinfo/prayers_tgpm.org
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment