ni kweli kabisa
On Thursday, May 24, 2012 1:57:37 PM UTC+3, Yona F Maro wrote:
> Mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya TAIFA ametoa taarifa
> inayojirudia kwenye magazeti kadhaa kuhusu Mamlaka hiyo kugundua
> upungufu kadhaa kwenye taarifa za wafanyakazi wa mejeshi yetu ya
> ulinzi na usalama .
>
> Taarifa hizo zilikuwa zinahusu ujazwaji majina katika fomu za kuombea
> vitambulisho vya taifa ambazo zilitolewa kwa wafanyakazi hao wa
> majeshi ambapo taarifa nyingi zilizozazwa zilikuwa tofauti na zile
> zilizokuwepo maeneo mengine .
>
> Inasemakana suala hili limesababisha hata uzinduzi rasmi wa kufungua
> mamlaka hiyo ili kila mtu achukuwe fomu za kuomba kitambulisha cha
> taifa kuahirishwa mpaka pale itakapo tangazwa tena .
>
> Dickson mwaimu ambaye ni mteule wa raisi naamini amepitia taratibu
> kadhaa zinazohusiana na ulinzi , uwezo wake na mengine kabla ya kupewa
> wadhifa huo , lakini hili la kuanika udhaifu wa majeshi yetu tena kwa
> kutumia fedha zetu kwenye magazeti kwa kujirudia inaonyesha udhaifu
> mkubwa wa mtendaji huyu haswa unaohusu mawasiliano kati yake na
> taasisi nyingine za ulinzi na usalama .
>
> Mkurugenzi huyu angekuwa safi na angekuwa na nia nzuri na majeshi yetu
> kabla ya kwenda kwenye vyombo vya habari na kutoa taarifa hizo
> angehakikisha kwamba anawasiliana na majeshi mengine ili kuweza
> kumaliza tatizo hilo haraka na mapema ili masuala mengine yaweze
> kuendelea kama kawaida na kusingekuwa na usumbufu wowote kama huu
> unaoendelea kusumbua ndani ya majeshi yetu sasa na baadhi ya viongozi
> katika serikali .
>
> Suala la kuwa na taarifa tofauti linajulikana kwamba kuna wengine
> wameowa au kuolewa na kubadilisha majina yao , wengine wamebadili
> dini , wengine wameamua tu kubadilisha majina yao kwa sababu Fulani na
> ni haki ya msingi ya mwanadamu kubadili hivyo vitu sheria haikatazi .
>
> Kwa kumalizia naomba serikali ihakikishe inaajiri wasemaji katika kila
> taasisi yake iliyo nyeti haswa hizi zinazohusu ulinzi na usalama wa
> watanzania ili wawe na kazi ya kutoa taarifa na kutoa maelezo mengine
> kwa umma na kama wanapokosea basi wakurugenzi wa taasisi hizo au
> makatibu wakuu au waziri ndio wanaweza kuwa wa mwisho katika kutoa
> ufafanuzi au kueleza jambo Fulani .
>
> Utoaji wa taarifa au upatikanaji ni haki ya kila mtu lakini una mipaka
> haswa pale taarifa hizo zinavyohisisha vyombo vyetu vya ulinzi na
> usalama lazima tuwe makini na tujenge uzalendo zaidi kwa taifa letu
> tusitake sifa za kijinga .
kabisa
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment