Friday 31 July 2015

[wanabidii] UKO WAPI UHALALI WA UKAWA



Uko wapi uhalali wa Ukawa?

KUFUNGASHA virago kwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond, Edward Lowassa, kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenda Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na hatimaye umoja wa vyama vinne vya upinzani, maarufu kwa jina la Ukawa kunaibua mjadala mzito wa kisiasa nchini.


Kwa kuzingatia taarifa rasmi ya Ukawa iliyotolewa Jumatatu wiki hii kuhusu kumkaribisha kwao rasmi (kwa mikono miwili) mwanasiasa huyo, Lowassa sasa ndiye nembo ya umoja huo. Sasa ndiye kinara wa kuivusha Ukawa hadi Ikulu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa maneno mengine, ni kwamba sasa Lowassa ndiye kinara wa siasa za upinzani nchini.


Huyu ndiye Lowassa yule yule ambaye Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wibroad Slaa, amekuwa akimtangaza mara kwa mara katika majukwaa kwamba si kiongozi mwadilifu na wakati mwingine akitumia maneno makali kwamba ni fisadi.


Kwa kipindi chote cha kung'aa kwa Dk. Slaa katika majukwaa ya kisiasa, sambamba na kukua kwa siasa za upinzani nchini, Lowassa ametajwa kuwa miongoni mwa vinara wa tuhuma za ufisadi miongoni mwa wanaCCM.


Ujumbe uliokuwa ukitoka jukwaa la siasa za upinzani, hususan chama kikuu cha upinzani – Chadema, na hata viongozi wengine akiwamo Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, ni kwamba CCM si wasafi – ni mafisadi na miongoni mwao ni Lowassa. Kwa mfano, tukio mojawapo lililoibua tuhuma hizo ni mkutano wa hadhara wa Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam, Septemba 15, mwaka 2008.


Miaka saba baadaye tangu tukio hilo la Mwembe Yanga, mambo yanataka kugeuzwa. Vyovyote itakavyokuwa, ni kwamba sasa wanasiasa wa upinzani wanapaswa kuchagua moja kati ya mawili na kwa kweli, mojawapo wamekwishakuchagua na kubakiwa na jambo moja jingine tu. Jambo hilo ni kukana yale waliyowaeleza Watanzania kuhusu Lowassa.


Naam, sasa wanalojukumu la kukiri uwongo wao mbele ya umma kwamba Lowassa si fisadi, bali ni mtu safi na mwadilifu. Wasiishie kusema hayo tu, waruhusu maswali ya wananchi aliyetumia vizuri fedha za ujenzi wa ofisi ya ubunge katika Jimbo la Monduli.


Ni dhana dhaifu, kuamini kwamba jukumu la msingi ni kuiondoa CCM madarakani bila kutafakari timu inayoshiriki katika uondoaji huo imebeba taswira gani mbele ya jamii, taswira ambayo imetengenezwa na wanasiasa wenyeji ndani ya upinzani ambako Lowassa amejiunga.















--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment