Tuesday, 28 July 2015

[wanabidii] CHADEMA lazima ijiandae kukabiliana na mambo yafuatayo...

CHADEMA lazima ijiandae kukabiliana na mambo yafuatayo...

Hata kabla ya kuja kwa Lowasa ndani ya CHADEMA kulikuwa kumeanza kuonyesha dalili mbaya sana;

Mosi, katika kura za maoni; kuna malalamiko mengi sana ya kujihusisha na rushwa kwa baadhi ya wagombea wa ubunge. Changamoto kubwa ni kwamba ushahidi wa rushwa ni mgumu mno kuuthibitisha. Ikumbukwe kuwa hata ndani ya CCM kulianza na minong'ono ya rushwa kutoka kwa watu wa kawaida lakini viongozi wakawa wanaziba masikio kwa pamba leo hii rushwa inakitesa chama cha mapinduzi.

Pili, kuna baadhi ya makada waliotoka CCM na hata wale waliokuwepo ndani ya chama wamebadili kabisa njia ya ushindini, kwani kwa sasa njia wanayoiamini sana ni kutoa rushwa, wengi wao wameshinda kura za maoni ndani ya CHADEMA, na wengine ndani ya Chadema wanaamini katika ushindani wa hoja tu na si rushwa hawa ni wachache sana na nafasi yao kwa sasa ndani ya chama inafifia sana tena mno kwa sababu nguvu ya PESA kwa sasa ndani ya CHADEMA imeingia kwa kasi.

Tatu, Hatari nyingine ninayoiona ndani ya chama ni kupenda mno vitu vya Uliberali kuliko vya Kijamaa. CHADEMA inaamini katika Mrengo wa kati yaani mazuri ya Ujamaaa na ya Uliberali. Mimi naona chama kimeegemea sana kwa sasa kwenye Uliberali wakati kimefika hapa kilimo leo kwa sababu ya kuegemea sana kwenye Ujamaa wa Kisasa. Bila kurudi kwenye Ujamaa wa kisasa naona hatari sana ndani ya chama.

Nne, Ujio wa Lowasa una faida na hasara. Mosi, endapo kundi la Lowasa litaanza kuwanyang'anya makada wa CHADEMA nafasi walizonazo kwa kisingizio kuwa hawana hela za kufanya siasa ndani ya chama, kuna hatari sana ya CHADEMA kukabiliana na upinzani mkubwa ndani ya chama kuliko wakati wowote ule. Pili, Kuna kundi kubwa bado lina mini katika Dr. Slaa nalo linatakiwa baadae lipewe maelezo ya kutosha kabisa kuwa kwa nini Dr. Slaa asigombee URAIS. Hasara yake nayo iko kwenye kuaminisha Watanzania kuwa ni fisadi na kwa sasa kuwashawishi kuwa Lowasa si fisadi hili jambo litaitesa sana CHADEMA.

Tano, shutuma za ufisadi kama silaha kubwa ya CHADEMA lazima wataalam wa siasa ndani ya chama wajiandae kuja na hoja zenye mashiko ili kuendeleza neno hili ambalo limeonekana kwa muda mrefu kama nguzo ya CHADEMA.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment