Sunday, 29 July 2012

Re: [wanabidii] Neno La Leo: Na Wabunge Wetu Wengine Ni Wezi, Hakyamungu!

Hivi kwa mwendo huu tutafika katika nchi ya neema tuliyohadiwa? AU tutazunguka na kusubiri miaka 40 kama wana wa Israeli ili kufika nchi ya asali na maziwa? Ewe M'nyezi Mungu mwingi wa rehema na huruma utulinde, utuongoze na ulilinde Taifa letu la Tanzania. Utuepushe majaribu na matamanio ya wizi na ufisadi ili tuweze kufika nchi tuliyoambiwa na Mtume Mussa.

Mungu Ibariki Tananzania

Amen
Sent from my BlackBerry® smartphone from Orange Botswana

-----Original Message-----
From: <mouddymtoi@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 29 Jul 2012 14:01:29
To: <makene_84@yahoo.com>; <wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Neno La Leo: Na Wabunge Wetu Wengine Ni Wezi, Hakyamungu!

Makene.
Umenena kweli na umegusa kwa ufasaha madudu yanayo fanywa na wabunge waheshimiwa wanao tegemewa kusimama na kuwasemea wananchi shida zao.

Ukweli ulio uchi ni kwamba ccm na viongozi wake wamechangia kwa kiasi kikubwa kuleta makwazo kwa watanzania na hakika watu hao hawawezi kuwa sehemu ya utatuzi wa matatizo waliyo sababisha maana uwezo wao kutatua matatizo umefika kikoma. Hivyo tunahitaji watu wenye muona mpya utakao tukwamua kwenye tope tulimo nasa.

Naamini tanesco ni sehemu ndogo tu ya uozo uliojichimbia kwenye matumbo ya viongozi wa ccm, siku akibahatika kutokea mtu mwenye uso wa mbuzi na kufukua uozo uliofichwa mali asili na utalii, kwenye ,madini, ubinafsishaji wa mashirika ya viwanda nk. Itakuwa balaa kubwa na laana kubwa kwa watu wa dongo la taifa hili.

Wakati wa kufanya uamuzi mgumu ni sasa, tuwajue kwa majina wabunge walio honga/waliohongwa ili tujue jinsi ya kuwachinjia baharini wakati muafaka ukifika.



----------
Sent via Nokia Email

------Original message------
From: makene tumaini <makene_84@yahoo.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, July 29, 2012 6:24:23 AM GMT-0700
Subject: Re: [wanabidii] Neno La Leo: Na Wabunge Wetu Wengine Ni Wezi, Hakyamungu!

Maggid

Kwanza ni vyema, ukaweka vyema majina ya huyu Profesa Waziri wa Nishati na Madini. Naona umeyaandika kwa kadri unavyotaka, si kwa kadri inavyotakiwa.

Ok back to the topic. Yaliyojiri Dodoma kwa siku kadhaa juu ya mazingara ya tuhuma za ufisadi na rushwa katika suala la nishati, ni dalili nyingine tu ya matatizo kubwa ambalo watawala hawa hawa waliotufikisha hapa tulipo wamekuwa wakiyalea, wakiyapalilia na kuyakuza kwa sababu wananufaika nayo, ama katika ustawi wao wa kiuchumi na kisiasa-kijamii au vyote.

Ni dalili ya matatizo makubwa ambayo yamesababishwa na watawala hawa hawa, ambao kwa bahati nzuri sana, wamefanikiwa kutuaminisha kuwa akili (kiwango fulani cha kufikiri) zilizosababisha zina uwezo wa kulitatua tatizo hilo hilo, kisha tukasonga mbele. Mzaha mkubwa.

Maggid

Mtu akikusoma kwa makini katika hii article yako nzuri, atagundua suala moja kubwa, ambalo kwa bahati mbaya nao unaanza kuwa ugonjwa wetu mkubwa lakini mbaya kabisa. Kujadili matokeo ya tatizo badala ya kushughulikia chanzo/kiini cha tatizo/matatizo. Haya yaliyojiri siku ya Ijumaa na Jumamosi, lakini yakiwa yameanza siku chache kidogo nyuma katika corridors za bungeni na mahotelini, ni matokeo tu ya matatizo/ tatizo kubwa ambalo limelelewa na watawala hawa hawa kwa manufaa yao. Nasi tunashangilia comedy za bungeni.

Maggid, Watanzania wengi leo wamevutiwa kwenye hili shimo kubwa la kujadili matokeo badala ya kiini/chanzo cha matatizo. Na hii ndiyo exit nzuri ya watawala wetu wa leo. Wanafurahia kweli wanapoona taifa kila mara haliwezi kumaliza mjadala mmoja, kwa sababu tumekuwa hodari kweli kweli wa kujadili OFFSHOOTS. This is another offshoot from the same people!!!!

Offshoot hii inazidi ku-cement nadharia ya kwamba hapa tulipofikia, kwa sababu si rahisi akili ile ile iliyosababisha tatizo ikaweza kulitatua, tukasonga mbele, Watanzania wanahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutawala. Period. Mengine itakuwa kudanganyana. Kama kweli tunataka kuitibu kansa hii ambayo Mwalimu aliitabiri siku nyingi, hatuna budi kukata kiungo, kabla haijasambaa.

Lakini pia kwa kujadili matokeo haya na kuacha kiini cha matatizo, watawala wamefanikiwa kabisa kutuingiza kwenye hatua moja muhimu ya uwendawazimu unaoanza hatua za awali. Kurudia mara kwa mara, kufanya jambo lile lile, kwa namna ile ile, kisha utarajie mabadiliko. Ni lazima tuondoke hapo, kama kweli tumedhamiria.

Wanaojua kilichokuwa kikijiri katika mahoteli na logdes au wanakokutanika wanaoitwa waheshimiwa (kwa kweli bado napenda neno ndugu), kisha kikaendelea kujiri katika vikao vya kamati ya bunge, kisha kwenye kamati ya namna hiyo hiyo lakini ya CCM, kisha kwenye circles zingine serikalini, walibaki midomo wazi, wakipigwa na butwaa kusikia michango ya  baadhi ya wabunge, hasa waliopata nafasi ya kuchangia kwa kuzungumza siku ya Ijumaa na jana Jumamosi. Unafiki mkubwa. Wanachangia kwa MIKIKI na MAKEKE, hata kumsifia mtu ambaye usiku mzima walikuwa wakisema lazima aondoke!!!!!

Maggid, dalili hii nyingine tena, inaendelea kusisitiza kuwa rushwa na ufisadi, ambao Mwalimu aliwahi kusema ni hatari kuliko kitu chochote na tishio la amani kwa nchi kwa wakati usiokuwa wa vita, hauna dini, hivyo si suala la wachungaji wala mashehe, wala viongozi wa dini za kipagani. Shehe/Mchungaji/mpagani aliyejiunga na hawa watawala, hawezi kuwa upande wa usafi hata kama hajatajwa au kuwekwa hadharani.

Maggid

Nawe unataka kukubali kuvutwa au kusukumiwa kwenye shimo la uzembe wa kuendelea kujadili matokeo ya matatizo kila mara ila mara?

Leo hii taifa hili linaanza tena kujadili TANESCO wakati inajulikana wazi kuwa nishati, madini, biashara, viwanda, utalii na maliasili ndiko ambako wamesimika miguu yao ya UFISADI unaozidi kuliteketeza taifa!

Taifa hili tena linalazimika kujadili matokeo ya tatizo kubwa, wakati inajulikana wazi kuwa serikali iligoma kutekeleza maagizo 23 juu ya ufisadi wa Richmond, ya bunge hili hili ambalo eti sasa linaonekana ni bingwa.

Lakini ni bunge hili hili tena, likaamua masuala yanayohusu ufisadi huo wa Richmond yatashughulikiwa na Kamati ya Bunge ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje, ambayo Mwenyekiti wake wa Edward Lowassa!

Ni bunge hili hili limejadili juzi suala la Mkurugenzi wa TANESCO, bila hata kugusia, hata kidogo suala la maamuzi ya bunge juu ya sakata la David Jairo ambalo mpaka sasa serikali haijaleta bungeni utekelezaji wa maagizo hayo kama ilivyoagizwa na bunge hili hili ambalo leo inaonekana limesahau kila kitu kuhusu sakata la Jairo.

Kuna ufisadi wa wazi ulikuwa unavuka kiwango cha sakata la Jairo, mathalani kama tukiamua kufanya mlinganisho hapa katika baadhi tu ya matokeo na dalili ya tatizo kubwa katika nishati.

Ni bunge hili hili, ambalo karibuni kamati yake ya kudumu ya fedha na uchumi imemchagua mwenyekiti wake kuwa ni Chenge, ambaye pia ataisimamia serikali katika mgawanyo na matumizi ya mapato na matumizi, ikiwemo fedha za rushwa ya Rada!!!!! Come on, halafu u still expect different results from watawala hawa na washirika wao...A big joke!

Eti tunashangilia kuvunjwa kamati, kisa rushwa na conflict of interest. Muda gani sasa Kamati ya LAAC ambayo iligawiwa kihila kwa Mrema, imetuhumiwa kwa rushwa???? Kwangu kinachozidi kunishangaza kila siku ni mbunge KUHONGWA, yaani Mbunge anahongwa!!!

Ok! Juzi wamekubaliana, tena wakashangilia sana wakati Mbunge Selasini alipokuwa kiweka mambo hadharani kwa kiwango fulani hivi, lakini ni hawa hawa walipoambiwa kuwa WALIHONGWA kwa kiwango kikubwa tu wakati wa uchaguzi wa Ubunge wa Afrika Mashariki, waling'aka wakisema hakuna ushahidi!!!

Conflict of interest??? Nani aliwateua hao wabunge kuwa kwenye kamati hizi walizomo sasa ambako wengine wana-conflict of interest za wazi kabisa.

Nimalizie, kwa baadhi yetu tuliokuwepo hapa Dodoma, tuliobahatika kutumia taaluma hizi kujua walau kilichokuwa kikijiri, tunatarajia kuwa wanahabari wetu wataandika kwa ufasaha mkubwa na kuanika uchafu wote, wakijaribu kuchokonoa chanzo cha tatizo hili, ili jamii ijielekeze kutibu kansa hii kwa ujumla wake.

Makene


--- On Sun, 7/29/12, maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:

From: maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Neno La Leo: Na Wabunge Wetu Wengine Ni Wezi, Hakyamungu!
To: "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, July 29, 2012, 11:14 AM

Ndugu zangu,

Waziri
Muhongo ameusema ukweli wake kule Dodoma. Nami nimefuatilia sinema hii
ya Dodoma, kila inavyoendelea ndivyo ninavyozidi kuchoka. Ama hakika,
tunakokwenda siko, tuna lazima ya kujipanga upya.

Namsifu
Waziri Muhongo kwa ujasiri wake. Amutusaidia sana kuyajua yale ambayo
yangetuchukua muda mrefu kuyajua. Kwa kusimama kwenye ukweli Waziri
Muhungo ameitendea haki nchi yetu tuliyozaliwa. 

Na
tulipofikia hapa ni ukweli tu ndio utakaotusaidia kutupa ahueni ya hali
mbaya tuliyonayo kama taifa. Huu si wakati wa kutanguliza siasa za
vyama bali kuitanguliza Nchi yetu tuliyozaliwa na tunayoipenda.
Kutanguliza uzalendo.

Leo
tunabaki vinywa wazi kusikia kuwa hata wachungaji, na wengine
wamejiingiza Bungeni, kuwa nao wanawaibia Watanzania wenzao. Kwamba nao
hawatosheki. Wanaiba huku wakitaja neno la Mungu. Leo hata wale
wanaojinadi kuwa ni watetezi wa wanyonge wameanza kutiliwa mashaka.
Uwezo wao wa kiuchumi unahusianishwa na ' madudu' kama haya ya Tanesco.
Na kuna hata wenye ' kuwafuturisha' wenzao wenye uwezo kwa fedha
walizowaibia  wananchi wanyonge. Hawa hawana cha swaumu bali wanashinda
na njaa kwa dhambi ya wizi wao.

Tuna
lazima sasa ya kuamka na kuwabana wezi wetu. Mwizi ni mwizi tu, hata
kama ni mheshimiwa Mbunge.Na ukweli ndio unaohitajika sasa. Na si nusu
ukweli, bali ukweli mzima hata kama  utatugharimu maisha yetu. 

Nimepata kusimulia   kisa cha kijana aliyehangaika sana kuusaka ukweli. Katika pitapita zake akaliona duka. Kibao kimeandikwa dukani ; " Hapa tunauza ukweli".


Dukani hapo ukweli unauzwa kwa kilo. Bei ya robo kilo ya ukweli imeandikwa, vivyo hivyo, bei ya nusu kilo ya ukweli. Lakini, mwenye duka hakuandika bei ya ukweli mzima,  kwa maana ya kilo nzima ya ukweli.


Kijana yule akauliza; " Mie nataka ukweli kilo nzima, mbona hujaandika bei?"
" Alaa,  unataka kilo nzima ya ukweli?" Aliuliza mwenye duka.
" Naam" Akajibu kijana yule." Basi, zunguka uje ndani nikuambie bei yake".


Alipoingia ndani dukani, kijana yule akaambiwa;" Kijana, hatukuandika bei, maana, gharama ya ukweli mzima ni uhai wako. Je, uko tayari?"


Kijana yule akatimua mbio. Nyuma aliacha vumbi. Hakuwa tayari kulipa gharama ya ukweli mzima.


Katika Uislamu inasemwa;  sema ukweli, hata kama unauma na kwamba unaweza kupelekea umauti wako.


Hakika, maandiko ya kwenye vitabu vya dini zetu hizi yana ya kutufundisha. 


Na hilo ni Neno langu la Leo.


Maggid Mjengwa,
Sweden.
http://mjengwablog.com





--

Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com

Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com

Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 

 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment