Wednesday, 25 July 2012

RE: [wanabidii] Re: NA HAYA YA JKT TUTAYARUDISHA PIA?

Masuala ya ukatili wa kijinsia yalikuwa miongoni mwa sababu za kufuta JKT, je, safari hii itakuwaje?

 

From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On Behalf Of zittokabwe@gmail.com
Sent: Sunday, July 22, 2012 11:31 AM
To: Chambi Chachage
Cc: Wanazuoni - Informal Network of Tanzanian Intellectuals; wanabidii; mabadilikotanzania@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Re: NA HAYA YA JKT TUTAYARUDISHA PIA?

 

Haya katika JKT hayatarudi kamwe. Kumbuka hivi sasa masuala ya haki za binaadamu yameshika mizizi. Jeshi lazima libadilike, taasisi za haki za binaadamu pia zitakuwa makini kufuatilia.

 

Zitto 

Sent from my iPhone


On Jul 22, 2012, at 10:18 AM, Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com> wrote:

 

----- Forwarded Message -----
From: Blogger <no-reply@blogger.com>
To: chambi78@yahoo.com
Sent: Sunday, July 22, 2012 2:50 AM
Subject: [UDADISI: Rethinking in Action] NA HAYA YA JKT TUTAYARUDISHA PIA?

 

"Afande Chacha alimsogelea [Sifuni], na sasa alikuwa akisema kwa sauti ya chini, "Sasa hizi taabu ulizozipata siku zote hizi za nini. Mimi nilikwambia siku nyingi kwamba ningeongea na Afande Kongoro awe anakupa kazi rahisi, lakini wewe umeendelea kuringa. Unaona sasa?" Baada ya kutopata jibu, aliendelea, "Nafasi yako ya mwisho, sivyo nitahakikisha kwamba unapohama wiki ijayo utapelekwa Kambi la Nachingwea kwenye nyoka wengi ukafe huko! Unasikia?" Sasa alikuwa amemsogelea, akijaribu kumshika, lakini kabla hajafanya hivyo, yule msichana alipiga ukelele mkali uliopasua anga na kusikika mbali...Pale ndani kulikuwa na mayai yamevunjika, matrei yametawanyika kama vile yametupwa. Afande Chacha alikuwa amesimama, kamnyooshea kidole cha kumkemea Sifuni, huku akiwa amejawa na hasira. "Unaona hasara unayolitia taifa hili? Unaona?" alipayuka kwa nguvu. Kisha aliwageukia maafande wenzake waliokuwa wamefika na kusema kwa sauti ya hasira, "Nimemkuta huyu msichana hapa akimeza mayai kama kenge! Nilipoingia alitaka kukimbia, badala yake akaangusha matrei ya mayai!" "Mwongo! Mwongo huyu!" yule msichana alipiga kelele huku akilia kwa nguvu. "Alitaka kuni..." (Chachage Seithy L. Chachage, Makuwadi wa Soko Huria, ukurasa wa 74 - 75)

 

"Nilikuwa mhudumu Officer’s Mess, mpishi na msafishaji. Huyo jamaa alikuwa ni mgeni kutoka Makao Makuu ya JKT Dar es Salaam. Kwa kweli sikutaka kufanya kazi pale Mess lakini tulichaguliwa special na Matron, mimi kwa vile niijua kupika vyakula mbalimbali hasa za kizungu. Lakini uzuri wa hiyo kazi ni kuwa uanambulia mabaki ya vyakula (leftovers), na mara nyingine kulikuwa hakuna. Basi huyo Afande alikaa kambini wiki kadhaa. Katika kumhudumia tukawa tunaongea na mimi nikawa namheshimu kama kaka vile. Wala sikusikia mapenzi yoyote kwake. Basi jioni fulani, kanialika chumbani kwake kunywa soda na biskuti na kwa Maongezi zaidi. Sasa kama ulienda jeshi unajua njaa kali unayokuwa nayo. Nikaenda, kanikaribisha vizuri, nilipewa soda na tukawa tunaongea. Basi nikaona mwenzangu anabadilika ghafla! Mara ananikumbatia kwa nguvu, na kunibusu na mengine. Nikajaribu kuaga lakini jamaa hakuniachia. Baada ya ku-plead naye aniachie, kaniachia. Kaomba msamaha na kaniomba niendelee kukaa nimalize hizo soda alizoninulia. Kama mjinga nikamwamini, nikakaa nakunywa hizo soda. Tukaendelea na Maongezi, kukaa kidogo huyo kanirukia, najaribu kusimama huyo, kanivuta na kuniangusha kitandani! Mimi saa hizo nikawa naogopa kabisa nia yake!Kaniambia eti, “ukipiga makelele najua nitasema nini! Nyamaza! Huna sababu ya kunikatalia!” LOH! Kanizaba kibao! Nikamwuliza kwa nini anaifanyia hivyo, na mimi nilikuwa namwona kama kaka yangu!Hapo sasa ikaniingia. Nabakwa! Loh!" Nilimpiga mangumi na mateke lakini..." (Chemi Che-Mponda,  http://swahilitime.blogspot.com/2011/08/marudio-miaka-baada-ya-tukio-kaniomba.html )



--
Posted By Blogger to UDADISI: Rethinking in Action at 7/22/2012 09:50:00 AM

 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment