Wednesday, 25 July 2012

Re: [wanabidii] Ufafanuzi wa Mhe Zitto Kabwe Kuhusu kusafishiwa Njia ya Urais 2015

If this is his time and if he is God's chosen, let it be. Why fearing this? At the end every human being will remain who it is. No matter who leads us. yeyote mwenye nia njema na ya dhati ya kuthubutu kuomba ridhaa ya kuwa rais  ana haki kikatiba. Na kama ni chaguo la Mungu hakuna atakayezuia. Ila kama sio chaguo la mungu basi tutena kwenye mateso makali zaidi. Uongozi wowote wa juu ni mtakatifu/mtukufu. Kama kwa bahati mbaya hatutaongozwa na hekima ya mungu tukaweka wrong number, then we are doomed. Ni vizuri tuendelee kutafakari na sioni sababu kwa nini wananchi wasiendelee kuongea wanachohisi kinafaa baabaye. Ni kama mama anayetarajia kujifungua miezi kadhaa ijayo, watu wa karibu wataendelea kuoredict na kuongea ongea juu ya ujio huo. na hasa kipindi hiki ambambo tumekata tamaa sana na hakuna cha kutuondoa hapo tulipo. It is like an opium. Hardship and yet we are thinking for a greater future. Well, may we be blessed so that we always have healthy thinking and the best choice on place.

2012/7/24 Azaveli Lwaitama <kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com>
Magessa,
Ukisoma kwa makini  kile kinachoitwa nukuu za waliyosema Wabunge Hakima na Nassari na kichwa cha habari cha stori ya gazeti la Mwananchi utagundua tu kuwa wale wabunge hawakuwa wanazungumza juu ya nani watapendekeza Chadema impendekeze kama mgombea wa Urais kwa mwaka 2015 bali walikuwa wanasema kuwa wakati wowote taifa litakapo ona ni muafaka Mh.  Zito kuwa Rais wao wataunga mkono hoja hiyo...Sasa kichwa cha habari cha eti wabunge wa CCM na wa Chadema walikaa mahali wakakubaliana kuwa Mh. Zito ndiye mgombea  2015 kilikuwa na lengo gani kama si kuzusha jambo ndani ya Chadema kwa matumaini kuwa litakivuruga Chadema. Ndiyo maana wala haikuitaji eti washinikizwe na mtu ndipo Mh.Halima na Mh. Nassari wakanushe kujenga hoja nje ya taratibu za  chama chao za kuunga mkono Mh. Zito kugombea Urais 2015... Yeyote aliyeandika stori ya gazeti la Mwanachi alitaka kuanzisha mjadala juu ya jina la mgombea wa Urais nje ya taratibu ambazo vyama vya CCM na Chadema wamejiwekea...Lengo lilikuwa kutafuta kuimbua mifarakano ndani ya Chadema ...Bila hata ya kushinikizwa na mtu ilibidi Mh. Halima Mdee na Mh. Nassari wakanushe kutoa kauli zilizolenga kuibua mjadala juu ya eti mgombea wa Urais mwaka 2015 kwa wakati huu...
 
Lengo la stori ya gazeti la Mwananchi lilifanikiwa kiasi kwani naona hata wewe Magess tayari umejiaminisha kuwa eti "kwa kutafakari kidogo tu haya yalioandikwa na zitto..ni kwamba wabunge wale waliyatamka waliyonukuliwa kuyatamka ktk tamasha lile, pengine walilazimishwa kuyakanusha!" Lengo lilikuwa ni kuibua mjadala juu ya jina la  mgombea badala ya maswala yatakayo kuwa muhimu kuzingatiwa katika kila chama kupendekeza jina la mgombea kwa wakati huo... Wabunge wote wale pamoja na Halima na Nassari inwezekana kabisa walisema Mh Zito anafaaa kuwa Rais kama ambavyo hata wao Mh Halima na Mh. Nassari wanavyofaa kuwa Rais... Kusema hivyo si kusema walikuwa wamedhamilia kupendekeza kuwa mwaka 2015 Mh. Zito lazima ndiye awe mgombea. Hiyo ni kupindisha mantiki ya hoja ya kusema siku yoyote chama chake kikiona inafaa Mh. Zito anazosifa za kupendekezwa. Stori ile ya gazeti la Mwananchi ilisukumwa na vimichezo vya Ze Komedi vinavyochezwa na CCM kutafuta kubaki madarakani milele kwa kutumia mbinu ya wagawe uwatawle kwa kuegemea mambo ya juu juu lakini ambayo yanauwezo mkubwa wa kuwagawa watu kama  maswala ya dini, kabila, na umri.
Mwl. Lwaitama

Date: Wed, 25 Jul 2012 10:10:59 +0300

Subject: Re: [wanabidii] Ufafanuzi wa Mhe Zitto Kabwe Kuhusu kusafishiwa Njia ya Urais 2015
From: magessabm@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

kwa kutafakari kidogo tu haya yalioandikwa na zitto..ni kwamba wabunge wale waliyatamka waliyonukuliwa kuyatamka ktk tamasha lile, pengine walilazimishwa kuyakanusha!

2012/7/25 Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
na Zitto Kabwe

Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012, kulikuwa na habari
yenye kusomeka 'Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015'. Habari
hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala umekuzwa
zaidi baada ya Wabunge ndugu Halima Mdee na ndugu Joshua Nassari
kukanusha maneno waliyonukuliwa kusema. Napenda kusema masuala
yafuatayo.

Moja, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola,
Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David
Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa
kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi.

Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwemo Joseph
Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamata na Peter Serukamba.
Wabunge hawa hawakualikwa na mimi na wala sikufanya mazungumzo nao
yeyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumza au
hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa.

Waheshimiwa wote walipewa nafasi ya kusalimia na wote walizungumza.
Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo ni ndugu Halima Mdee,
Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.

Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na
video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya
documentary ya tamasha lile la kihistoria.

Pili, sikuhusika kwa namna yeyote ile na kuandikwa kwa habari hii
iliyozusha mjadala. Wala sikujua kama habari hii ingeandikwa maana
katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja maana nilitaka liwe
tukio la Kigoma tu.

Kama mwandishi kaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi
itaonekana kwenye videos hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi
zao nini walisema Kigoma na kipi kiliwasukuma kusema walioyasema
Kigoma. Nisingependa kuhusishwa kwa njia yeyote ile na matamshi yao,
habari iliyowanukuu na hata makanusho yao. Maana mwisho wa siku ukweli
ndio utasimama.

Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya
kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya
urais yanapotajwa zinashangaza sana.

Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea
Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Urais mpaka hapo mchakato
utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha
bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii
na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa
hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.

Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema
'weka akiba' sio akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba
ya maneno. Tusimalize yote.

Zitto Kabwe

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--

Sent from Samsung Galaxy Ace GT-S 5830 --The future of Android Technology

0 comments:

Post a Comment