Kaka Rehani.
Umenena yaliyo ya kweli, kweli tupu. Viongozi wengi wenye uchu wa
madaraka hupenda kufarakanisha kundi hatari ili wazidi kukaa
madarakani, na CCM hilo wanalijua vizuri ndio maana wana nafasi za
fadhira pindi wanapotimiza matakwa yao. Wana kundi la waandishi wa bei
poa ambao ni rahisi kununulika kwa kamera na laptop.
Chadema wanatakiwa wawe makini sana na kundi linalochonganisha
viongozi ili wafarakane yatokee yale yaliyo ikumba NCCR Mageuzi.
On 7/25/12, Selemani Rehani <srehani@hotmail.com> wrote:
>
> Mwalimu Lwaitama,
>
> Nakubaliana na wewe kabisa. Kama kuna jambo ambalo Chadema wanatakiwa kuwa
> macho na kuweka mikakati madhubuti ni hilo la kujaribu kuwagombanisha
> viongozi wa Chadema, kuwachafua na kuwapaka matope hata kwa mambo ya
> binafsi, kuwapaka matope kuwa ni chama cha fujo, vurugu, udini na ukaskazini
> na kampeni zote chafu. CCM haina jipya la kusema bali ni kufanya propaganda
> chafu, kutumia vyombo vya habari na kila mbimu chafu ili tu kukipaka matope
> Chadema. Hawana jambo ambalo wanaweza kuwapelekea wananchi, hawana jipya,
> baada ya miaka 50, na hali hii tulina nayo, watasema nini?
>
> Wakati wa uchaguzi nakumbuka ile tahariri iliyowahi kuandikwa katika gazeti
> la Daily News, sikuamini macho yangu. Nakumbuka wakati ule TV stations
> zilipokuwa zikitangaza habari binafsi kwa muda wa mawiki ambazo hazikuwa na
> tija yoyote kwa mwananchi.
>
> Angalia walivyo mabingwa wa kupindua hoja na kueneza propaganda: Unakumbuka
> ambavyo walivyopotosha matukio yale ya Arusha? Kimsingi agenda ya kudai
> katiba mpya ni ya Chadema, angalia hivi sasa, hilo hata halisemwi na imekuwa
> ni kama agenda yao wakati wao hawakutaka kabisa suala hilo. Halipo katika
> manifesto yao, katika ahadi za papo kwa papo na wala hawajahi kuliunga
> mkono. Siku za nyuma walipinga wazi wazi. Leo tunatoa maoni juu ya uandishi
> wa katiba mpya, huu ni ushindi mkubwa kwa Chadema, lakini hilo halisemwi!!
>
> Angalia walivyopindisha suala la posho na kulifanyia propaganda chafu. Hoja
> ya Chadema ilikuwa na mantiki kubwa sana na kimsingi walikuwa wanapinga zile
> sitting allowances na si zile posho za kujikimu pale mtumishi anapokuwa nje
> ya kituo chake cha kazi" Lakini, suala hilo lilichakachukuliwa na
> kuwachanganya wadanganyika na hawakuweza kuelewa nini ilikuwa hoja ya
> Chadema.
>
> Angaila madai ya Madaktari yalivyochakachuchuliwa na kuonekana kuwa eti
> wanadai milioni saba kwa mwezi!! wakati hoja za msingi ni vifaa tiba na
> upatikanji wa madawa n.k. Hii ndio kazi ya CCM na vyombo vya habari uchwara
> vya Tanzania. Wanaandika habari wakitegemea kuwa watapewa ukuu wa Wilaya au
> ukuu wa Mkoa. Ni aibu. Utashangaa karibu na uchaguzi vyombo vya habari,
> wasanii, na hata mashirika mbalimbali ya umma yatakavyogeuka na kuegemea kwa
> magamba. Hicho ndio kipindi kama navyosema mwandishi mmoja mahiri kuwa "watu
> huvua akili zao na wakazirejesha baada ya uchaguzi". Hii yote ni li-mfumo
> bovu, ambalo kila mtu anafikiri ni muhimu akajipendekeza ili kesho akumbukwe
> katika ufalme.
>
> Ni lazima niseme propaganda hizi chafu zina kuwa very effective kwa sababu
> Watanzania wengi si watafutaji wa mambo, si watafutaji ukweli, hawatafakari
> na wanasahau haraka sana, wanaamini chochote wanachoambiwa na magamba na
> hasa viongozi.
>
> Hivi kweli unaweza kuhusisha mgomo wa madakatari na chama cha siasa??!!
> wakati ni serikali yenyewe ndio ilitumia pesa nyingi katika sherehe za mika
> 50 na matokeo yake kushindwa kuwalipa interns, baadae serikali hiyo hiyo
> ikawakomoa kwa kuwahamisha interns, hapo ndipo chanzo cha mgomo, ule wa
> kwanza. Unahitaji nini kutambua hili?? Ni nani aliwatuma kufanya yote
> hayo??
>
> Wapo wanaoamni kuwa eti propaganda hizi sio effective, yaani hazifanyi kazi,
> ni za kupuuza. Hawa, wanajidanganya, kwa utamaduni wa Watanzania, mbinu hizi
> zinafanya kazi. Chadema inabidi wajipange kweli kukabiliana na siasa hizi za
> maji taka. Mimi ninawaombea. Mungu atawasaidia.
>
> Selemani Rehani
>
>
>
>
>
>
> From: kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Subject: RE: [wanabidii] URAIS 2015 : JOSHUA NASSARI AMKANA ZITTO KABWE
> Date: Tue, 24 Jul 2012 12:57:33 +0000
>
>
>
>
> Magessa,
> Katika nchi hii kwa wakati huu gazeti linaweza kuwa makini lakini wahariri
> na waandishi wake mmoja mmoja wakawa watu wanaoweza kutumiwa na chama
> tawala cha CCM katika mikakati yake ya kila siku ya kujaribu kukibomoa chama
> cha Chadema kwa kuwagombanisha viongozi wake pale kinaposhindwa
> kukigombanisha na wananchi wa Tanzania kwa kukisingizia eti ni chama cha
> mauaji ya yule au huyu na eti kuwa cha viongozi wagomvi na wenye kulea vujo
> mikutanoni na kutoa matusi kama walivyojaribu kufanya kule Singida wiki
> iliyopita... Kwani wewe ukumsikia mkuu wa kaya ziarani Mbeya akirudia
> ujumbe huu wa CCM wa eti viongozi wa vyama vya upinzani ni wagomvi wakati
> wote huku CCM ikiendelea kistaarabu kuwa- bize ikitekeleza ilani ili mwaka
> 2015 wananchi warudishe kwa kishindo? Nina uhakika mchezo huu wa
> kugombanisha Mh Zito na viongozi wenzake ndani ya Chadema utarudiwa tena na
> tena na magezeti makini kama Mwananchi ...Hii si mara ya kwanza wala
> haitakuwa mara ya mwisho.
> Mwl. Lwaitama
>
>
>
>
>
> Date: Tue, 24 Jul 2012 15:37:16 +0300
> Subject: Re: [wanabidii] URAIS 2015 : JOSHUA NASSARI AMKANA ZITTO KABWE
> From: magessabm@gmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> lakini mbona wote wanapinga?haya yalitungwaje na gazeti makini kama
> mwananchi?natafakari!
>
>
> 2012/7/24 Emma Kaaya <emmakaaya@gmail.com>
>
> Katika barua yake kwenda kwa mhariri mtendaji mkuu wa Mwananchi. Hii
> ni sehemu ya waraka huo wa Nassari.
>
> Nukuu hiyo si ya kweli. Nimesikitishwa sana na upotoshaji mkubwa wa
> kunilisha maneno mdomoni uliofanyika katika sehemu kubwa ya habari
> hiyo (mbali na nukuu hiyo) kwa maslahi ambayo sijui ni ya nani.
>
> Wakati ukijiandaa kuchukua hatua kutokana na sababu ya pili ya
> kukuandikia barua hii ambayo nitaieleza punde hapa chini, naomba
> utafakari masuala kadhaa, ikiwemo; kwa nini ilichukua siku zaidi ya
> tano kwa habari hiyo kuandikwa?
>
> Pili, kutokana na usumbufu mkubwa ambao nimeupata kutoka kwa
> Watanzania wa maeneo mbalimbali wanaotarajia kuniona mwakilishi wao
> nikizungumzia masuala yanayowahusu wao, ambayo ni muhimu zaidi kuliko
> jambo jingine lolote kwa sasa.
>
> Lakini pia nikiwa Mtanzania anayetambua umuhimu na unyeti wa nafasi ya
> urais katika nchi hii na kwamba inaamuliwa kwa maslahi mapana ya umma
> wa Watanzania wala si uchu wa watu wachache, hivyo nisingeweza kutamka
> maneno hayo ambayo gazeti lako limeandika, naomba kukuandikia rasmi
> kukutaka ukanushe habari hiyo ukurasa wa mbele kwa uzito huo huo
> ulioipatia habari hiyo katika toleo tajwa.
>
> Lakini pia nikiwa Mtanzania ambaye ni mwanachama wa Chama cha
> Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho kinaamini kuwa kwa sasa
> suala la urais si kipaumbele, bali muhimu kwa wakati huu ni
> kushughulika kujua mizizi au vyanzo vya matatizo makubwa
> yanayowakabili Watanzania ikiwemo umaskini, ujinga, maradhi, ufisadi
> na utawala mbovu wa CCM, kwani serikali imekuwa ikishughulikia
> matokeo.
>
> Kama ambavyo chama changu, Watanzania wengine makini na mimi mwenyewe,
> naamini kuwa kwa sasa suala la muhimu kwetu kama taifa ni kutafuta
> mizizi au vyanzo vya matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ya
> Watanzania.
>
> Kwa chama changu na mimi mwenyewe pia kama mwakilishi makini wa
> Watanzania, naamini kuwa siku zote suala la urais linategemea mahitaji
> ya Watanzania na kamwe haliwezi kuamriwa kwa kufuata matakwa na utashi
> au uchu wa watu binafsi.
>
> Lakini pia suala la nikiwa kama mwanachama mwaminifu wa CHADEMA na
> ninayeipenda nchi yangu kwanza, naamini kuwa suala la urais linafuata
> katiba, kanuni na taratibu za chama, hatua ambayo haijafikiwa kwa
> sasa.
>
> Naomba kusisitiza kuwa sijawahi kutamka, siwezi kutamka na sitarajii
> kutamka maneno hayo uliyoyaandika kwenye gazeti tena kwa kuninukuu na
> kuniwekea maneno mdomoni. Naomba kurudia tena kukutaka ukanushe habari
> hiyo ukurasa wa mbele kwa uzito huo huo ulioipatia habari hiyo katika
> toleo tajwa.
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
>
>
> --
>
>
> Sent from Samsung Galaxy Ace GT-S 5830 --The future of Android Technology
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
--
"Tukosoane, Turekebishane, Tuwajibishane, ndipo Tusameheane". Regia Mtema.
--
+255 (0) 713 (784) 24 67 64.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment