Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),
inapenda kutoa ufafanuzi juu ya mafao ya kujitoa. Ufanunuzi huu
unakwenda sambamba na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na
vyombo vya habari na kuleta mkanganyiko miongoni mwa Wanachama na
Wadau wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
Kufuatia hali hiyo, Mamlaka inatoa ufafanuzi ufuatao:
- Marekebisho kuhusu kusitisha fao la kujitoa yamefanyika ili kutimiza
lengo na madhumuni ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa
mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu hali
ya maisha uzeeni.
- Ni kweli kuwa Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria
ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho. Mchakato wa marekebisho hayo
ulihusisha wadau kwa kuzingatia utatu yaani wawakilishi kutoka Vyama
vya Wafanyakazi, Chama cha waajiri pamoja na Serikali.
- Kwa kutambua tofauti ya ajira, tofauti ya mazingira ya kazi, tofauti
ya sababu za ukomo wa ajira, na umuhimu wa Mwanachama kunufaika na
michango yake wakati angali katika ajira, Mamlaka inaendelea na
mchakato wa kuandaa miongozo na kanuni za mafao ambazo lengo lake ni
kuboresha maslahi ya Wanachama. Miongozo na kanuni hizo zitajadiliwa
na Wadau wakiwemo Wafanyakazi, Waajiri na Serikali kabla ya kuanza
kutumika.
- Kufuatia kuanza kutumika kwa Sheria hiyo maombi mapya ya kujitoa
yamesitishwa kwa kipindi cha miezi sita hadi pale miongozo
itakapotolewa ili kuiwezesha Mamlaka na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
kutoa elimu kwa Wadau.
- Tangazo hili halitowahusu Wanachama waliojitoa kabla ya tarehe
20/07/2012.
- Mamlaka inakanusha vikali kwamba, sitisho la fao la kujitoa si kwa
sababu za Kiserikali au kwa sababu mifuko imefilisika. Tunapenda
kuwahakikishia kwamba Mifuko yote ipo thabiti na michango yote ya
Wanachama ipo salama.
- Hivyo, Mamlaka inawaomba Wanachama na Wadau wote wa Sekta ya Hifadhi
ya Jamii kuwa na utulivu wakati mchakato huu ukiendelea kwa lengo la
kulinda na kutetea maslahi ya Mwanachama.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji
SSRA-Makao Makuu
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+
unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment