Tuesday 31 July 2012

[wanabidii] TAMKO LA SERIKALI KUHUSU KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MWANAHALISI

SERIKALI ya Jamhuri ya Tanzania, imelifungia gazeti la Mwanahalisi kwa
muda usiojulikana kwakile kilichoelezwa kuwa na mwenendo wa kuandika
habari na makala za uchozezi.

Sababu nyingine ya kufungiwa kwa gazeti hilo ni pamoja na kujenga
uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani
na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa
nchi.

Akisoma tamko la Serikali leo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi
Wizara ya Habari (MAELEZO), Phabian Lugaikamu, alisema kuwa katika
toleo la gazeti hilo namba 302, 303 na 304 ya mwaka 2012 na mengine
yaliyotangulia yalichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga
hofu kwa jamii.

"Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi ameitwa na kuonywa mara nyingi
lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa
jamii,pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa
habari"alisema
Aidha alisema kuwa mhariri huyo mara zote katika utetezi wake amekuwa
akinukuu kifungu cha 18 cha katiba ya nchi kinachotoa uhuru wa kutoa
maoni na kwa makusudi kutokunukuu kifungu ca 30 cha katiba hiyo
kinachoweka ukomo wa uhuru.

"Serikali imeamua kulifungia gazeti hilo kutochapishwa kwa muda
usiojulika kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976, kifungu
namba 25(i),adhabu hiyo itaanza tarehe 30 julai,2012 kwa mujibu wa
tangazo la serikali namba 258 lililochapishwa katika gazeti la
Serikali na kutolewa jijini Dra es salaam julai 27,2012"alisema

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment