Wednesday 28 September 2016

Re: [wanabidii] WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINAADAM NIELIMISHENI

1. Haki za binadamu zinahusiana na serikali au vyombo vyake kukiuka haki za msingi za raia (mfano, kama askari watapiga raia, serikali kushindwa kupeleka maendeleo kwa wananchi au kutumia vibaya madaraka).
2. Tetemeko la ardhi au maafa yanayotokana na nguvu za kiasili hazihusiani na kuvunjwa kwa haki za binadamu. Ila inaweza likawa tatizo la haki za binadamu, kama misaada inayopelekwa kwa walioathirika haiwafikii na hivyo kupelekea waathirika kuendelea kuteseka na hata kupata magonjwa kutokana na kutotibu majeraha yao na hatimaye kufariki dunia. Pia linaweza likawa tatizo la haki za binadamu kama serikali imeshindwa kuchukua hatua wakati ina jukumu la kufanya hivyo.
3. Mashirika mengi yanayotetea haki za binadamu huwa kwanza yanatoa msaada kwa waathirika (kama tatizo lenyewe liko ndani ya uwezo wao) na kufanya tathmini ya kilichotokea na kisha kutoa taarifa kama kulikuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu au la.
4. Hivi ndivyo ninavyoweza kuchangia kwa sasa.

2016-09-28 15:35 GMT+03:00 'Mashaka Makana' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Habari wote katika jamii! Naomba kufahamu MSINGI wa kuanzisha shirika la kutetea haki za binaadamu! Mwezi huu wenzetu wa Kagera walipatwa na madhara ya kuumia na wengine kufariki. Nini mchango wa wanaharakati wa haki za binaadamu kwa majanga ya aina hii? Au kwa uhalisia wanaharakati wa haki za binaadamu mmefanya nini kwa tukio hilo? Mbona hamsikiki kama ilivyo katika matukio mengine mfano police wakitumia nguvu zaidi kudhibiti mfano waandamaji- mara moja utaona au kusikia mikutano na waandishi wa habari kutoa matamko ya kulaani na nk. 

Kwali lingine naomba kuelimishwa, mtu aliekufa ana haki gani kama kifo chake kilitokana na kupigwa au kunyongwa au kupigwa risasi na wahalifu? Hapo je, wanaharakati hakuna kazi ya kufanya? Hili swali linawahusu pia wale wanaopinga adhabu ya kifo. Mfano mdogo tu, janga la tetemeko limeua watu Kagera na wengine wengi wanalala nje na wengine darasani na watoto wanasoma na wahanga wakiendelea kuishi darasanina wengine kuhitaji matibabu na makazi halafu unasikia au kushuhudia mtu au kikundi cha watu wanahujumu michango hiyo ya wahanga! Je huyu si muuaji? kwa nini asiuawe au wasiuawe hawa?

Naomba kuelimishwa!

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment