Thursday 29 September 2016

Re: [wanabidii] WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINAADAM NIELIMISHENI

Yesu alisema mkiwapenda wanao wapenda mtakuwa mmefanya jambo gani jipya, maana hata waovu hupendana. Wapendeni ADUI zenu kama baba yenu wa mbinguni anavyowapenda. Huwanyenyeshea mvua wahovu na wema. Kama hatuwezi hatuwezi kuumba mtu hata mmoja ushujaa wa kuua tunauazima kwa nani?



From: 'Mashaka Makana' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, September 28, 2016 3:35 PM
Subject: [wanabidii] WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINAADAM NIELIMISHENI

Habari wote katika jamii! Naomba kufahamu MSINGI wa kuanzisha shirika la kutetea haki za binaadamu! Mwezi huu wenzetu wa Kagera walipatwa na madhara ya kuumia na wengine kufariki. Nini mchango wa wanaharakati wa haki za binaadamu kwa majanga ya aina hii? Au kwa uhalisia wanaharakati wa haki za binaadamu mmefanya nini kwa tukio hilo? Mbona hamsikiki kama ilivyo katika matukio mengine mfano police wakitumia nguvu zaidi kudhibiti mfano waandamaji- mara moja utaona au kusikia mikutano na waandishi wa habari kutoa matamko ya kulaani na nk. 

Kwali lingine naomba kuelimishwa, mtu aliekufa ana haki gani kama kifo chake kilitokana na kupigwa au kunyongwa au kupigwa risasi na wahalifu? Hapo je, wanaharakati hakuna kazi ya kufanya? Hili swali linawahusu pia wale wanaopinga adhabu ya kifo. Mfano mdogo tu, janga la tetemeko limeua watu Kagera na wengine wengi wanalala nje na wengine darasani na watoto wanasoma na wahanga wakiendelea kuishi darasanina wengine kuhitaji matibabu na makazi halafu unasikia au kushuhudia mtu au kikundi cha watu wanahujumu michango hiyo ya wahanga! Je huyu si muuaji? kwa nini asiuawe au wasiuawe hawa?

Naomba kuelimishwa!
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment