Tuesday 27 September 2016

Re: [wanabidii] Hoja 11 zamrejesha Prof. Lipumba CUF

Sio Emma. Msajili hakuamua.. Amesema kilichopo.
Walimpelekea malalamiko. (waliompelekea walitaka awasaidie kutafsiri kinachowashinda) Akaamua kuwasikiliza waye nza akawatangazia kwa mujibu wa malalamiko hyao na kwsa kuzingatia katiba na myongozo waliyojiwekea basi Lipumba ni mwenyekit. Ni kama kumu liza kuwa leo ni siku gani> Akikujibu ni Jumanne hawi yeye kaifanya jumanne bali ndiyo
--------------------------------------------
On Sun, 9/25/16, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Hoja 11 zamrejesha Prof. Lipumba CUF
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, September 25, 2016, 8:35 PM

Suali
linalouliza ni lini msajili wa vyama akawa na mamlaka
kuamulia vyama vya siasa mambo yao ya
ndani?em
2016-09-25 9:34 GMT-04:00
'Lesian' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Mamluki
wa ccm na kwa kua anatumiwa lazima watafute namna ya
kuhakikisha anakuja kuharibu ukawa
Bytheway...mgogoro huu una lengo la kuharibu
ukawa na haswa Chadema lakini kwa navyofaham chadema
wanalijua hilo, kwa kua mzee seif nae kashindwa na huyu ma
luki wake, sasa bora watimke ukawa, na wale watu wanaoamini
ktk mabadi.iko walioko Cuf warud chadema CUF bora iishie
hapo Chadema in uwezo wa kusonga mbele yenyewe bila hawa
mamluki
Wanaofurahia ni ccm kwamba
wameshinda lakini ukitizama kwa jicho la ndani utaona
tu.....lipumba na pumba zake anavyotumika kuua jitihada za
upinzani nchini......aluta continuaaaaa

'mpombe mtalika' via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:

HOJA 11 zilizotolewa na
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji
Francis Mutungi, zimetosha kumrejesha katika wadhifa wake,
Mwenyekiti
'aliyejiuzulu' wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa
Ibrahim Lipumba.

Mbali ya Lipumba viongozi wengine ambao msimamo wa
Msajili
unawarejesha madarakani moja kwa moja baada ya kusimamishwa
na Baraza
Kuu la Uongozi la CUF, katika kikao chake cha Agosti 30,
mwaka huu
kilichofanyika jijini Dar es Salaam ni Naibu Katibu Mkuu
Bara Magdalena
Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua na Naibu Mkurugenzi wa
Habari
Taifa, Abdul Kambaya.
Wengine ni Mbunge wa Mtwara, Maftaha Nachuma, wajumbe
wa Baraza Kuu
Taifa, Masudi Omari Mhina, Thomas Malima, Ashura Mustafa na
Kapasha
Kapasha. Pia Musa Haji Kombo, Habibu Mnyaa na Haroub Shamis
ambao
wataendelea kuhesabika kama wanachama halali wa chama
hicho.
Katika barua yake kwa viongozi wa CUF, Msajili alieleza
kuwa amefikia
msimamo wake huo baada ya kupata nafasi ya kusikiliza pande
zote
zinazosigana katika mgogoro huo wa uongozi ndani ya chama
hicho.
Alisema katika kufikia maamuzi hayo amezingatia Mamlaka
na wajibu wa
Msajili kushughulikia mgogoro huo, Kujiuzulu kwa Profesa
Lipumba,
Profesa Lipumba kutengua barua yake ya kujiuzulu, Uhalali wa
Mkutano
Mkuu Maalumu wa CUF wa Agosti 21, mwaka huu na baadhi ya
wajumbe wa
Mkutano Mkuu Maalumu kuhitaji Profesa Lipumba aitwe katika
chumba cha
mkutano kujieleza.
Nyingine ni uhalali wa kura zilizopigwa kukubali au
kukataa Profesa
Lipumba kujiuzulu, uhalali wa kikao cha Baraza Kuu la
Uongozi la Taifa
la Agosti 28, mwaka huu, utaratibu wa kuchukua hatua za
kinidhamu,
uhalali wa kamati iliyoundwa na Baraza Kuu la Uongozi la
Agosti 28 ili
kufanya kazi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Taifa na
mwisho ni
kuhusu uhalali wa uteuzi wa viongozi wa kitaifa uliofanywa
na kikao cha
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa cha Agosti 28, mwaka
huu.
Kutokana na hoja hizo, Jaji Mutungi katika taarifa yake
kwa vyombo
vya habari jana alisema: "Hivyo, baada ya upembuzi kama
nilivyobainisha
hapo juu, msimamo na mwongozo wangu ni kwamba Profesa
Ibrahim Lipumba
bado ni Mwenyekiti halali wa Taifa wa CUF na walalamikaji
wanachama
waliosimamishwa na waliofukuzwa uanachama wote bado ni
wanachama halali
wa CUF.
"Aidha viongozi ambao uongozi wao uliathirika na
maamuzi yasiyo
halali ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa cha
Agosti 28, mwaka
huu, bado ni viongozi halali. Natumia fursa hii kuwapa
angalizo kwamba,
kwa kuwa kamati iliyoundwa kuongoza chama na viongozi
walioteuliwa na
kikao hicho si halali na kwa kifungu cha 88 (2) cha Sheria
ya Vyama vya
Siasa Sura ya 258, hawaruhusiwi kufanya shughuli yoyote ya
chama."
Msajili kushughulikia mgogoro
Msajili akifafanua hilo alisema kwa kifungu cha 10 (f)
cha Sheria ya
Vyama vya Siasa Sura ya 258 kinahitaji chama cha siasa
kuwasilisha
orodha ya viongozi wake wa kitaifa kwa Msajili wa Vyama vya
Siasa na kwa
kuwa Kifungu 8A (1) kinampa mamlaka Msajili kuhifadhi
taarifa za
viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa na kwa kuwa Kanuni ya
5 (1) ya
Kanuni za Usajili wa Vyama vya Siasa toleo namba 111 la
mwaka 1992
inakitaka kila chama kuwasilisha taarifa kwa Msajili
panapotokea
mabadiliko ya uongozi wa kitaifa wa chama husika.
"Hivyo kwa mustakabali wa majukumu yanayotolewa na
vifungu hivyo,
Msajili wa Vyama vya Siasa anao wajibu wa kuhakikisha
taarifa za
mabadiliko ya uongozi anazoletewa na chama cha siasa ni
sahihi, kwa
maana ya kujiridhisha kuwa mabadiliko hayo ya uongozi
yamefanyika na
mamlaka halali ya chama na pia yametekelezwa kwa mujibu wa
Katiba na
Kanuni za chama husika. "Kwa mantiki hiyo basi na
nikijielekeza kwenye
vifungu vya sheria nilivyoainisha, ni dhahiri kwamba Msajili
wa Vyama
vya Siasa anayo mamlaka na wajibu wa kisheria, kuchunguza na

kujiridhisha kuhusu usahihi wa mabadiliko katika uongozi wa
kitaifa wa
chama yaliyofanyika na masuala yote yanayohusiana na
mabadiliko hayo,"
alisema Msajili.
Kujiuzulu kwa Profesa
Lipumba Kuhusu hilo Msajili alisema kwa mujibu wa Ibara
ya 117 (2),
kiongozi wa Chama cha CUF, hata kama mhusika amebainisha
tarehe ya
kujiuzulu katika barua yake ya kujiuzulu, atahesabika kuwa
amejiuzulu
baada tu ya mamlaka iliyomchagua au kumteua kukubali.
Alisema kwa mujibu wa Ibara hiyo, ni sahihi kusema
kwamba Profesa
Lipumba alikuwa bado ni Mwenyekiti halali wa Taifa wa CUF
hata wakati wa
kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Agosti 21, hivyo hata yeye
kujiita
Mwenyekiti wa Taifa mstaafu kabla ya kujiuzulu kwake
kukubaliwa na
mamlaka husika si sahihi.
Kutengua barua yake ya kujiuzulu
Akizungumzia hilo Msajili alisema, "Katiba ya CUF iko
kimya kuhusu
hilo, hivyo hapakuwa na kizuizi kwa Profesa Lipumba kutengua
barua yake
ya kujizulu kwa kuzingatia ukimya huo kwa upande wa uongozi
wa CUF
kuchukua hatua pindi walipopokea barua yake ya kujiuzulu na
hivyo kutoa
mwanya kwa mhusika kuitengua barua yake ya kujiuzulu.
"Si hivyo tu, bali pia barua yake ya kutengua
kujiuzulu haikukataliwa
na uongozi wa CUF.Alichoelezwa Profesa Lipumba ni kwamba
asianze kazi
tarehe aliyopanga kuanza kazi ili asubiri kwanza Katibu Mkuu
ashauriane
na wanasheria wa chama, ambapo mpaka suala hili
linawasilishwa mbele
yangu, Profesa Lipumba alikuwa bado hajapewa mwongozo wowote
kuhusiana
na barua yake ya kutengua kujiuzulu," alisema
Msajili.
Uhalali wa hoja
Msajili akitoa msimamo wake kuhusu hoja ya uhalali wa
Mkutano Mkuu wa
Agosti 21, alisema pamoja na malumbano kuhusu akidi ya
wajumbe lakini
kwa vyovyote vile mkutano huo ulikidhi matakwa ya Ibara ya
114 inayosema
kuwa ili akidi kutimia idadi ya wajumbe waliohudhuria kikao
inapaswa
kuzidi nusu ya wajumbe wote, na hivyo idadi ya wajumbe 700
ilikidhi
matakwa ya Katiba.
Kuhusu hoja ya baadhi ya wajumbe kuhitaji Profesa
Lipumba aitwe
katika chumba cha mkutano kujieleza, Msajili alisema hata
kama Profesa
Lipumba angekuwa si mjumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu ili mradi
uwepo wake
yalikuwa ni matakwa ya wajumbe wa mkutano huo, basi alipaswa
kupewa
fursa katika mkutano huo kuthibitisha kuwa, barua iliyosomwa
na Katibu
Mkuu kuhusu kujiuzulu kwake ni yake na kueleza sababu za
kujiuzulu na
hivyo kumkatalia ilikuwa ni kukiuka Ibara ya 116 ya Katiba
ya chama
hicho.
Kwa hoja za uhalali wa kura zilizopigwa kukubali au
kukataa Profesa
Lipumba kujiuzulu, Msajili alisema zoezi la kupiga kura za
kukubali au
kukataa kujiuzulu kwa Profesa Lipumba lilifanyika katika
mazingira ya
vurugu na hivyo kufanya zoezi hilo kukosa uhalali na kutoa
mfano kuwa
zoezi la kujua idadi ya wapiga kura kabla ya kupiga kura
halikufanyika,
ukizingatia kuwa baada ya vurugu kuzuka, kuna wajumbe
walitoka nje ya
ukumbi kuogopa vurugu na watu wasio wajumbe kuingia ndani ya
ukumbi.
Kuhusu uhalali wa uteuzi wa viongozi wa kitaifa
uliofanywa na kikao
cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa cha Agosti 28, Msajili
alisema kwa
mujibu wa Ibara ya 115 (1) iwapo nafasi ya kiongozi yeyote
ipo wazi,
basi mamlaka yake ya uteuzi itamteua mtu wa kukaimu nafasi
hiyo.
"Kwa mujibu wa Ibara ya 91 (1) (m) mamlaka ya uteuzi
wa Naibu Katibu
Mkuu ni Baraza Kuu la Taifa, hivyo laiti uamuzi wa kikao cha
Baraza Kuu
la Uongozi Taifa cha Agosti 28 ungekuwa si batili, basi
uteuzi wa Joran
Bashange kuwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu ungekuwa sahihi, kwa
maana ya
kwamba Baraza Kuu la Uongozi lina mamlaka hayo.
"Hata hivyo kwa upande mwingine, uteuzi wa Mbaraka
Maharagande kuwa
Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa
Umma una
dosari nao si sahihi kwa sababu kwa mujibu wa Ibara ya 91
(1) (f)
mamlaka yake ya uteuzi ni Mwenyekiti wa Taifa na si Baraza
Kuu la
Taifa," alisema Msajili na kusema adhabu kwa mtu
anayefanya shughuli za
chama bila kufuata taratibu ni kifungo cha miezi sita, faini
isiyozidi
Sh milioni moja au vyote kwa pamoja.
Lipumba atinga ofisini kwa mdundiko
Katika tukio lingine mchana jana Profesa Lipumba
alifika katika ofisi
za chama hicho zilizopo Buguruni jijini Dar es Salaam huku
akiandamana
na umati wa wafuasi wa chama hicho huku wakisindikizwa na
ngoma maarufu
katika ukanda wa Pwani ya Mdundiko.
Wafuasi wa Profesa
Lipumba walianza kukusanyika katika ofisi hizo kuanzia
asubuhi baada
ya kupata taarifa za kuwepo kwa barua kutoka kwa Msajili wa
Vyama vya
Siasa, ikimtambua mwanasiasa huyo kama Mwenyekiti halali wa
chama hicho
kwa mujibu wa Katiba ya chama.
Ilipotimu saa saba mchana Profesa Lipumba alifika
katika eneo zilipo
ofisi hizo akiwa na kundi la wafuasi wake waliokuwa
wakicheza kwa ustadi
ngoma ya mdundiko, lakini walikumbana na kizuizi cha
kuingia ndani
kutokana na geti kuu kuwa limefungwa.
Zuio hilo lilidumu kwa muda usiozidi dakika nne, ambapo
baadaye
baadhi ya wafuasi wa kiongozi huyo waliamua kuruka ukuta ili
kuingia
ndani kumfungulia geti kumwezesha kuingia ndani.
Wakati matukio hayo yakiendelea, polisi waliokuwa
wamefika mapema ili
kudhibiti usalama katika eneo hilo walikuwa wakishuhudia
wakiwa ndani
ya magari matatu yaliyokuwa yamesimama kando ya geti,
wakiwatazama
wafuasi hao wakitumia nguvu ili kuingia ndani ya ofisi
hizo.
Hata hivyo haikuwa kazi rahisi kuingia ndani ya ofisi
hizo kwani
wakati wakiendelea kuruka ukuta, zilisikika risasi zikipigwa
na askari
wa kampuni binafsi ya ulinzi aliyekuwa analinda ofisi hizo,
lakini
alidhibitiwa baadaye na wafuasi hao ambao walimnyang'anya
silaha na
kuikabidhi kwa polisi.
Baadaye wafuasi hao walianza kumpa kichapo askari huyo
wa ulinzi
kabla ya wazee wa chama hicho kujitokeza na kumuokoa na
kulazimika
kumfungia katika choo kimojawapo cha ofisi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kuingia ofisini
kwake, Profesa Lipumba alisema kurejea kwake kunatokana na
uamuzi
uliotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, huku akieleza
hatua mbalimbali
alizochukua tangu alipoandika barua ya kujiuzulu, barua ya
kutengua
uamuzi wake na yaliyotokea katika vikao mbalimbali vya chama
hicho,
ambazo kimsingi zinamfanya kuwa na sifa ya kuendelea kuwa
Mwenyekiti
halali kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho.




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/
optout.






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment