Monday, 20 July 2015

Re: [wanabidii] SILAHA ZILIZOPORWA NA MAJAMBAZI KITUO CHA POLISI SITAKISHARI ZAKAMATWA

Ninadhani askari wetu wameonyesha uwezo wao na kuwa wanaweza kuamua kutotaniwa.
Kile kikosi maalum inaonyesha ni mahili sana. Basi iko haja ya kutoa mafunzo hayo kwa askari wetu wote. Umahilim huo ungeonyeshwa kituoni huenda majambazi wangekuwa wanapita mbali na vituo hivyo. sasa hii ya askari wetu kufa ndio tunaona ushujaa wa askari wetu nayo ina walakini. Ipo haja ya kuwafunza askari wetu kuwa more professional.
--------------------------------------------
On Mon, 7/20/15, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] SILAHA ZILIZOPORWA NA MAJAMBAZI KITUO CHA POLISI SITAKISHARI ZAKAMATWA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, July 20, 2015, 7:06 PM

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
20/07/2015
SILAHA ZILIZOPORWA NA MAJAMBAZI KITUO CHA POLISI SITAKISHARI
ZAKAMATWA,
KATIKA MAPAMBANO, MAJAMBAZI WATATU WAUAWA, WAWILI WAKAMATWA.
Oparesheni kali yakupambana na makosa mbalimbali ya uhalifu
wakutumia silaha za moto inaendelea jijini Dar es Salaam kwa
kushirikiana kwa karibu na mikoa jirani.
Katika tukio la hivi karibuni tarehe 12/07/2015 kundi la
majambazi waliokadiriwa kufikia 16 hadi 18 walivamia kituo
cha Polisi Sitakishari wakati wa usiku na kisababisha vifo
vya askari wanne na raia watatu pamoja na uporaji wa silaha
kadhaa na risasi.
Mara baada ya tukio hilo oparesheni kali ya usiku na mchana
kwa ushirikiano wa vikosi mbali mbali lianzishwa.
Matokeo ya oparesheni hiyo nikamaifuatavyo:
Mnamo tarehe 17/07/2015 zilipatikana taarifa zakuaminika
kwamba huko maeneo ya TOANGOMA mkoa wa kipolisi Temeke
kulikuwa na majambazi waliohusika kwenye tukio la
Sitakishari wakijiandaa kufanyatukio la uhalifu.
KikosiMaalum (TASK FORCE) kiliendaeneo la tukiona kuweka
mtego ilikuwanasa washukiwa.
Kutokana na taarifa zilizokuwepo askari wakikosi hicho
waliwasimamisha watu watano waliokuwa wamepakizana katika
pikipiki mbili lakini walikaidi kusimama na badala yake
mapambano makali ya kurushiana risasi yalianza.
Watuhumiwa watano walikamatwa na watatu kati yao walikuwa
wamejeruhiwa vibaya na hivyo walifariki dunia wakiwa njiani
kukimbizwa hospitali.
Majina ya waliofariki ni kama ifuatavyo:
ABBAS S/O HASHIM,
Mkazi wa mbagala.
YASINI,
Mkazi wa Kitunda Kivule.
SAID,
Mkazi Kitunda Kivule/Kijiji cha Mandimkongo Mkuranga.
Watuhumiwa wawili ambao ni
RAMADHANI S/O HAMIS ULATULE,Miaka 15, Mkazi wa kijiji cha
Mandimkongo Mkurangana
OMARY S/O OMARY AMOUR, Miaka 24, Mkazi wa Mbagala
Kimbangulile walipatikana na kuhojiwa.
Katika tukio hilo ilipatika na bunduki moja aina ya SMG
ambayo namba zake zilifutwa ikiwa na risasi 25.
Katika mwendelezo wa oparesheni hiyo kali, tarehe 19/07/2015
zilipatikana habari zakuaminika kwamba silaha zilizoporwa
Sitakishari zimefichwa mkoa wa jirani wa Pwani katika sehemu
isiyofahamika vizuri korini.
Katika ufuatiliaji Kundi kubwa linaloundwa na vikosi
mbalimbali vya Polisi lilienda mkoa wa Pwani na kufanya
msako.
Mafanikio yaliyopatikana katika msako huo ni kamaifuatavyo:
Katika kijiji cha Mandimkongo kata ya BUPU, Wilaya ya
Mkuranga, Mkoa wa Pwani katikati ya msitu/vichaka baada ya
taarifa zakuaminika kikosi maalum kilifukuaardhinina katika
shimo hilo zilipatikana bunduki 15 ambapo kati ya hizo
Bunduki SABA (07) niainaya (SMG), bundiki SABA (7) niainaya
SAR, MAGAZINE MOJA YA SMG yenye risasi 28, na zote
zimetambuliwa kwamba ni silaha za kituo cha Polisi
Sitakishari zilizoporwatarehe 12/07/2015.
Katika shimo hilo lililofukuli wapiailipatikana silaha moja
aina ya the NORINKO ambayo inafanyiwa uchunguzi kujua wapi
ilipoibiwa.
Pia katika shimo hilohilo zilipatikana fedha taslim za
tanzania shilling MILLIONI MIA MOJA NA SABINI(TSHS:
170,000,000/=)ambazo zilifungwa katika sanduku maalum.
Muhtasari wamafanikio nikama ifuatavyo:
Kukamatwa kwa watuhumiwa watano ambapo watatu walipoteza
maisha katika mapambano na polisi.
Kupatikana kwa silaha kumina sita ambapo kumi na nne kati ya
hizo ziliporwa katika tukio la Sitakishari na mbili ni za
majambazi.
Zimepatikana jumla ya risasi 53 ambapo risasi 28 niza kituo
cha Sitakishari na risasi 25 ni za majambazi.
Fedha taslimu za kitanzania shillingi million mia moja na
sabini (Tshs 170,000,000/=ambazozinachinguzwa.
WANAOTAFUTWA NA POLISI(WANTED PERSONS)
Oparesheni hii ni endelevu na kwamba bado inaendelea kwa
ukali uleule pamoja namafanikio yaliyotajwa.
Tunahitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi na wadau
mbalimbali ilikutokomeza kundi hili la watu wachache ambalo
limegundulika kuwa na tabia yakuvamia vituo vya Polisi kuua
askari na kupora silaha, kupora katika taasisi za fedha,
kupora kwa kutumia pikipiki(bodaboda), n.k.
Katika harakati hizo wafuatao wanatafutwa na Jeshi la Polisi
haraka iwezekanavyo:
ABDULAZIZI S/O AHMAD
ABDULRASHID @ USTAADH
ABDULAZIZ anaishijijini Dar es Salaam –Kiongozi wa Kundi
SHABAN S/O MOHAMED MTUMBUKA @ AMIR SHABAN NDOBE
HANNAFI S/O JUMANNE KAPELA @ MKAMBA @ SHEIKH HANNAFI
HASSAN S/O HARUNA ISSA @ DR. SHUJAA
ZAHAQ S/O RASHID NGAI @ MTU MZIMA.
ABUBAKAR S/O NGINDO @ ABU MUHAMMAD
KHAMIS S/O RAMADHAN
USTAADH RASHID (Aliua wakati katukio la Sitakishari).
S.H. KOVA - CP.
KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM YA POLISI D'SALAAM




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment