Tuesday, 28 July 2015

[wanabidii] Ndoto za slaa zimezimika ghafla, za lowassa zinazimika oktoba

Kwa sababu ya ujanjaujanja tu, kwa sababu ya usanii usanii tu, kwa sababu ya pesa ndoto za Dr. wilbroad Peter Slaa zimezimika. Lowassa naye ndoto zake zinazimika mwezi Oktoba baada ya uchaguzi mkuu. lowassa anajua kabisa hawezi kuwa rais lakini anapoteza nini kuondoka CCM au kukaa CHADEMA? Ndiyo faragha pekee anayobaki nayo.

Pole za pekee kwa Dr. Slaa, ulifanyakazi kubwa sana ya kukijenga chama na nadhani sasa utakuwa unakumbuka mizengewe aliyofanyiwa ZITTO. Nakumvuka kauli yako wakati ZITTO ana mgogoro na CHADEMA pale uliposema "HAMNA TATIZO NA ZITTO, BALI WATU WABAYA WENU WANATAKA KUWACHONGANISHA" jambo ambalo hukujua ni kuwa wabaya walikuwa ndani ya CHADEMA. Pole sana Dr. Ndoto za Urais zimeishia hapo. Pole sana Josephine Mshumbusi, ndoto za kuwa first lady zimeishia hapo, ngoja Regina Lowassa naye ajaribu bahari hiyo.

0 comments:

Post a Comment