Thursday 29 September 2016

Re: [wanabidii] WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINAADAM NIELIMISHENI

1.Kwa maoni yangu, haki za binadamu ni kanuni za msingi za maisha zinazopaswa zilindwe na mamlaka ya nchi ili raia waishi maisha ya heri (kanuni zinazolinda ustawi wa raia na mali zao).
2. Kanuni hizi za msingi ni kama vile: kuishi, kuheshimiwa, kupata riziki halali ya maisha, kutekeleza majukumu ya kifamilia, kijamii, kupata elimu, huduma za afya, maendeleo nk.
3. Jambazi kumwua polisi au raia au mume kumpiga mkewe au mtoto ni mambo ambayo yako nje ya haki za binadamu, lakini yako ndani ya makosa ya jinai kwa mujibu wa sheria za nchi. Ila polisi au mtu yeyote mwenye mamlaka ya kiserikali akimwua raia (kama si katika kujilinda au katika kutekeleza wajibu wake kisheria na unaoendana na kanuni za kimataifa zinazolinda ustawi wa watu) basi hata hapo haki za binadamu zimeguswa.
4. Kimsingi, haki za binadamu ni madai halali dhidi ya mamlaka ya nchi - yaani yale ambayo mamlaka ya nchi inapaswa iyatekeleze kwa raia wake.
5. Mamlaka ya nchi ikitekeleza inakuwa kwamba nchi fulani inaheshimu haki za binadamu na ikishindwa/kukiuka au kupuuza inakuwa kwamba nchi fulani inavunja haki za binadamu.
 

2016-09-29 14:11 GMT+03:00 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Loh swali zuri sana. Na mimi ni mmoja kati ya watakaofaidika japo nilikuwa naona aibu kuuliza.
Zamani sana katika mjadala mwanasheria mmoja alibwatuka neno ovu kabisa Akaseka " LENGO KUU LA HAKI ZA BINADAMU NI KUMTENGANISHA MWANADAMU NA MUNGU" Kabla hajaongeza nikamvaa. Nikamshambulia.Akaniangalia kwa dharau. Mwisho wa maneno yangu akasema "Wewe ndugu naona una akili. Subiri wakati ukifika tumia akili zako kuelewa." Nikamuuliza wakati gani? Akasema pale itakapotangazwa kuwa NGONO NI HAKI ZA BINADAMU. Nikamwambia mpaka kurudi kwa Yesu hakutatokea kitu hicho. Ilipotokea namtafuta sana kuntaka radhi.

Jingine: Huwezi kuwasikia wanaharakati majambazi wanapomuua Polisi. Hawathibutu kusema. Lakini Polisi akithubutu tu hutajua walikotokea.

Jingine: Kuna mataifa ndiyo tu yanayoweza kutoa tafsiri ya gaidi. Angola ilipambana na gaidi Savimbi lakini usingesikia akiitwa gaidi labda Nyerere tu. Ghadafi aliitwa gaidi na mataifa hayo kila mwanaharakati akamwita gaidi. Kuna mmoja nilimuuliza kwanini unamwita Gadafi gaidi akaniuliza kama juzi nilisikiliza VoA. Yaani kwake ni gaidi kwa sababu VoA ilimwita gaidi. Sasa hivi Urusi inaisaidia Syria kupambana na magaidi lakini husikii wanaharakati wakisema. Ila Asaad ndiye anaitwa muuaji. Ukiuliza watasema Husikii VoA nini? Atakayejibu atusaidie mpaka huko.
Muhingo

--------------------------------------------
On Wed, 9/28/16, 'Mashaka Makana' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

 Subject: [wanabidii] WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINAADAM NIELIMISHENI
 To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
 Date: Wednesday, September 28, 2016, 3:35 PM

 Habari
 wote katika jamii! Naomba kufahamu MSINGI wa kuanzisha
 shirika la kutetea haki za binaadamu! Mwezi huu wenzetu wa
 Kagera walipatwa na madhara ya kuumia na wengine kufariki.
 Nini mchango wa wanaharakati wa haki za binaadamu kwa
 majanga ya aina hii? Au kwa uhalisia wanaharakati wa haki za
 binaadamu mmefanya nini kwa tukio hilo? Mbona hamsikiki kama
 ilivyo katika matukio mengine mfano police wakitumia nguvu
 zaidi kudhibiti mfano waandamaji- mara moja utaona au
 kusikia mikutano na waandishi wa habari kutoa matamko ya
 kulaani na nk. 
 Kwali lingine naomba kuelimishwa, mtu aliekufa ana
 haki gani kama kifo chake kilitokana na kupigwa au kunyongwa
 au kupigwa risasi na wahalifu? Hapo je, wanaharakati hakuna
 kazi ya kufanya? Hili swali linawahusu pia wale wanaopinga
 adhabu ya kifo. Mfano mdogo tu, janga la tetemeko limeua
 watu Kagera na wengine wengi wanalala nje na wengine
 darasani na watoto wanasoma na wahanga wakiendelea kuishi
 darasanina wengine kuhitaji matibabu na makazi halafu
 unasikia au kushuhudia mtu au kikundi cha watu wanahujumu
 michango hiyo ya wahanga! Je huyu si muuaji? kwa nini
 asiuawe au wasiuawe hawa?
 Naomba kuelimishwa!



 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment