Ndugu,
Mimi ninayo machache ya kibidii, kimabadiliko na hasa katika Jimbo la Kigamboni.
Kusema ukweli sijaona mikakati ya dhati kwa Chama chetu kuwa Serious na hili jimbo, sawa yawezekana muda bado wa kuanza kutangaza nia ila naamini ni vema atleat kuwe na mtu ambaye atakuwa anasemwa semwa kuhusu kugombea Jimbo hili lililojaa taabu na manung'uniko chungu nzima toka kwa wakazi wake. Tuchukue mfano wa SIMANJIRO hivi sasa wakazi wake wanasubiri ti 2015 wamsimike JAMES OLE MILLYA kwa ajili ya kutetea haki zao. Hili liko pia katika majimbo ya Muleba Kusini, Karagwe, Songea Mjini na kwingineko kwingi.
Natoa wito kwa Wanachama wa CHADEMA kigamboni kuanza kujipigia ndogondogo ili tukae mioyoni mwa watu kusubiri tu idhini kama ilivyokuwa kwa JOHN MNYIKA 2010. Then nina ushauri uongozi Jimbo la Kigamboni kuwa MSTARI wa mbele kutoa matamko hasa yanayohusu Chama Tawala kwenda kinyume. Mfano Wananchi kule Kimbiji wanataka kunyang'anywa ardhi yao sijasikia Chama kikitoa tamko.
Mtetezi wetu amekuwa NYARONYO KICHEERE. Na kwa kweli nichukue fursa hii kumshukuru na kumpongeza huyu Bwana maana anavyotutetea,it is Convisingn na intia moyo. Nimeona pia makala yake kwenye Tanzania Daima leo alivyomchambua Bibi yangu Prof Anna Tibaijuka. Please endelea hivyo. Na kama ni kaazi wa Kigamboni please anza kujenga Mazingira.
Vijana tuanze kujitangaza kwa ajili ya Kigamboni
DB
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment