Friday, 27 July 2012

Re: [wanabidii] IDARA YA USALAMA WA TAIFA YAKANUSHA KUMTESA DR ULIMBOKA STEVEN

Ni muhimu wote tukakubali kuwa usalama wa Taifa letu uko mikononi mwa vyombo vya dola kimojawapo ikiwa ni idara hii ya Usalama wa Taifa. Hivyo ni busara hata tunapoisaidia kuikosoa tukaonyesha kuiheshimu. Pia ni muhimu nayo ikaonyesha hivyo.
Tuhuma zinazoikabili ni vizuri zikakoma kwa idara yenyewe kujionyesha kuwa safi.
Tukianzia kwa Dr. Mwakyembe, viongozi kadhaa wa siasa, na sasa Ulimboka ukweli tunajisikia kutokuwa salama kama allegations hizi zikiwa za kweli.
Lakini pia majibu yanayotolewa yanaweza kuonyesha anayejibu ni mtu wa namna gani. Mimi ikitoka taarifa nyingine kuwa majibu hayo hayakutolewa na idara nitakubali maana mwanaHALISI wametoa vielelezo ambavyo mtu hudiliki kutumia maneno mawili kuwa eti ni uzushi. Tunategemea kujibu hoja za namba za simu majina ya watu nakadhalika.
 
Vinginevyo ni muhimu kunyamaza na kufanya mabadiliko ya kimya. Watu huelewa kuwa idara hii ni ya Usalama wa Rais. Lakini kwa kweli ili iweze kuwa usalama wa Taifa ni pale ambapo hata Rais akuhatarisha usalama wa nchi idara inamshughulikia. Nasema hivyo na kama sivyo ilivyo mimi ningehusika nayo ningeijenga hivyo.
 
Napendekeza kuwa Idara hii ijaribu kujisafisha kwa kutojihusisha na mambo ya barabarani ya siasa za wanasiasa ila na ili iweze kujihusisha na maswala ya usalama wa Taifa tu. Madini yetu yanaibiwa. Ufisadi unashamiri na mambo mengi. Wanasiasa wanajilundikia marupurupu mambo hayo yanahatarisha usalama wa taifa letu ndiyo ya kufanyia kazi na kuishauri serikali ifanyeje.

--- On Fri, 7/27/12, flano mambo <flein47@yahoo.com> wrote:

From: flano mambo <flein47@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] IDARA YA USALAMA WA TAIFA YAKANUSHA KUMTESA DR ULIMBOKA STEVEN
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, July 27, 2012, 3:03 AM

Kwa kweli jamani Idara yetu ya usalama inajidhalilisha, mimi binafsi naiheshimu sana. Sasa ni ajabu kuona idara kubwa na nyeti kama ile inatoa maelezo ya tuhuma nzito kirahisi kienyeji kiasi hicho? kumekua na tuhuma nyingi sana kuhusu idara hiyo na jinsi baadhi ya maofisa wanavyotumika hata kwa maslahi ya watu binafsi, vyama vya siasa nk. Ningekua mimi ningetumia nafasi kama hizi kutoa maelezo yenye ushawishi mkuu kwa vielelezo kushinda vile vya gazeti. Hebu angalia sasa huyu ndugu hapo chini alivyouliza maswali? je idara iliposoma gazeti haikua vema kuandaa majibu ikijibu hoja na fact zilizoandikwa kwa gazeti? sasa wanalipiga dongo gazeti ila hawajajibu hoja za gazeti?

Jibuni hoja

From: Reginald Miruko <rsmiruko@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, July 27, 2012 12:49 PM
Subject: Re: [wanabidii] IDARA YA USALAMA WA TAIFA YAKANUSHA KUMTESA DR ULIMBOKA STEVEN

Tuelezeni kwanza Ramadhani Ighondu ni nani? Siku ya tukio alikuwa anamwitia nini Ulimboka? Baada ya kukutana naye waliachana wapi? Amekamatwa na polisi, au ndo yule 'kichaa' wa Kenya? Namba za simu zilizotajwa ni za Rama kweli? Kwa sasa  Rama yuko wapi? Nadhani majibu ya maswali haya ndiyo yalistahili kuwa sehemu ya majibu yenu, lakini kwa haya mepesi hamtupati.

2012/7/27 mwemezi makumba <mwecoma@yahoo.com>
Basi hivyo tu! kweli Serikali ya Kikwete mmetudharau sana watanzania? Idara ya usalama wa Taifa mnatuhumiwa kufanya mauaji na vitendo vya kikatiri kwa raia wanaotumia haki yao ya uhuru wa kujieleza na kudai haki zao halafu mnajibu tuhuma hizo kirahisi rahisi tu? Gazeti mnalotaka tulipuuze limewataja kwa majina na nambazenu za simu na ushahidi mwingine...bado mnadhani tutachagua kuwaamini ninyi hasa baada ya yaliyotokea? Mnafikiri mtaendelea kuchagua kuamini mnachoamini mpaka lini? kwa nini msifungue macho na mkubali kuwa mko uchi kwa sasa..hakuna kinachofanyika ndani yenu kisichojulikana...ulegevu na ubovu wa idara yenu umewafanya mgeukane ninyi kwa ninyi; tamaa ya pesa na ulafi vimewafanya mtumike kisiasa na mkanyage amaadili yenu! Ni ajabu jinsi ambavyo akili ya binadamu inaweza kuchezewa na binadamu mwenzake kiasi cha kuamini kuwa "You are untouchable". Napendekeza kauli hizi mnazotoa kwa umma msingekuwa mnatuletea...ziishie huko huko ikulu ambako pengine wanawaamini. Mnamdanganya huyo jamaa na anaweza kujikuta anashindwa kuongoza kwa sababu mnampotosha au mnamfanya ashiriki katika mipango na maamuzi yenu potofu. Pole sana rais wetu!

From: Damian Gabagambi <gabagambi2005@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, July 27, 2012 11:32 AM
Subject: Re: [wanabidii] IDARA YA USALAMA WA TAIFA YAKANUSHA KUMTESA DR ULIMBOKA STEVEN

No substance.
 
Regards,

Damian M. Gabagambi, PhD.
Senior Lecturer
Sokoine University of Agriculture
Department of Agricultural Economics & Agribusiness
P. O. Box 3007
Chuo Kikuu
Morogoro-Tanzania

Tel: +255 23 260 3411-4 Ext. 4268
Cel: +255 754501541/655501541/786 830730
Fax: +255 23 260 1390
Email: gabagambi2005@yahoo.com; gabagambi@suanet.ac.tz

From: Henry Kaisi <henry.kaisi@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, July 27, 2012 11:22 AM
Subject: [wanabidii] IDARA YA USALAMA WA TAIFA YAKANUSHA KUMTESA DR ULIMBOKA STEVEN

Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza taarifa zenye tuhuma kadhaa
dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Taarifa hizo zimekuwa zikitolewa
kwenye vyombo vya habari zikiihusisha Idara hii na matukio ambayo
yanaidhalilisha na kuzua maswali mengi kwa wananchi. Kati ya tuhuma
hizo ni tukio la kutekwa kwa Dr. STEPHEN ULIMBOKA, Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Madaktari na madai ya kufanywa kwa mipango ya kuwadhuru
baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani. Gazeti moja la kila wiki
limekuwa likurudia tuhuma hizo mara kwa mara kwa madai kwamba ni
habari za uchunguzi na kuihusisha Idara.

Idara inataka kuwahakikishia wananchi kwamba taarifa hizo ni zaUZUSHI
NA UONGO ambazo zina nia ya kuharibu jina na sifa ya Idara. Taarifa
hizo zimekuwa zikiunganishaunganisha vipande vya taarifa mbalimbali
ili kukidhi malengo yaliyokusudiwa na wanaolitumiagazeti hilo. Idara
haikuhusika wala haihusiki na matukio yoyote yaliyotajwa katika tuhuma
hizo. Hivyo tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo.

Matukio yaliyotajwa katika tuhuma hizo yanachunguzwa na Jeshi la
Polisi ambacho ndicho Chombo Chenye Dhamana, na kwa Maslahi ya Taifa
si vizuri kuachia upotoshaji huo uendelee.

Aidha, tunapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa uzushi na tuhuma
zinazotolewa dhidi ya Idara hazitatuvunja moyo bali zitatuunganisha na
hivyo kutuimarisha katika azma yetu ya kuhakikisha nchi yetu
inaendelea kubaki salama kwa kushirikiana na wanachi na Vyombo vingine
vya Ulinzi na Usalama.

Imetolewa na Idara ya Usalama wa Taifa,

Makao Makuu,

DAR ES SALAAM

26 Julai, 2012.

--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
=RSM=

0 comments:

Post a Comment