Thursday, 26 July 2012

Re: [wanabidii] Taarifa za Kutekwa kwa Ndugu Heche Manchare Mwanasheria wa NEMC

 
Uswahili umetuzidi. Hebu mwambie jirani yako mtaani unakoishi kuwa -maji yake yatokayo nyumbani kwake chooni anayatiririshia katika mtaro wa wazi nje ni kero yananuka, yanazagaa, watoto wanayakanyaka, harufu, nzi na mbu na yanaingia uwani kwako uone itakuwaje? uadui mkubwa na anaona kitendo sio kizuri. Kama wapangaji walichanga hela ili aite Vacuum tanker lorry ije kunyonya alizitumia hela na wakimuuliza mkali na kumtishia mpangaji kuwa atamfukuza. Ni hivyo vijijini, serikali za mitaa, mwenye kiti ni Mungu mtu muamua yote pekee. maofisini ni hivyo vinaonekana ila mnanyamaza yanabaki maneno ya corridor tu kila mtu analinda maslahi yake. Kumkomoa mtu kwa kumtendea uonvu ndio dhana iliyopo bongoland. Ukimtaja muovu au jambazi polisi kwa siri utakuta jambazi anajua ni wewe uiliomtaja na kweli ni jambazi lakini atakuua kama kulipiza kisasi kwa kumtaja. Na hivyo ndani ya kaya, familia, koo-mbakaji analindwa. wewe ndugu wa kimbelembele kutaka haki itendeke utachukiwa na kufanyiziwa kukomeshwa. Uovu hulindwa kutenda haki -kulilipizwa kisasi cha aina nyingi sio tu kutekwa, hata kusingiziwa uchawi wakaja kukuchoma moto ndani ya nyumba yako kuwa-mchawi.Ndani ya Afrika zipo nchi zinaishi katika misingi cjanya (ya Kizungu ya kutokuficha ni uwazi na haki) na wapo waishio katika misingi ya uonevu ya mila (mfugaji kaoza kitoto cha miaka 8 eti alipie ada ya watoto-males sio auze mifugo asomeshe watoto) uonevu unaonekana lakini hakuna anayethubutu kuukemea. Unaendelea tu miaka hadi miaka. wapo waishio katika misingi ya undumakuwili ya Uswahili. Anafanya maovu, asisemwe, asiadhibiwe, akiadhibiwa au kutajwa analipiza kisasi. au, ana maovu mengi yanayojulikana lakini bado anataka au anagombea uongozi kwa mbinu na watamchagua au kumpigia kura pamoja na maovu yote au akirudi jimboni atapokewa kwa shangwe, pembeni watamsema na kutoa taarifa zake za siri. Ni ajabu.

From: "gm26may@gmail.com" <gm26may@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, 17 July 2012, 10:28
Subject: Re: [wanabidii] Taarifa za Kutekwa kwa Ndugu Heche Manchare Mwanasheria wa NEMC


Hii Teka teka hii is another threat to our nation

Mbona Kenya Juzi wamebomoa majumba makubwa zaidi and it was a big operation zaid ya mara 5 ya ile ya kwetu lakin hatujasikia mtu atekwe?


Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

-----Original Message-----
From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 17 Jul 2012 00:26:27
To: Wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Taarifa za Kutekwa kwa Ndugu Heche Manchare Mwanasheria
wa NEMC

Ndugu zangu

Naomba kupata updates zozote kuhusu kutekwa kwa mwanasheria wa tume ya
mazingira Tanzania NEMC anayeitwa Heche Manchare .

Inasemekana utekaji huu unahusiana na vunja vunja za nyumba maeneo ya
Mbezi Beach.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.




0 comments:

Post a Comment