Thursday 30 July 2015

Re: [wanabidii] Lowassa ni mzigo, Slaa angekuwa chaguo sahihi!

Mama nkya,mbwambo hapo ameandika kwa mawazo yake na sivyo ilivyo,namkatalia kabisa....tuhumu maana yake nini,letene wansheria hapa kutuhumiwa si mkosaji mzee mbwambo
Pili lowasa kalisema hili vzr juzi au hakulisikia,he did apolitical renponsibility,msikilize mh lissu amelifafanua pia vzr,msikilize mh lissu jana kaeleza what they meant by list of shame.....
Kiukweli mbwambo kaandika not analytically but with bias,na hapo ndo napomshangaa nae amekurupuka kidogo boss wang wa zamani jet
Jingine wanasiasa ni tofauti kabisa na wana habari au wananchi,we dont have permenet enemy in politics
Pia kumbuka cdm wana watu wanaojua kuanalyse mambo na wamesema wamelete wajuzi hao toka nje,na ni upepo ndio ulio muuza lowasa,he has people at his back,he has mass people,he cn bring change....kidogo mzee slaa ashaanza kuchuja ila mbwambo halion kabisa na anabishana na tafit mbambali
So simuungi mkono mr mbwambo for the above small arguments
Nawasilisha
Lesian

'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

>Johnson Mbwambo, nakupongeza kwa mara ya pili. Unafanya unafanya kazi ya nchi. Mungu akubariki sana.
>Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
>
>--------------------------------------------
>On Thu, 7/30/15, Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com> wrote:
>
> Subject: Re: [wanabidii] Lowassa ni mzigo, Slaa angekuwa chaguo sahihi!
> To: "WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Thursday, July 30, 2015, 1:53 PM
>
> Hii
> inafurahisha miaka ya nyuma watanzania tuliwekwa kwenye
> kundi la wavivu wa kusoma.
> Wanabidii tulijadili sana hili na cafe
> ikaanzishwa pale mikocheni sijui kama bado ipo.
> Jinsi nanavyosoma makala ndefu ndefu za siasa
> najiuliza vipaji hivi vingetumika kuandika uhamasishaji
> maendeleo na wasomi wetu wakasoma kama wanavyoshabikia
> sihasa tungeenda mbali
> On Jul 30, 2015 7:21 AM,
> "fadhil fadhil" <fadhil.fadhil96@gmail.com>
> wrote:
>
>
> Johnson Mbwambo
> Lowassa ni mzigo, Slaa
> angekuwa chaguo sahihi!
>
>
> WAKATI naandika makala hii,
> habari zilikuwa zimezagaa ya
> kuwa Umoja wa Vyama vya Upinzani nchini (Ukawa), na hasa
> Chadema walikuwa
> wamekubaliana kumpokea Edward Lowassa na kumfanya kuwa
> mgombea urais wao kwenye
> Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Nathubutu kueleza wazi kwamba hilo
> ni kosa ambalo
> watalijutia kwa miaka mingi.
>
>
> Sijui nini kilikuwa
> kinaendelea katika vichwa vya viongozi
> wa Ukawa wakati wakifanya maamuzi ya mwisho ya kumpokea
> Edward Lowassa na hata
> kumfikiria kuwa ndiye anayestahili kupeperusha bendera yao
> kumkabili Dk. John
> Magufuli wa chama tawala, CCM, kwenye patashika ya Oktoba ya
> kuwania kukamata
> dola.
>
>
> Najua ya kwamba 'siasa ni
> mchezo mchafu', lakini bado
> najiuliza maswali kibao kichwani mwangu ya ni hoja zipi
> Chadema ilizizingatia
> katika kumkubali Lowassa – mtu ambaye chama hicho
> kilimuorodhesha katika ile
> orodha ya Mwembe Yanga ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini
> – List of shame
> (orodha ya aibu).
>
> Chadema haikupata
> kumuondoa Lowassa katika orodha hiyo. Na
> ndiyo sababu wengi wetu tumepigwa na butwaa kwa hatua yake
> ya ghafla ya
> kumkubali mtu huyo kuwa anakifaa chama hicho kubeba bendera
> yao ya kuwania
> urais.
>
>
> Je, ni kwa sababu labda
> ana maono (vision) ya namna ya
> kuikomboa nchi hii au ni kwa sababu tu ya mapesa yake? Au
> tuseme ni kwa sababu
> ya 'umaarufu' wake? Au labda ni kwa sababu ya uwezo wake
> kiutendaji? Au ni kwa
> sababu ya marafiki zake matajiri atakaohama nao? Vyovyote
> vile, umma unawadai
> viongozi wa Chadema na Ukawa majibu ya maswali haya.
>
>
> Hivi Chadema (achilia mbali
> CUF) inawezaje kusimama jukwaani
> na kumnadi urais (au hata kuwa naye tu jukwaani) mtu ambaye
> yumo katika orodha
> yao ya mafisadi papa nchini? Wataanzia wapi na wataficha
> wapi nyuso zao? Au
> labda ni kwa kuwa IQ ya Watanzania ni ya kiwango cha chini,
> na ndiyo maana
> wanaamini watasahau ya jana kuhusu mgombea urais huyo?
>
>
> Hivi nani asiyejua ya kuwa
> Lowassa anahamia Chadema si kwa
> sababu ya kukipenda chama hicho na sera zake, lakini ni kwa
> sababu ya kuikomoa
> CCM iliyomtosa? Hivi kweli mtu anayeingia chama kulipa
> visasi au kukikomoa
> chama chake cha zamani anaweza kuwa na faida yoyote kubwa na
> endelevu kwa chama
> hicho alichohamia na kwa Watanzania kwa ujumla? Tangu lini
> visasi binafsi na
> kukomoana vikachukua nafasi ya mustakabali wa taifa?
>
>
> Vyovyote vile, Chadema na
> Ukawa yao itabidi, kwenye kampeni
> ya urais waanze kwanza na kumsafisha Lowassa (sijui kwa
> sabuni gani) ndipo
> waeleze sera zao kwa wapiga kuwa. Itabidi kwanza wazifute
> hadharani kauli zote
> za nyuma ambazo ziko kwenye kumbukumbu walizozitamka dhidi
> ya Lowassa
> kumhusisha na ufisadi, na ndipo waanze kumnadi au hata
> kuhalalisha tu kuwa naye
> kwenye jukwaa wakati wa kampeni.
>
>
> Baba wa Taifa, Mwalimu
> Nyerere, alipata kusema ya kuwa mtu
> akishakuwa tu na tuhuma kubwa za ufisadi hafai kufikiriwa
> urais, na naamini ni
> kwa hoja hiyo hiyo CCM iliamua kumtosa Lowassa hata bila ya
> kufikisha jina lake
> kwenye vikao vya juu kabisa vya maamuzi – Kamati Kuu, NEC
> na Mkutano Mkuu.
>
>
> Sasa, ni 'maajabu'
> kwamba Chadema, badala ya kujisifu
> kwamba, kimechangia kuifanya CCM imtose urais mtu aliyekuwa
> kwenye orodha yao
> ya 'list of shame', ndicho hicho kinachompokea kwa
> mbwembwe – yaani mtu yule
> yule kiliyempiga vita kuwa ni fisadi!!! Jamani, ni kwa
> sababu ya mapesa yake tu
> au ni kwa sababu ya maslahi binafsi na si maslahi mapana ya
> chama na
> Watanzania?
>
>
> Nimedadisidadisi ni vipi
> Chadema na Ukawa walikubali
> kumpokea mtu ambaye chama tawala CCM kilimtosa kwa sababu ya
> tuhuma za ufisadi
> - mtu ambaye Chadema kilishiriki kueneza habari nchini nzima
> kuwa ni fisadi.
>
> Jibu nililopewa na ninalopewa
> ni kwamba eti Lowassa ni 'mwathirika' tu wa mfumo
> (system) wa kifisadi wa Serikali ya CCM. Eti sasa wanadai ya
> kuwa Lowassa ni
> msafi ila mfumo wa kifisadi ndiyo tatizo kuu linalopaswa
> kupigiwa kelele! Mbona
> haya hawakutueleza tangu mwanzo? Au ndo wameyajua baada ya
> yeye kutoswa na CCM?
>
>
> Lakini hapa kuna swali
> jingine. Huo mfumo (mimi nauita
> mtandao) uliwekwa na unaendeshwa na kina nani? Si kweli
> kwamba nyuma ya mfumo
> huo kuna watu na Lowassa, kama mmoja wa watu walioshika
> nafasi za juu za
> uongozi nchini, ni sehemu ya mfumo huo? Kweli
>
> Watanzania tumepoteza uwezo
> wa
> kufikiri (we have gone crazy)!
>
> Ndugu zangu, nasisitiza
> tena ya kwamba Chadema na Ukawa
> wamefanya kosa ambalo watalijutia. Nadiriki kusema ya kuwa
> kama kweli
> watamsimamisha Lowassa kuwa mgombea urais wao, basi
> wameshindwa uchaguzi wa
> Oktoba hata kabla hawajaingia kwenye kampeni zenyewe.
>
> Kama
> wamesahau, waulize
> kilichomkumba Augustine Mrema kwenye uchaguzi wa mwaka 1995
> baada ya kutoka CCM
> akiwa na huo unaoitwa 'umaarufu' ambao leo tunaaminishwa
> Lowassa anao hivi sasa
> nchini!
>
> Binafsi, sioni namna
> yoyote ambayo Rais Kikwete na CCM yake
> ataukabidhi urais kwa Lowassa Novemba mwaka huu.
> Ninachokiona ni kwamba sasa
> Kikwete na CCM yake watafanya kazi usiku na mchana
> kuhakikisha Lowassa hakamati
> Ikulu.
> CCM
> watapindua kila jiwe kuhakikisha Lowassa hawi rais wa nchi
> hata kama
> atasimama kwa tiketi ya Ukawa. Kama mnabisha, subirini
> Oktoba muone matokeo!
>
> Kwa mtazamo wangu,
> niliamini, na bado naamini ya kuwa 'The
> Chosen
>
> One' kutoka Ukawa
> alistahili kuwa Dk. Slaa wa Chadema. Takwimu za
> uchaguzi wa mwisho wa mwaka 2010 zinaonyesha ya kwamba
> walijiandikisha wapiga
> kura 20,137,303 lakini waliopiga kura ni 8,626,283. Kati ya
> kura hizo
> zilizopigwa Rais Kikwete alipata kura 5,276,827, Dk. Slaa
> kura 2,271,941 na Lipumba
> kura 695,667.
>
>
> Kwa takwimu hizo, na kwa
> kigezo cha lojiki, Slaa anampiku
> Lipumba kwa mbali. Ingawa katika siasa kuna mambo mengi ya
> kuzingatia kabla
> chama husika hakijateua mgombea urais wake, lakini utahitaji
> maelezo ya
> kuridhisha kumtosa mtu ambaye uchaguzi uliopita alipata kura
> 2,271,941 na
> badala yake kumteua mtu ambaye aliambulia kura 695,667 tu.
> Kwa hiyo, kwangu
> mimi, uteuzi wa Dk. Slaa ungekuwa ni uteuzi sahihi awepo
> Lowassa au kwenye
> Upinzani au asiwepo.
>
>
> Kiupambanaji, Dk. Slaa ni
> zaidi ya Lowassa. Ana ujasiri. Kumbukumbu
> zinaonyesha kwamba damu yake na ya mkewe Josephine (sijui
> kama wameshaoana)
> iliwahi kumwagika akipambana na dola kuwatetea wanyonge.
> Aidha, ni mwadilifu,
> mweledi, ana busara, na hana maamuzi ya jazba kama Lowassa
> (rejea skandali ya
> Richmond) au Magufuli.
>
>
> Katika kipindi cha miaka 15
> iliyopita, Dk. Slaa amewaongoza
> Watanzania (wakiwemo wabunge) kubadilisha kabisa mwelekeo wa
> uwajibikaji wa
> watawala wetu Tanzania. Aidha, amehangaika huku na kule
> nchini kuwaamsha wapiga
> kura usingizini ili wawatathmini watawala wao (siwaiti
> viongozi) wakiwa na upeo
> mkubwa wa ufahamu.
>
>
> Ninadiriki kusema kuwa hata
> kufungwa jela kwa hivi karibuni
> kwa mawaziri wawili wa zamani – Daniel Yona na Basil
> Mramba, ni matunda ya kazi
> ya muda mrefu ya kupambana na ufisadi ya Dk. Slaa na wenzake
> kadhaa pamoja na
> vyombo vya habari.
>
>
> Tofauti na wagombea urais
> wengine ambao wangeweza kuteuliwa
> kutoka Upinzani – Lowassa, Lipumba, Mbowe nk, Dk. Slaa
> yeye anaingia katika
> kinyang'anyiro hicho akiwa na rekodi safi ya nyuma ya
> utendaji jimboni na hata
> alipokuwa ndani ya Bunge. Hadi leo rekodi hiyo haijapata
> kuchafuliwa na kashfa
> yoyote ya ufisadi au nyingine yoyote kubwa.
>
>
> Kama, mpaka sasa, Halmashauri
> ya Wilaya ya Karatu inaendelea
> kuwa mfano wa kuigwa nchini wa halmashauri zinazochacharika
> kuwaletea wananchi
> wake maendeleo makubwa, ni kwa sababu ya msingi mkubwa wa
> Dk. Willbroad Slaa
> aliouweka akiwa mbunge wa jimbo hilo.
>
>
> Ndugu zangu, kama bunge sasa
> linachangamka na linasimama
> kidete kupambana na ufisadi nchini (mfano Escrow), ni kwa
> sababu huko nyuma
> kulikuwa na kina Slaa ndani ya bunge hilo waliojitolea
> "kufa kidogo" kutetea
> wanyonge na ambao walionyesha ujasiri wa kutoiogopa serikali
> kwa kuibana kweli
> kweli. Hawa wa sasa wanafuata tu njia iliyoanzishwa na hao
> waliowatangulia –
> yaani Dk. Slaa na wenzake.
>
>
> Ndugu zangu, nihitimishe kwa
> kusisitiza mambo mawili. La
> kwanza ni
> kwamba Dk. Slaa ndiye
> aliyestahili kuwa chaguo sahihi la kumkabili
> Dk.
> Magufuli, na si Lowassa,
> Lipumba, Mbowe au Mbatia. La pili ni kwamba kwa
> kumkubali Lowassa kuwa mmojawao, Chadema na Ukawa
> 'wameipoteza' kabisa agenda
> ya ufisadi. Itabidi sasa wafunge midomo yao kuzungumzia vita
> ya ufisadi, kwa
> sababu sasa Watanzania wanaamini kuwa walikuwa wakibwabwaja
> tu maneno lakini si
> waumin wa kweli wa vita hiyo!
>
>
> Niambieni; ni wapi ambako
> kuna ushahidi kuwa Lowassa alipata
> kukubali "kufa kidogo" kuwatetea wanyonge na masikini wa
> nchi hii. Ni mjinga tu
> ndiye asiyejua kwamba Lowassa ndiye chaguo la urais la
> mabilionea wa Tanzania
> ambao wengi wao mapesa yao hawakuyapata kihalali.
>
>
> Hakuna namna yoyote ambayo
> Lowassa anaweza kudai kuwa katika
> patashika zake za kuusaka urais anawakilisha maslahi ya
> masikini waliozagaa
> vijijini! Tiketi yake ni ya mabilionea wenzake na ndiyo
> atakaowawakilisha
> kwenye kampeni. Mtu wa namna hiyo akiingia Ikulu, kamwe
> hawezi kuwakumbuka
> masikini wala wanyonge bali atawakumbuka mabilionea wenzake
> waliomwingiza
> Ikulu.
>
>
> Rejeeni ile hafla yake ya
> Arusha ya kutangaza nia ya kuwania
> urais ilivyokuwa ya mapesa mengi ndo utaelewa
> ninachomaanisha ninaposema ya
> kuwa si mwakilishi wa masikini na wanyonge. Na ndiyo maana,
> kwangu mimi, bado
> nitaendelea kuamini ya kuwa The Chosen One kutoka Upinzani
> wa kumkabili Dk.
> Magufuli alistahili kuwa Dk. Slaa.
>
>
> Ni bora CCM, ambayo sasa
> inaanza kujirudi na kujisafisha kwa
> kuwatosa watuhumiwa wa ufisadi miongoni mwao kuliko Chadema
> na Ukawa ambao sasa
> wanapokea makapi ya CCM yanayokimbia tuhuma za ufisadi.
> Lowassa, kama
> alivyokuwa mzigo kwa CCM, atakuwa tu mzigo kwa Chadema na
> Ukawa yao! Time will
> tell! Tafakari.
>
>
> Raia Mwema
>
> Toleo la 416
>
> 29 Jul 2015-
>
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>  
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>  
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and
> Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>  
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
> kudhibitisha ukishatuma
>
>  
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and
> Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>
>--
>Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>---
>You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment