Sunday 25 September 2016

[wanabidii] Raha ya mapinduzi ufanikiwe nini Hatima ya Mtatiro,Seif na wengine!

Mara zote msajili wa vyama vya siasa ndiye amekuwa muamuzi wa kukubali ama kubatilisha mapinduzi ya uongozi ndani ya vyama vya siasa.

Kwa historia tokea vyama vingi vianze kama sikosei ofisi ya msajili imeongozwa na majaji wa tatu;Wa kwanza marehemu Jaji Liundi,pili Jaji John Tendwa na sasa Jaji Mutungi.Kwa historia kidogo ofisi ya msajili imeshawahi kubariki kupinduliwa/kuondolewa wafuatao;

1.Augustine Mrema aliwashinda akina Marando,Lissu,Baregu na wengine ndani ya NCCR Mageuzi...hivyo ikawapasa kutafuta mlango wa kutokea baada ya mbinu zao kushindwa.

2.Mrema tena akiwa TLP aliwapindua waliotaka kumuondoa kwenye uenyekiti.

3.Mapalala alipinduliwa na akina Maalim Seif Cuf na ofisi ya msajili ikabariki.

4.Hamad Rashid aligongwa nyundo CUF na kuvuliwa umakamu mwenyekiti na uanachama.

5.Mbatia naye kabakizwa ofisini na uenyekiti Taifa NCCR Mageuzi na msajili dhidi ya mapinduzi yaliyoshindwa chini ya wasaidizi wake.

6.Kwa sasa Lipumba kashinda rufaa kwa msajili dhidi ya CUF.Kinachofurahisha ni kuwa wafuasi wengi wa CUF bara wamekuwa wakimuunga mkono dhidi ya Seif.

Raha ya mapinduzi ni ushindi....siioni nafasi ya Mtatiro kwa sasa ndani ya CUF na kuna siku nilionya kuwa anatumika kama "taulo",hasa ukizingatia hana wafuasi wanaomuunga mkono bara.Maalim Seif na wenzake zanzibar wanakazi kubwa kwani bosi wao sasa karudi na kimsingi Lipumba sasa atakuwa mwenyekiti haswa Natalie's chini ya Seif...atataka Seif amtii hapa patam ngoja tuweke akiba ya maneno

0 comments:

Post a Comment