Tuesday 31 July 2012

[wanabidii] RE: SEREKALI LEGELEGE

Ndugu Watanzania sasa ndio naamini kuwa Serekali ya CCM inayoongozwa na CCM ni legelege na inabidi ijiuzulu au Watanzania tuitoe madarakani Mwaka 2015.

 

Wakati tumerudishiwa fedha za RADA na kuwepo kwa taarifa rasmi kuwa kuna viongozi wa Tanzania na Wafanya biashara wameficha kwenye Benki za Uswiss dola bilioni 300 kwa nini Kiongozi kama Rais asiamuru fedha hizo ziletwe zikaboresha mishahara ya Madaktari na Walimu.

 

Mimi napata mashaka kuwa huenda viongozi wanaotajwa ni hao hao wenye madaraka makubwa Serekalini. Sekta ya Elimu na Afya sio za kufanyia mzaha. Kwa wenzetu kuliko wajenge mabarabara ya Lami nchi nzima ni bora watu wawe na afya na elimu nzuri. Hapa kwetu tunakimbilia kujenga mabarabara ili wawekezaji wanaolifilisi Taifa na Wakubwa wenye biashara za Malori wapate njia za kutumia.

 

Aubu kubwa sana. Serekali iache kutishia Wafanyakazi. Iwalipe kama inavyolipa Wabunge. Wafanyakazi wana hasira. Watu wanaacha ualimu wanakimbilia ubunge. Kisa wabunge wanalipwa zaidi. Watanzania inabidi kwa pamoja tuchukue hatua za haraka sana. Lazima tupewe matumizi ya fedha za rada, epa, kwa maandishi na dola bilioni 300 zirudishwe.

Mkereketwa

Lengai Ole Letipipi

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment