Tuesday, 21 July 2015

Re: [wanabidii] Kiteto tumejipanga na Magufuli wapinzani wataisoma mwaka huu

Wanakiteto kwa kweli mna kazi. Nimekuwa nikija huko mara kwa mara na kuona mnavyotumiwa na wanasiasa kupigana. Mnao uwezo wa kumaliza uhasama ila mmewaachia wanasiasa kuwatumia kwa faida yao na nyie mnajikuta mnashabikia tu bila kujali mustakabali wa vizazi vyenu.
Hakuna tatizo linalotokana na siasa za upinzani huko Kiteto.
Nilidhani makala kama hizi zingezungumzia namna ya kuwaunganisha wakazi wa wilaya hiyo ambayo inafananishwa na maeneo yenye machafuko kama Darfur au Somalia.
Tumia nafasi hii kujenga sio kuzidisha uhasama

Sent from My Ipad

On 21 Jul 2015 15:28, "'mpombe mtalika' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Na Mkulima wa Kiteto

Wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto mkoani manyara tumejipanga vilivyo wapinzani wajiandae kisaikolojia kuisoma namba, kuanzia hapa Kibaya, Matui, Ngusero, Dosidosi, Kongoli, Mbigili,Lang'otoni, Lairelo, Njoloo,  Mbeli pamoja na Mrijo juu na chini na sehemu zingine.

Mwanzo tulikuwa na Mashaka na mchakato wa weagombea urais wa ccm kutoka na mgombea mmoja kuwapa kiburi watu wa jamii Fulani hapa kiteto na kusababisha mapigano ya mara kwa mara kati ya wafugaji na wakulima.

Lakini wana kiteto kwa ujumla tuna imani kubwa na dr. Magufuli  kutokana na utendaji wake serikali hususani kwa kusimamia ujenzi wa madaraja yakiwemo ya hapa kiteto kama madaraja chemchem, Ngarenalo na mengineyo

Pia tunaamini Dr.magufuli atamaliza uhasama uliopo baina ya wafugaji na wakulima inayotokea hapa ambapo mwaka wa jana watu kadha walipoteza maisha kutoka pande zote mbili za wafugaji na wakulima haswa katika maeneo ya Matui, Chekanao, Lang'tomoni pamoja na Irela.

Tunapenda kumpongeza Dr. Magufuli na Rais Jakaya Kikwete sasa Kiteto tumeanza kuiona lami katika maeneo ya kibaya na  na ujenzi wa barabara zingine za kiwango cha lami unaendelea, hilo tukio la kwanza kwa wakazi wa halmashauli ya wilaya ya Kiteto kuwa na lami tangu uhuru hatukuwahi kuwa na lami tulikuwa tukiiona kwenye tv na kuisikia kwa wenzetu.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment