Wednesday, 29 July 2015

Re: [wanabidii] TULIOMWITA LOWASSA FISADI TUMUOMBE RADHI

Kila anayetubu kwa dhati husamehewa Nkya. Lakini uwe mwangalifu na siasa. Umesikiliza upande mmoja tu kwamba EL alipewa amri ya simu, kutoka juu, kupitia kwa Katibu Mkuu kwamba mkataba usivunjwe. Haingii akilini katika taratibu za utawala kupokea maagizo na kutekeleza katika mtiririko huu! Agizo haliendi hivyo, na mimi binafsi siwezi kutekeleza agizo la jinsi hii. Je anayesemekana alitoa agizo akisema hajawahi kupiga simu kuzuia kuvunja mkataba? Na hii inawezekana sana katika hali ya mambo sasa hivi - kurukana! Nani atakuwa mkweli? Ni kupakana matope, tupate upande mwingine wa shilingi, kwamba ni kweli lilikuwa agizo? Kwa nini EL haku test authenticity ya agizo hilo? Unaridhika na maelezo/maagizo ya subordinate wako? 

Please


From: 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Cc: WANA BIDII <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, July 29, 2015 4:43 PM
Subject: [wanabidii] TULIOMWITA LOWASSA FISADI TUMUOMBE RADHI


Nimemsikiliza Edward  Lowassa  kwenye you tube tuliyowekewa humu jukwaani akiulizwa maswali na wanahabari kuhusu kashfa ya Richmond iliyotokea alipokuwa Waziri Mkuu miaka minane iliyopita. Kulingana na  majibu aliyoyatoa hata mimi kama mwanahabari niliwahi kumwita fisadi kwa sababu ya  kashfa hiyo. Lakini kulingana na maelezo aliyoyatoa ninakiri nilifanya dhambi maana kumsingizia mtu uongo ni dhambi na binafsi baada ya kusikia upande wake mimi kwa upande wangu namuomba radhi.
 
Kumbe kinara wa  kashfa ya Richmond alikuwa bosi wake. Lo!  Sasa inaingia akilini ni kwa nini TOR za Mwakyembe hakikumuweka Lowassa kama sample ya kuhojiwa kashfa ya Richmond ilipotokea. Lakini kwa unyenyekevu Lowassa alijiuzulu kuinusuru serikali nzima  isianguke. Mungu mwema miaka minane  baadaye ukweli kamili wa Richmond unajulikana. Kama ulichokisema ni kweli Lowassa, Mungu atakupigania kwa sababu ni wewe  na Mzee Mwinyi peke yenu mna rekodi ya kujiuzulu kuonyesha uwajibikaji kutokana na nafasi zenu na siyo kosa mlilolitenda  ninyi wenyewe. Viongozi wengine mpaka umma upige kelele sana ndipo wajibaraguze kujiuzulu mfano kashfa ya escrow 2014. Sasa ninaelewa ni kwa nini baadhi ya watu wana hofu baada ya LOwassa  kukubaliwa na UKAWA kuwa mgombea Urais.

Namshukuru sana aliyetuwekea hii you-tube huku jukwaani maana baadhi yetu ambao hatuko site tungeweza kuendelea kufanya uchambuzi wetu kwa kutumia habari nusu nusu tulizopewa miaka iliyopita kuhusu kashfa ya Richmond.

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment