Friday 2 September 2016

[wanabidii] UDIKTETA, USULTANI ULIINGIA CHADEMA MWAKA 2006 WALIPOFUTA UKOMO WA MADARAKA KWENYE KATIBA

UDIKTETA, USULTANI ULIINGIA CHADEMA MWAKA 2006 WALIPOFUTA UKOMO WA MADARAKA KWENYE KATIBA

 

Na Daniel Mbega

 

FREEMAN Aikaeli Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anahamaisha wanachama wake wafanye maandamano Septemba Mosi, 2016 kwa kile anachokiita ni 'Operesheni ya Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta)'.

Anasema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli inaendeshwa kidikteta hasa baada ya majaribio yao ya kuitikisa kwa kususia vikao vya Bunge kushindwa huku serikali ikipiga marufuku mikutano yote ya siasa na kuwahamasisha wananchi wafanye kazi za maendeleo.

Mbowe amekwenda mbali zaidi baada ya kuwatisha viongozi wa chama hicho kwamba yeyote ambaye hatashiriki maandamano aliyoyapanga yeye na kuwashawishi viongozi wenzake wayakubali, basi atakuwa amejitoa kwenye uongozi kwa sababu ni 'msaliti'.

Niliandika hivi karibuni kwamba, lingekuwa jambo la busara sana kama Chadema wangeanza kwanza na Operesheni ya Kupambana na Udikteta ndani ya Chadema (Ukucha) kabla ya kuanzisha Ukuta, lakini baadhi ya watu walinikosoa.

Leo nataka kueleza kwamba, ingawa viongozi wa Chadema wamekuwa na kawaida ya kukanusha kwa nguvu zote huku wafuasi wao wasiopenda kujiongeza kwa kutafakari mara mbili wakiunga mkono, lakini udikteta umeshamiri ndani ya chama hicho na zaidi kuna usultani uliotamalaki. SOMA ZAIDI: http://goo.gl/kxKXKk


--
DANIEL MBEGA
INVESTIGATIVE JOURNALIST, BLOGGER, RESEARCHER & PUBLISHER
CELL: +255 767 939 319/ +255 715 070 109
WHAT'S APP: +255 656 331 974
BLOGS: www.kilimohai.wordpress.com
               www.brotherdanny5.blogspot.com

"Kama hawatuwekei mgombea mzuri, kwanini watutawale?" Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam, 1995

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment