Friday 30 September 2016

Re: [wanabidii] WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINAADAM NIELIMISHENI

Watu wanaangalia tumboni street Ludovick sio kuangalia haki za binadamu kiuhalisia. Unaangalia unapata wapi funding ya shirika lako au donor wako nani na unausoma muelekeo wake na anataka nini ambapo wewe budi uzingatie ili uapate hela zaidi ktk shirika lako, scholarship na trips nyingi za ulaya na warsha nchini, matamko ya media. Hapo ndipo wanapokiuka maadili ya kazi ay utetezi wa Haki za Binadamu. Huangalii uhalisia wa tatizo uwe neutral.

Mimi hualamika sana yanayoendelea mkoa wa Morogoro na kwingineko. Mfugaji anatoka kilomita 800 hadi kijiji cha kilosa au ngerengere. Analishia shamba mifugo kisha anachapa raia. Lakini harakati na wazungu wao wanaowapa hela daima research zao na uharakati ni mfugaji anaonewa na sio mfugaji wa kabila lingine ila la Maa Groups. Leo hii Bunju, Kiromo, Ruvu Bagamoyo mabonde ya mpunga na kilimo cha mbogamboga kumejaa wafugaji. toka lini Bunju, Kiromo kukawa na Mmang'ati. mmasai-Chalinze, Magindu lakini sio Kiromo, Saadani. Leo hii wakulima na wavuvi ya Mlingotini au Nyamisati na Utete Rufiji hawana amani. Lakini ukienda Manyara, Munduli, Loliondo na ndani ya NCAA wao wafugaji wamejaza mifugo kwa maelfu, wanalima kwa treka na plau za kukukotwa na ng'ombe wanauza mazao na kujilisha na wakiuza kujaza mifugo zaidi beyond land's carrying capacity. Lakini hawalishii mifugo mazao yao na mzaramo hawezi kuhamia Monduli eti avamie tu na kuanza kulima! Anajipenda au vipi? Lakini daima wazungu na washenga wao-wafugaji wa kimasai wanaonewa! Jee wanavyozidisha mifugo hiyo na kulima ambapo walikuwa hawalimi si wanamaliza ardhi yao ya kuchungia na kulisha mifugo? No-jibu serikali inawaonea kwa kuweka conservation areas? Mbona Conservation areas nyingi za wanyamapori na misitu maji zipo kwa wakulima. Protected forests zimezuia kilimo ili maji yapatikane hawa jee hawaonewi? Forests hizo zina wanyama pia na National Park kama Sleous, Mikumi, Udzungwa, Ruaha etc zipo kwa wakulima na wafugaji wanakuja kuhamia humo? Utaona upendeleo uliopo kwetu sisi wenyewe kujikanyaga na kujionea unatokana na Tumboni Street. Kujifanya tunatetea Haki za Binadamu na kuilaumu serikali kuonea lakini hatuangalii pande zote. Hata vyama vya siasa ni kujaza tumbo tu ili donors wao waendelee kuwapa hela. Huwezi ukaona kiongozi anayechachamalia demokrasia akafanya bidii pale alipo ktk jimbo lake kuhamasisha maendeleo na Sera, sheria, miongozo ipo. Ila yupo kuhamasisha kupinga na kuharibu utekelezaji akitegemea kukuza jina lake tu na mafao toka donors. Jimbo lake resources zipo, manpower ipo ila maendeleo-wachache sana huyazingatia. Ila safari, vikao, mapigano na vyombo vya sheria na Media kukusa matukio ndio issue.

Mtu wa Media swali kuu si kuwauliza wananchi maswali ya kuelimisha mfano kwa nini mnatupa taka hapa kwenye chanzo chamaji au mfereji wazi, kwa nini unaona hii ni barabara au reli na unajenga hapa na unaona kabisa. Huu mtaro umejaa maji ya kinyesi inaonekana bomba hili wewe umeunganisha kuyaleta hapa kwa nini unafanya hivi? Haulizi haya ya kuonyesha kwa video yake ila atauliza uchafua huu unawapa shida gani na mnaiambia nini serikali? Mnaishauri ifanye nini?! Hao ndio watanzania. Ukifika nje za ofisi za NGO za Haki za Binadamu-angalia mazingira ya nje. Mitaro imejaa takataka, imeota majani, ina malundo ya taka ngumu, kuna biashara wazi mainzi yamejaa, bar mpaka usiku wa manane, makelele ya music kwenye makazi yenye watoto wadogo na vitoto vinajiuza umalaya nje ya majengo hayo. Ila maandamano yap[o kisiasa zaidi. Haki sio kisiasa tu bali kiafya, kimazingira, kimakazi salama. Hatujitambui, hatujielewi, ndio maana tupo hapa tulipo pamoja na kuwa na mifumo mizuri Kisereikali, kijamii.
Kama ni haki basi hata police au mgambo anapofukuzwa na aria na kupigwa mawe kwa kutekeleza sheria, kuuawa NGO za Haki za Binadamu sekta zote na sekta husika-ziwajibike na kukemea. Za mazingira-sisilale raia wanapoyaharibu. Za Jinsia-zichakalike baba anapobaka kuhakikisha kesi inachukua muda mfupi na wanaomlipia dhamana kuvuriga kesi wawekwe ndani maana ushahidi mpaka wa DNA upo sasa dhamana ya nini? Sio tu anapobaka mwenyekiti au mchungaji mpaka ndugu wa damu. Vamia danguro zote zifungwe na wamiliki wakae jela maisha. Hapa Kazi tu ili tulikomboe taifa. Wakili unayemtetea mbakaji evidence zipo unataka nini wewe si ufungwe tu? Mtu kahukumiwa kifungo cha maisha unakuta alibaka lakini baaya ya miaka 5 ametoka msamaha wa Rais ulipotolewa ameinginzwa ktk msamaha katoka! Funga huyo aliyemtoa akae maisha jela.

Jana nimeambiwa mkulima Ruvu ya Bagamoyo alimwaga dawa ya magugu ili apande mpunga wake wagungu yakifa. Mwenyemifugo akaingiza mashambani ng'ombe zikala majani hayo kwenye birika la irrigated rice wakafa. Yeye mfugaji alimkuta mtu mwingine sio mmiliki wa shamba hilo akampiga mkuki ta tumbo ukatokezea upande wa pili yupo hoi kalazwa hospitali Bagamoyo. Haki hizi za kulishia mashamba mtu kwao na customary land yake, unampiga ,mkuki unaua-mbona hatuoni maandamano na warsha kutetea wakulima bali zaidi wafugaji kuonewa. Hawa wanatoka mbali na kuzagaa nchi nzima. Tunahitaji sasa sheria ya kila mtu akae kwake hakuna kuzurura na mifugo. Ikipatikana-ikamatwe na kuuzwa. Ikiingia Parks na protected forest-kamata, uza utumie hela kwa uhifadhi.

Andamaneni tu kutetea haki za kujaza matumbo yenu ila tuendako kubaya. Ua polisi uwape nafasi majambazi kwani polisi hatofika kupambana na majambazi eneo ambapo mlipiga police wa kutuliza fujo na wa ulinzi. majambazi yatakesha yanakula, yanalewa ndani ya majumba na yanabaka mpaka vichanga mbele ya macho yako. Hata USA unaona jinsi polisi wanavyouawa wakipambana na waandamanaji ay wavunja sheria lakini jeshi linaendelea pia kuwabonda hao wanaovunja sheria na kuwaua wasipozingatia amri. Huko kwenye Demokrasia wanapambana pia vipi daima hapa bongo ni serikali tu inayokosea haina haki? Akiuawa askari ni sawa akibondwa mawe ni raha na furaha kwa wanaharakati wakae kimya? Kwa Somo (askari) kunaliwa na kwa Mwali pia (Raia)!!

Kama Kawa
--------------------------------------------
On Fri, 30/9/16, Joseph Ludovick <josephludovick@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINAADAM NIELIMISHENI
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, 30 September, 2016, 6:21

Hakuna aliye
jibu MASWALI ya Muhingo. Maana haya asemayo Magobe tumeuliza
tukiwa tunayajua. Swali ni hivi, Lissu kukamatwa akalazwa
ndani bila Dhamana inakiuka haki zake zaidi kuliko askari
anayeuliwa akiwa kwenye majukumu yake?

Swali liko hapo. Uswahiliswahili tuache!

Mimi naijua sehemu ya jibu sahihi. Wana harakati wa hapa
bongo wengi ni tawi ama basi mapandikizi ya CHADEMA! Nani
anataka kubisha!?
On 29 Sep 2016 22:11,
"'ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:


Basi ipo haja kurudi nyuma na kuunganisha maneno. HAKI NA
WAJIBU WA BINADAMU.

Kama kweli madhali mtu kavaa magwanda ya uaskari akifaniwa
gasia na mtu ambaye hakuvaa magwanda basi wanaharakati
wanakaa kimya hiyo ni kasoro kubwa maana na askari ni
binadamu. Kama kundi la watu likiji-organise na kuanza
kunyanyasa maaskari mwanaharakati hahusiki nalo basi
uanaharakati ni ajera mbaya

------------------------------ --------------

On Thu, 9/29/16, Telesphor Magobe <tmagobe@gmail.com>
wrote:



 Subject: Re: [wanabidii] WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINAADAM
NIELIMISHENI

 To: "wanabidii@googlegroups.com"
<wanabidii@googlegroups.com>

 Date: Thursday, September 29, 2016, 3:07 PM



 1.Kwa maoni yangu, haki

 za binadamu ni kanuni za msingi za maisha zinazopaswa

 zilindwe na mamlaka ya nchi ili raia waishi maisha ya
heri

 (kanuni zinazolinda ustawi wa raia na mali zao).

 2. Kanuni hizi za msingi ni kama

 vile: kuishi, kuheshimiwa, kupata riziki halali ya
maisha,

 kutekeleza majukumu ya kifamilia, kijamii, kupata
elimu,

 huduma za afya, maendeleo nk.

 3.

 Jambazi kumwua polisi au raia au mume kumpiga mkewe au
mtoto

 ni mambo ambayo yako nje ya haki za binadamu, lakini
yako

 ndani ya makosa ya jinai kwa mujibu wa sheria za nchi.
Ila

 polisi au mtu yeyote mwenye mamlaka ya kiserikali
akimwua

 raia (kama si katika kujilinda au katika kutekeleza
wajibu

 wake kisheria na unaoendana na kanuni za kimataifa

 zinazolinda ustawi wa watu) basi hata hapo haki za
binadamu

 zimeguswa.

 4. Kimsingi, haki za

 binadamu ni madai halali dhidi ya mamlaka ya nchi -
yaani

 yale ambayo mamlaka ya nchi inapaswa iyatekeleze kwa
raia

 wake.

 5. Mamlaka ya nchi ikitekeleza

 inakuwa kwamba nchi fulani inaheshimu haki za binadamu
na

 ikishindwa/kukiuka au kupuuza inakuwa kwamba nchi
fulani

 inavunja haki za binadamu.

  



 2016-09-29 14:11 GMT+03:00

 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:

 Loh swali

 zuri sana. Na mimi ni mmoja kati ya watakaofaidika japo

 nilikuwa naona aibu kuuliza.



 Zamani sana katika mjadala mwanasheria mmoja alibwatuka
neno

 ovu kabisa Akaseka " LENGO KUU LA HAKI ZA BINADAMU
NI

 KUMTENGANISHA MWANADAMU NA MUNGU" Kabla hajaongeza

 nikamvaa. Nikamshambulia.Akaniangalia kwa dharau. Mwisho
wa

 maneno yangu akasema "Wewe ndugu naona una akili.

 Subiri wakati ukifika tumia akili zako kuelewa."

 Nikamuuliza wakati gani? Akasema pale itakapotangazwa
kuwa

 NGONO NI HAKI ZA BINADAMU. Nikamwambia mpaka kurudi kwa
Yesu

 hakutatokea kitu hicho. Ilipotokea namtafuta sana
kuntaka

 radhi.







 Jingine: Huwezi kuwasikia wanaharakati majambazi
wanapomuua

 Polisi. Hawathibutu kusema. Lakini Polisi akithubutu tu

 hutajua walikotokea.







 Jingine: Kuna mataifa ndiyo tu yanayoweza kutoa tafsiri
ya

 gaidi. Angola ilipambana na gaidi Savimbi lakini
usingesikia

 akiitwa gaidi labda Nyerere tu. Ghadafi aliitwa gaidi
na

 mataifa hayo kila mwanaharakati akamwita gaidi. Kuna
mmoja

 nilimuuliza kwanini unamwita Gadafi gaidi akaniuliza
kama

 juzi nilisikiliza VoA. Yaani kwake ni gaidi kwa sababu
VoA

 ilimwita gaidi. Sasa hivi Urusi inaisaidia Syria
kupambana

 na magaidi lakini husikii wanaharakati wakisema. Ila
Asaad

 ndiye anaitwa muuaji. Ukiuliza watasema Husikii VoA
nini?

 Atakayejibu atusaidie mpaka huko.



 Muhingo







 ------------------------------ --------------



 On Wed, 9/28/16, 'Mashaka Makana' via Wanabidii

 <wanabidii@googlegroups.com>

 wrote:







  Subject: [wanabidii] WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINAADAM

 NIELIMISHENI



  To: "wanabidii@googlegroups.com"

 <wanabidii@googlegroups.com>



  Date: Wednesday, September 28, 2016, 3:35 PM







  Habari



  wote katika jamii! Naomba kufahamu MSINGI wa
kuanzisha



  shirika la kutetea haki za binaadamu! Mwezi huu
wenzetu

 wa



  Kagera walipatwa na madhara ya kuumia na wengine

 kufariki.



  Nini mchango wa wanaharakati wa haki za binaadamu kwa



  majanga ya aina hii? Au kwa uhalisia wanaharakati wa
haki

 za



  binaadamu mmefanya nini kwa tukio hilo? Mbona
hamsikiki

 kama



  ilivyo katika matukio mengine mfano police wakitumia

 nguvu



  zaidi kudhibiti mfano waandamaji- mara moja utaona au



  kusikia mikutano na waandishi wa habari kutoa matamko

 ya



  kulaani na nk. 



  Kwali lingine naomba kuelimishwa, mtu aliekufa ana



  haki gani kama kifo chake kilitokana na kupigwa au

 kunyongwa



  au kupigwa risasi na wahalifu? Hapo je, wanaharakati

 hakuna



  kazi ya kufanya? Hili swali linawahusu pia wale

 wanaopinga



  adhabu ya kifo. Mfano mdogo tu, janga la tetemeko

 limeua



  watu Kagera na wengine wengi wanalala nje na wengine



  darasani na watoto wanasoma na wahanga wakiendelea

 kuishi



  darasanina wengine kuhitaji matibabu na makazi halafu



  unasikia au kushuhudia mtu au kikundi cha watu

 wanahujumu



  michango hiyo ya wahanga! Je huyu si muuaji? kwa nini



  asiuawe au wasiuawe hawa?



  Naomba kuelimishwa!















  --







  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com







   







  Kujiondoa Tuma Email kwenda







  wanabidii+unsubscribe@

 googlegroups.com 
Utapata Email ya



  kudhibitisha ukishatuma







   







  Disclaimer:







  Everyone posting to this Forum bears the sole

 responsibility



  for any legal consequences of his or her postings,
and

 hence



  statements and facts must be presented responsibly.

 Your



  continued membership signifies that you agree to this



  disclaimer and pledge to abide by our Rules and

 Guidelines.







  ---







  You received this message because you are subscribed
to

 the



  Google Groups "Wanabidii" group.







  To unsubscribe from this group and stop receiving

 emails



  from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@

 googlegroups.com.







  For more options, visit https://groups.google.com/d/

 optout.











 --



 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com







 Kujiondoa Tuma Email kwenda



 wanabidii+unsubscribe@

 googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha

 ukishatuma







 Disclaimer:



 Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility

 for any legal consequences of his or her postings, and
hence

 statements and facts must be presented responsibly.
Your

 continued membership signifies that you agree to this

 disclaimer and pledge to abide by our Rules and

 Guidelines.



 ---



 You received this message because you are subscribed to
the

 Google Groups "Wanabidii" group.



 To unsubscribe from this group and stop receiving
emails

 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@

 googlegroups.com.



 For more options, visit https://groups.google.com/d/

 optout.













 --



 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com



  



 Kujiondoa Tuma Email kwenda



 wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com  Utapata Email ya

 kudhibitisha ukishatuma



  



 Disclaimer:



 Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility

 for any legal consequences of his or her postings, and
hence

 statements and facts must be presented responsibly.
Your

 continued membership signifies that you agree to this

 disclaimer and pledge to abide by our Rules and

 Guidelines.



 ---



 You received this message because you are subscribed to
the

 Google Groups "Wanabidii" group.



 To unsubscribe from this group and stop receiving
emails

 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.



 For more options, visit https://groups.google.com/d/
optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com



Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma



Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/
optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment