Tuesday 31 July 2012

Re: [wanabidii] Fw: Fwd: Fw: That was 55 years ago !! It is happening now !!

 
Ukimpa mtanzania mkopo alime sio alimiwe na hao G8-atafanya kweli hatokiuka misingi ya mkataba? Huenda hao G8 wameona matatizo Africa pamoja na TZ. Kwani Zimbabwe au Mozambique baada ya kuondoka Wakulima wa kizungu wa mashamba makubwa kuna mashamba makubwa ya wenyeji? Mbona waliokuwa wanalimishwa manamba kwa trekta na majembe ya mkono wamekimbia mashamba na wamekuwa wakikimbilia South Africa ambako wanapata matatizo mengi. Kwao kuna food inseucity na njaa ila ardhi kibao mzungu kaiacha ambayo aliichukua huko nyuma? 
 
Mifano ya mikopo ni mingi Africa hata TZ. Mashamba ya Shayiri, ngano baadhi ya maeneo ya mkoa wa Arusha analima nani baada ya settlers kuondoka huko na kuna boreholes ktk mashamba hayo? Hata kuchangia kwa kuuza mbuzi mmoja kila boma ili zonal borehole drilling office isafishe na ifufue borehole na kuweka bomba kunyweshea mifugo au mashamba tatizo bali kutembea kilometa 20+ kwa siku kutafuta maji au kunywesha mfugo ndio kunakoendelea. Siku hizi kuna makampuni private kibao ya kuchimba visima vifupi na virefu. Lakini tazama mlimbikizo wa mifugo na mama anavyotembea mwendo mrefu na punda kutafuta maji tu na ambapo mbuzi mmoja kila kaya na tajiri ng'ombe mmoja kwa kaya au boma ingetoa fedha za kutosha kwa kijiji au vijiji kuchangia borehole moja wakatandaza mabomba. Nani achangie hivyo? Matatizo tunayo.
 
Huenda G8 wanaogopa aana wanatujua sisi waafrika kuwa mtu atapewa mkopo atafanya anasa, ataoa wake wengi, atatoroka nyumbani, hatofanya kilichotegemewa ni arusi, sherehe za ufahari etc.
 
Hao unaowaona baadhi wajengao DSM mabondeni ktk mafuriko wameuza majumba magomeni, kariakoo etc kwa ma-milioni wamechezea na kuhamia mafurikoni.
 
Ni wachache waliopata hata mafunzo ya vitendo ya shamba darasa wamefanya kuzingatia maelekezo. Kama ni youth-ni mafunzo ya capacity building kila funding na training NGO inapowafikia na ikiondoka NGO ikija nyingine wanaunda kundi jipya, baada ya posho za training kuisha wanarudi tena kijiweni-nani alime hata bustani ambapo youth wengine mfano iringa daima ni matenga ya nyanya, biringanya, bamia wanapeleka mijini kuuza na wengi hawajapata mafunzo hayo!
 
Ikiwezekana, Mikataba ya TIC katika kuwapa ardhi wawekezaji katika agro-industries ili walime mashamba wajaze Silos tupate food security nchini, wafanye processing na wauze nje izingatie mengi ila wawekezaji hao waje watatufaa. Ujio wao utampa mtu guarantee kwamba akilima na kupanda zao fulani aliyempa mkopo ndio mnunuzi na atapeleka kiwandani kwake mazao hayo. Sio hawa wanunusi wabongo wa Private, public Practice wanauoza dawa na mbegu feki na kununua mazao mabichi shamba kwa bei ya dhuruma. Samaki mkubwa kumla mdogo asiyeweza kupambana.
 
Utumwa tunautaka wenyewe, hata ikiwepo PPP kwa nia nzuri tunajionea na kujiibia wenyewe. Licha ya hizo nchi za vita kila mmoja kupigana na kutaka awe Rais yeye. Hapa bongo, utauona mijini na vijijini asubuhi saa moja tunacheza pool nje ya nyumba, mtu anakula breafast na beer asubuhi. Mchana video majumbani watoto wanatoroka shule kuangalia. Kila mtu biashara ni vichubua uso, mitumba, vitumbua, chakula sio Kilimo au uzalishaji ni circulation ya mitumba, used items na vyakula mitaani vya sambaza TB.
 
Mtu akichimba dhahabu au Tanzanite na mawe mengine ya vito kama mchimbaji mdogo  kulewa na anasa. Kati ya watu 100 wachimbaji wadogo wapatao hela ni 6 tu waliowekeza kikamilifu (Utafiti wa Mugusu, Nyangarata, Nyamigele Lake zone). Wengine ni kuongeza mifugo kupata wealth status kwa kuilimbikiza na zio kuzalisha mali na bado ataoza kitoto kidogo cha kike ili auze eti asomeshe kaka zake. Unaambiwa ni mfugaji, sio auze wale aliokuwa nao hapana aoze kachanga. Na jitu zima linaoa kachanga cha miaka 8.
 
Angalia maeneo ya ardhi yaliyopo Mkuranga, Rufiji, Handeni, mabonde ya Mtwara, Lindi, Ruvu halafu uone nani analima-vizee vishamba vidogo. Watoto wao wenye nguvu wapo wanacheza karata 3 eti jembe la mkono. Isipokuwa usiku wapo na mafuso kuiba mahindi ya vizee yanaingizwa mjini tunachomewa. Kama jembe la mkono halifai-anachumaje na kuiba mahindi ya jembe la mkono? Kama jembe la mkono halifai, akija mnyarwanda, mhindi, mpemba, mbona anamkatia mraba analima kutwa kwa jembe hilo kisha analewea zote!!
 
Kinyesi kimezagaa cha traditional livestock na cha mbuzi wa kisasa wa maziwa waliosambazwa vijijini kusiko mifugo ili kuboresha lishe (CONCERN, FAO, TASAF etc); kimezagaa kijijini (kwa wafugaji) lakini mashamba hayawekwi mbolea!! Ila kinyesi kinazalisha mainzi na wadudu wengine na kuleta trachoma. Tatizo la kwanza ukiuliza kijijini hapo-Ardhi imechoka, haizalishi tuna uhaba wa chakula. Tunaomba tuletewe mbolea ya 'Minjingu'. Hapo upo Makuyuni, Naitolia, Mswakini (mifugoni) au Upo Lindi (traditional goats na hybrid Cows and goats kijijini  na kuku kibao). Mifugo ya hybrid- zero grazing na ile ya traditional herding huachwa ikizagaa kiasi kwamba inabidi wanakijiji walime mazao isiyoliwa na mifugo ili waninue nafaka za chakula. Ukitekeleza sheria ya kukamata mfugo na kutoza faini ndio unataka uchomewe nyumba au upigwe mkuki. Kiasi kwamba, hata mashamba ya shule hayalimiki ili wanafunzi wapate uji shuleni. wazazi hawawajibiki na mifugo yao. tatizo kuu la kushindwa lishe shuleni-ardhi chakavu (kinyesi kipo, agric agricultural extension worker ana ofisi mita chache kutoka shamba la shule anabofya simu kutwa)mifugo inayofagaa (wanyama pori wa majumbani!!). Waache G8 agro-based companies waje.
 
Wavivu hata utubebe hatubebeki. daima hutolea mifano baadhi ni-Kawaangalie Wazigua Wasomali Ruvu-Makuruge Village. Wenyeji wakazi wanajipanga daily kwao na wengine kutoka kila asubuhi  kununua bidhaa wanazozalisha kwa jembe la mkono mpaka mikeka na majamvi wasukayo kwa kutumia phoenix plants (mikindu) ya hapo Ruvu. Wao wenyeji wapo hapo kuabudu uvivu na bonde zuri ardhi bwerere.Sasa barabara inajengwa ya lami kila mtu mbioni kuuza na bar zimeanza kujipanga na milingoti ya majengo ya anasa Ruvu hadi Msata.
 
Arable agric land Tanzania inageuzwa plots za majumba na mipango miji hiyo tunaipanga wenyewe kutanua miji endlessly kumeza vijiji-tunajiweka pabaya. Mfano, Mabonde ya mji wa Morogoro ni ya kilimo kwa sababu maji yanatelemkia mjini na mabonde hayo ndio mji na unapanuka kuzamisha mashamba yote. Huko nyuma, ardhi ya Kibaha yote ni ya kilimo sana ni-Mji. Hivyo hivyo itakuwa ya Kilosa, Bunju-Zinga-Kitopeni-Ruvu Basin ya Bagamoyo hadi Lugoba-Msata, Bwewe, Pangani River-basin-Hedaru-Ruvu ya Same-Kilimanjaro you name it-Tuna jimaliza wenyewe, hatujihurumii.
 
Kwa nini tusiwe na miji na mashamba? Mbona Ulaya nchi zilizoendelea kuna miji-cities with farms? Watu wakilima Dar na waliunda Development villages, watu wenye mifugo DSM wakaambiwa wahamie nje ya miji vijiji vya ujamaa-vya maendeleo (Goba, Bunju, Changanyikeni, Tegeta, Kigamboni etc)na magombe yao inayozurura mjini, mbuzi etc. Mara sheria ikatoka hakuna mashamba DSM ni- Mji. Unapochukua ardhi ya vizee Bunju, Zinga etc waliokuwa wakilima kuzunguka nje ya nyumba au umbali fulani, ukapima viwanja vizee vishindwe kulipia, na hawana social security cash money kila mwezi, unawafanya wauze vijukuu vyao viwe changu doa umri mdogo ili waweze kula chakula.na watakufa kwa HIV muda mfupi, unaongeza vijana mashoga!!
 
Hao wajao kulima, kama atachukua ardhi ya kimila, muhusika (mwenyeji-owner)asaidiwe na mwekezaji kuipima kwa vile ana hela. Land owner apate title Deed na apewe mkataba wa kufaidika kwa milioni kadhaa kila mwezi. SIO TIC pekee ifaidike. Kijiji ambapo customary land owner yupo kifaidike pia maana ardhi ipo hapo na kijiji kinaadhirika pia. Hii itawasaidia customary land owners na kijiji husika kiwe na mipango ya benefit sharing (Benefit sharing scheme).Hii itapunguza matajiri na wasomi wajanja kufaidika kutokana na ardhi pekee kama ilivyo mikataba tunayosikia na Tanesco. Mapato na matumizi ya kijiji yawe wazi na mwekezaji atumie sheria ya GVT kujenga facilities za mafao kuzuia viongozi kule chini kujinufaisha binafsi. Itakuwa vema, kuwe na village land use plan na title Deed kwa kila kijiji ambacho kitapata G8 agro-based investments. hii itaondoa magomvi ya ardhi na uvamizi wa wawekezaji ambao mwingine watu wa Siasa huusababisha.
 
Kama kuna mpango wa kaya kufaidika, marufuku kaya kuiuza ardhi kabisa mpaka ipite miaka 10-20 kuwe na mkataba na sheria ili kuepuka watu kuuza ardhi kujifanya wanakwenda kwingine wanayonyingi, halafu kusababisha land conflicts kwingine au kuhamia restricted or disastrous area. Serikali au mwekezaji anapoboresha eneo, marufuku muhusika kuuza eneo. Kama atachukua ardhi ya serikali iliyokuwa ya Mamlaka ya Pamba, kahawa, Sisal, NAFCO, Magereza etc na viwanda vyake-ihakikishwe analima hasa. sio anachukua ardhi na mikopo ya World Bank, African Dev Bank kisha anahamia Kenya, Canada kujenga majumba na kupangisha in $ mashamba hayalimwi. Kiwanda cha pamba alichopewa hafanyi ukarabati kinaguwa ni karakana au store ya used papers na types na spare za magari anaanza biashara kinyume na mkataba. IMF ililazimisha PPP na kuuza mashirika ya GVT kupunguza gharama ya GVT, mbona wawekezaji wenyeji matajiri waliochukua hawakufufua uchumi; wanaonunua mazao under PPP ni vibaka wezi kudhulumu wakulima kuliko GVT parastatals? Na hao wezi under PPP ni waafrika, watanzania walioanzisha makampuni binafsi vibaka wa hali ya juu. Uchumi unadidimia wao wanatajirika.
 
Na ndio maana wawekezaji wa nje wanarudishwa maana sisi uswahili kujila na kujiumiza wenyewe kwa wenyewe. Na sasa ukiwa mkweli msema wazi na mfuatiliaji mpenda haki unawindwa kuuawa.Inakuwa bora mkoloni mambo leo arudi na kuwe na viongozi madikteta ili uchumi ukue. Tunajiuza na kuuza ardhi kama kanzu anyway na tunajimaliza wenyewe.Eti kwa vile TZ ardhi nyingi, kubwa, bwerere, una uhuru wa kuhamia popote na ukatesa watu kwa kuvamia vyanzo vya maji, misitu ya hifadhi kufyeka, kuingiza wageni na mifugo wakalishia, kuwasha moto, kulishia mashamba ya wenzio mifugo utakavyo ( Kiambata-ambapo wewe ukilima hulishii mifugo yako mahindi hayawi majani ya mifugo), kuvamia maeneo ya mifugo ukalima mpaka wildlife migratory routes, kukaribisha majambazi wakavamia watu vijijini wakisha uza mazao gulioni. Ukimaliza kuiba mamilioni hayo ni kuyaangamiza pombeni. 
 
Itafika wakati tutarudia kwa Mh Baba wa Taifa wa Mwl Nyerere tulikotoka wakati wa ujamaa wa kukagua kila nyumba nani anafanya nini, ukubwa wa mashamba ya chakula na ya mazao ya biashara yaliyolimwa kwa msimu na kuandikisha wageni kwa balozi kila wanapokuja ktk kaya. Inatia uchungu na kichefuchefu. Bado ifike tuwawajibishe extension workers na wabunge, madiwani waonyeshe action plan zao na watathiminiwe wamehamasisha maendeleo gani katika majimbo yao. Ama sivyo ni maneno na kushutumiana tu"wewe umefanya nini pale ulipo katika jimbo au eneo lako la kazi kama mshauri na mtaalamu kijijini-mtaani? Unacho cha kuonyesha?
Yataka Rais dikteta na mwenye mikono na macho ya Pweza. 
 
From: Kult <kultathman@yahoo.com>To: wanabidii@googlegroups.com Sent: Monday, 30 July 2012, 13:46Subject: Re: [wanabidii] Fw: Fwd: Fw: That was 55 years ago !! It is happening now !!
DONT WANT U TO FOFOWARD THIS MAIL TIO MYID
 
Kult's World
From: severina martin <sisoba2003@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, May 24, 2012 11:07 AM
Subject: Re: [wanabidii] Fw: Fwd: Fw: That was 55 years ago !! It is happening now !!
UKOLONI UNAPIGA HODI HUOOOOO!

From: Solomon Msomba <msomba2000@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, 24 May 2012, 10:17
Subject: Re: [wanabidii] Fw: Fwd: Fw: That was 55 years ago !! It is happening now !!
Wanabidii,
Leo asubuhi nimekuwa nikiangalia Jambo Tanzania TBC. Nimesikia G8 wanataka kuwafadhiri large Agro-based Companies kuja Africa kuanzisha mashamba makubwa na kupewa mikopo itakayowezesha haya Makampuni kuwa na nyenzo zote za kilimo cha kisasa. Baada ya hapo watu watakaokuwa wanayazunguka makampuni hayo watakuwa na mashamba yao watakayolimiwa na kuhudumiwa kwa gharama ndogo. Mimi najiuliza hao G8 kwa nini wasimkopeshe mkulima wa kati kwa riba nafuu ambaye ni mwafrika/mtanzania baadala yake akopeshwe mwamerika au mfaransa? Baada ya kutafakari nimeona haya kweli ndiyo Mwalimu aliyasema 1958. Na kwa serikali yetu ya sasa upo uwezekano mkubwa kupokea hili wazo la mtu kama OBAMA kama furushi bila kutaka kujua kilichomo ndani. Hapa hamna tofauti watazania kupewa bomu kwenye mfuko halafu tusijadili kilichomo ndani. Jamani tujadili hii serikali ya sasa haina cha kupoteza endapo tutakubaliana na G8. Cameron na OBAMA wamesema ushoga ruksa, sisi tunakataa. Lakini hii ya kukubali wazo la kilimo ni sawa kukubali Ushoga. Tena la kilimo ni baya zaidi kwa sababu litaishia kwenye kifo cha watanzania kama Mwalimu alivyosema 1958. Naomba watanzania badhi ya viongozi wamekaa kwa muda mrefu kwenye madaraka wamechoka kufikiri. Hawa ni binadamu wamechoka!!!. Tunahitaji viongozi wengine wanaoweza kufikiri kwa undani kwa ajili ya watanzania. Tafakari. --- On Tue, 5/22/12, Balama Chelestino <balamapc@yahoo.co.uk> wrote:

 
--
---- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    

0 comments:

Post a Comment