Friday, 2 September 2016

Re: [wanabidii] CHADEMA MMECHAFUKA,MJISAFISHE

Alisema anavyo vingi



Wale wale


On Sep 2, 2016 9:58 AM, "'Lutgard Kokulinda Kagaruki' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Hivi Magu bado anatoa vyeo siyo? Huwezi kuhangaika hivi kama si kutafuta ulaji!

LKK

Sent from my iPad

On 1 Sep 2016, at 5:35 PM, 'misangocharles' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Siku nyingi sana nilijiuliza hivi busara za dada yangu mpendwa Katabazi zilipatwa mushkeri wapi. Leo ndo nimejua! Pole

Sent from my Huawei Mobile

'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


CHADEMA MMECHAFUKA,MJISAFISHE 

Na Happiness Katabazi 

 AGOSTI  31 mwaka huu, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) kilitangaza  kuhairisha  mikutano,maandamano  yake yasiyo na kikomo waliyokuwa wamepanga yaanze Leo  nchi nzima ambapo maandamano hayo yalipewa jina la Operesheni UKUTA  kwamba wanadai Demokrasia kwasababu kuna viashiria Vya Udikteka Katika serikali inayoongozwa na Dk.John Magufuli.

Uamuzi huo ambao umekuja umechelewa umetangazwa  na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe Katika mkutano wake na waandishi wa Habari uliofanyika Katika Ofisi za Makao makuu ya Chama hicho Dar es Salaam.

Mbowe akitaja baadhi ya sababu za kuahirisha maandamano hayo haramu kisheria na ambayo yalishapingwa na Makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo baadhi ya viongozi wa dini  ,serikali kupitia Jeshi la Polisi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali lakini bado Chadema hadi kufikia Agosti 30 Mwaka huu, wakiendelea kushikilia msimamo wao Kuwa maandamano ya UKUTA yapo pale pale Leo Septemba Mosi Mwaka huu alisema ,Sababu Moja wako ni kwamba eti viongozi wa kidini wamewasii  sana wasitishe Operesheni UKUTA waliyopanga kuifanya Leo.

Itakumbukwa kuwa Agosti 24 Mwaka huu, niliisambaza makala yangu Katika mitandao ya kijamii iliyokuwa na kichwa cha Habari kisemacho ; " UKUTA WA CHADEMA NI BATILI  KISHERIA ".

Ndani ya makala hiyo nilieleza wazi wazi Kuwa oparesheni UKUTA ni haramu kisheria na Kwa Mungu vile vile kwasababu   Mwenyezi Mungu Katika Kitabu cha Warumi 13:1-2 kinasomeka kama ifuatavyo : "  Kila  mtu na atii mamlaka iliyo Kuu; Kwa maana Hakuna mamlaka isiyotoka  Kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo a wasiyo mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu ; nao washinda nao watajipatia hukumu" . 

Wakati Kifungu cha 43(4) Cha Sheria ya Polisi na wasaidizi wake  ya Mwaka 2002 inatoa mamlaka wa kwa Polisi Kuzuia mikusanyiko pindi inapokuwa na sababu za Msingi za kufanya hivyo.

Na Kifungu cha 43(6) Cha Sheria ya Polisi na Wasaidizi wake, kinatoa Haki ya kukata rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani kwa mtu Anayepinga mamlaka hayo ya Jeshi la Polisi yaliyopo Katika Kifungu cha 43(4) cha Sheria hiyo.

Hadi Leo hii Chadema au vyama vingine Vya siasa vilivyokatia rufaa amri hiyo ya Jeshi la Polisi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani hivyo amri hiyo ya Jeshi la Polisi ni halali na itaendelea kuwepo kwasababu amri hiyo ya Jeshi la Polisi haijatenguliwa na Mahakama wala Waziri wa Mambo ya Ndani.

Sote ni mashahidi kwa zaidi ya Mara Tatu Jeshi la Polisi limekuwa likitoa matangazo kwa umma ya Kuzuia mikutano na maandamano kwa vyama Vya siasa kwa Sababu Kuwa Haki ya Usalama siyo rafiki.

Lakini viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mbowe, Wakili wao Tundu Lissu na viongozi wengine wa Chadema na wafuasi wao walikuwa wakipingana waziwazi na amri hiyo ya Jeshi la Polisi na wengine kufikia Hatua Kulipaka matope Jeshi la Polisi Kuwa linatumika kugandamiza Chadema na kwamba polisi hawana mamlaka ya Kuzuia mikutano .

Ujinga huo wa kuaminisha wafuasi wa Chadema Kuwa Polisi hawana mamlaka ya Kuzuia mikusanyiko ,maandamano ulikuwa ukifanywa na Mwanasheria ninayemheshimu sana Tundu Lissu na kwamba bahati Mbaya baadhi ya watu walimuamini Lissu na wakajikuta nao wakiamini Polisi hawana mamlaka ya Kuzuia mikutano Kumbe sikweli na wengine kupitia ile makala yangu baada ya kuisoma na kuwaonyesha Kifungu kinachowapa polisi mamlaka ya Kuzuia mikutano walifumbuka akili na wakampuuza Lissu .

Napongeza uamuzi wa Chadema wa kuairisha kufanya ile Operesheni Yao haramu ya UKUTA kwasababu endapo wangefanya wangejikuta wamepata matatizo ya kuangukia Katika mikono ya dola bila Sababu za Msingi.

Lakini uamuzi huo  wa jana wa Chadema umekuja ukiwa umechelewa na umeleta madhara kwa baadhi ya watu wakiwemo wafuasi wao kwa Kukamatwa, kulala mahabusu ,magerezani ,kufunguliwa Kesi, kufanya baadhi ya wananchi waishi kwa Hali ya wasiwasi Kuwa hiyo Septemba Mosi Chadema wangeandamana yangetoa madhara gani.

Pia umwamba ule wa kijinga uliokuwa ukifanywa na Mbowe na viongozi wenzake wa kuamasisha wafuasi wao washiriki maandamano hayo haramu waliyopanga yafanyike Leo pia umekichafua Chama hicho Mbele ya wapenda Amani na wazalendo wa kweli wa taifa hili na sasa wanakiona Chama hicho kina viongozi ambao Si watu wa kawaida ambao ka zaidi ya Miezi miwili sasa wamekuwa wakiwaamasisha wafuasi wao wa kaahidi amri ya Jeshi la Polisi , kauli ya Rais Dk.John Maguli iliyozuia maandamano na mikutano na ikawa inawaamasiha wafuasi Hao na wapenda demokrasia wajitokeze Leo waandamane bila kikomo nchi nzima.

Hivi sasa Chadema kimejidhiirisha kina baadhi ya viongozi ambao hawapendi kutii mamlaka licha Biblia ,Sheria na Katiba za nchi zinawataka wafanye hivyo. Kwasababu kama kweli Chadema kinaheshimu mamlaka, Sheria hata Jana Mbowe alivyotangaza kuahirisha Operesheni UKUTA asingethubutu Kusema Kuwa wamearishisha zoezi Hilo na watalifanya baada ya mwezi mmoja.Huu ni uhuni.

Kiongozi wangu wa Kanisa la Elshadai Temple la Bokobasiya, Nabii Kanali Mstaafu Bruno Kinunda hajashiriki kuwafuata kuongea nanyie ,Nabii Kinunda Jumapili iliyopita alilitaka Kanisa tuombe hili maandamano hayo Mungu atumie njia zake ayasambaratishe na ndivyo yaliyokuwa Mungu ameyasambaratisha tena kwa kutumia vinywa vyenu Nyie wenyewe wakina Mbowe na wenzako ambao mlikuwa mstari wa Mbele kuhamasisha maandamano hayo yafanyike ambayo endapo yangefanyika yangetuletea Mashaka makubwa.

Kwa tunaomwamini Mungu na tunaofahamu dola linafanyaje Kazi ni wazi ya Maombi yakuliombea taifa hili Amani na mshikamano yanayoombwa na watumishi wa Mungu na wananchi mbalimbali Mungu ameyasikia kwa Mungu huyo huyo kaamua kuwatumia nyie nyie wahamasishaji wa wananchi wasiitii amri za mamlaka muende mbele ya um ma huku mkimulikwa na Televisheni mkatangaza kuhairisha maandamano hayo ambayo yalishalaaniwa na makundi mbalimbali nchini.

Bila Shaka Nyie viongozi wa Chadema mliokuwa mnashupalia kufanyika Operesheni UKUTA mlikuwa mmeishavamiwa na mapepo ndani yenu yaliyokuwa ya nawatuma,   muwaamasishe wananchi wasitii mamlaka ,waandamane bila kikomo na kwa Tafsiri nyepesi hayo maandamano yasiyonakikomo ni wafanye vurugu watu wamwage Damu lakini mmeshindwa kwa jina Yesu na pia vyombo Vya Ulinzi na Usalama vipo imara na vimewabana mbavu kisheria.

Kwanza Mbowe,Lowassa,Lissu na viongozi wengine wa Chadema hamfahi kupewa madaraka makubwa ya nchi hii mbele ya safari kwasababu Nyie wote ni wakristo na kutwa mnajifanya mnamwamini Mungu .

Busara ya Edward Lowassa ambaye aliwahi Kuwa Ofisa wa JWTZ na waziri Katika Wizara mbalimbali na hatimaye waziri Mkuu hadi alipoji udhuru   Kwasababu  ya kashfa ya Mkataba  wa Richmond  mwaka 2008 , Fredrick Sumaye ambaye naye alikuwa Waziri  Mkuu tena kwa Miaka 10 kushindwa kutambua Kuwa Septemba Mosi ni siku ya Majeshi iko wapi hadi wakaendelea kuhamasisha wafuasi wao  wajitokeze Septemba Mosi ambayo ni siku ya majeshi kwaajili ya kushiriki maandamano haramu ya UKUTA yasiyo na kikomo?

Nawauliza kwanini Kabla ya kufikiria kuanzisha hiyo Operesheni UKUTA hamkushirikisha Mungu na Hao viongozi wa dini waiombee hiyo Operesheni yenu ili ije ikubali we na serikali umma?

Si nanyie Chadema mnamsemo wenu maarufu  Mnaosema; Mnaanza na Mungu na Mtamaliza na Mungu?"  .  Ilikuwaje zoezi la UKUTA Kabla ya kulitangaza hamkulikabidhi Kwa Mungu na Hao sijui viongozi wenu wa kidini mlificha  Majina Yao?

Sidhani kama Operesheni UKUTA mwanzo kabisa mngeikabidhi mikononi mwa Huyo Mungu wenu  mnayedai mnamuomba maana Miungu sikuhizi ni Mingi sana ,asingeingwa kiasi hiki kila kosa na serikali bila Shaka UKUTA mlimkabidhi Mungu wa Kuzimu ndiyo maana ameshindwa kufurukuta Mbele ya Nguvu za Mungu wa Elshadai.


Mbowe Kasema wamekutana Mara Kadhaa na viongozi wa kidini na kufanya mazungumzo na amuwezi kukaidi ushauri wa viongozi wenu wa kiroho ,sawa kama kweli Hamuwezi kukaidi ushauri wao kwanini Mlivyokuwa mkienda Kwenye mazungumzo na viongozi wa dini kwanini mlipokuwa mkitoka Katika hivyo vikao mnarudi huku mitaani Mnasema UKUTA Huko pale pale?

Mbowe Kasema viongozi wa dini wanaenda kuzungumza na Rais Magufuli Kisha watawarejeshea majibu Chadema waliyoyapata kwa rais. Wakati huo huo Mbowe anasema Oktoba Mosi UKUTA  utafanyika .

Tumuulize Mbowe ,hivi anafahamu Kuwa ndani ya muda gani hayo mazungumzo kama yatamalizika baina ya viongozi wa dini na rais Magufuli?Ina maana Tayari rais Magufuli amesishawapatia Hao viongozi wa dini tarehe ya kukutana na hao viongozi wa dini na kwamba Tayari ameishajua Kabla ya Oktoba Mosi Mwaka utakuwa umeishapatikana? 

Rais Magufuli Atakuwa ni Mjinga wa aina gani ambaye atakubali kuingia Kwenye mazungumzo wakati Tayari Mwenyekiti wa Chadema Mbowe Ana Dhamira ya kuendelea zoezi la UKUTA ,Oktoba Mosi Mwaka huu na sio mazungumzo?

Agosti 29 Mwaka huu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju alisema UKUTA ni batiri kisheria na msimamo wa serikali ni kwamba serikali  haiitaji mazungumzo wala majadiliano na viongozi wa dini kuhusu   suala la UKUTA.

Masaju alisema Kwasababu  suala la UKUTA siyo la mazungumzo Bali  linaitaji wananchi  na watii Sheria za nchi na kwamba Hao viongozi wa dini walioshauri serikali Ifanye mazungumzo na Chadema ,viongozi Hao warudi Kwenye nyumba zao za ibada wawasisitize waumini wao watii mamlaka kama Warumi 13:1-2 ninavyowataka watii mamlaka na watii Sheria za nchi .

Ibara ya 59(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inasema  hivi ;   "  Mwanasheria Mkuu atakuwa ndiye mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na, kwa ajili hiyo, atawajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria zitakazopelekwa kwake au atakazoagizwa na Rais kuzitekeleza, na pia kutekeleza kazi au shughuli nyinginezo zilizokabidhiwa kwake na Katiba hii au na sheria yoyote."

Masaju ndiye Mwanasheria Mkuu wa serikali na msimamo wa serikali kisheria ameishautoa Kuwa serikali haiitaji mazungumzo na mtu yoyote kuhusu UKUTA ,na mambo mengine ya kisiasa na badala yake inataka wananchi watii Sheria na mamlaka sasa inakuwaje Jana Mbowe anaueleza umma Kuwa viongozi wa dini wameiisii Chadema iache Operesheni UKUTA kwasababu wao viongozi wa dini wanaenda kufanya mazungumzo na Rais Magufuli wakati Tayari Mwanasheria Mkuu kaishasema serikali haitaki mazungumzo Inaitaji Sheria?Hapa Mbowe umetulisha Tango Pori.


Na hata Huyo Rais Magufuli aliwapa kulinda Katiba na Sheria na Ni Magufuli ndiye aliyekuwa wa kwanza kupiga marufuku mikutano ya siasa kwasababu muda wa kufanya siasa ulishapita na kutaka watu wakafanye Kazi.Mbowe na viongozi wako wa kidini mnamaanisha rais Magufuli anataka Kulamba matapishi yake ?

Ibara ya 37 (1)  ya Katiba ya nchi inasema; " Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote".

Hivyo ni wazi kabisa Rais Magufuli hawezi kuvunja  matakwa ya Ibara ya 37(1)  ya Katiba kwa kisingizio cha majadiliano ya viongozi wa dini kwa Sababu ushauri wa viongozi wa dini halazimiki kuufuata kwasababu siyo ushauri wa kisheria wala Katiba na Mara Kadhaa Magufuli amejiapiza atafuata na kuzingatia Sheria .

Halafu sini hawa Chadema Uchaguzi Mkuu wa 2015 ilipomalizika ,Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Chadema alishindwa Katika kinyang'anyiro cha urais na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( NEC ) ,ikamtangaza Magufuli ndiye mshindi  muda mfupi baadaye Chadema walitangaza kutoyatambua Matokeo hayo .

Na ni Chadema Hao Hao wamekuwa wakimuita Magufuli ni Dikteka na wakafikia Hatua hadi za Kutengeneza Fulana zimeandikwa 'DIKTETA UCHWARA" ? 

Sasa inakuwaje Jana Mbowe Mbele ya waandishi wa Habari anatamka bila aibu Kuwa eti wale viongozi wa dini waliwashawishi wasifanye Leo Operesheni UKUTA ,Chadema aridhie viongozi Hao wa dini waende kuonana na rais Magufuli ambaye wanamuita Dikteka Uchwara wajadili kuhusu UKUTA wao ?

Hivi Katika akili ya kawaida Tayari hawa Chadema walishatoa hukumu dhidi ya Magufuli Kuwa ni Dikteta uchwara,Ana minya Demokrasia sasa iweje Jana Mbowe akubali suala la kuandamana ambalo Anadai ni la kidemokrasia akubali lipelekwe Mbele ya Dikteta Uchwara ( Rais Magufuli) ambaye Walisema anaminya Demokrasia aliamue?Uongo mtakatifu ndiyo huu.

Katika Hali kama hiyo Huyo waliyomuita Dikteta uchwara ,mminya Demokrasia atawaruhusu waandamane?Mbowe acha tabia ya kutufanya wote Hatuna akili na hatufahamu mchezo unaocheza.


Binafsi Nasema Sababu zilizotolewa na Mbowe Jana za kuahirisha zoezi la UKUTA ni dhahifu mno na zilizojaa uongo mwingi ,uchonganishi pia. Na ni hatari kutolewa na kiongozi wa aina yake Katika Jamii.

Mbowe kuzungumza mambo mengi yasiyona Uhusiano kabisa na mkutano wake wa Jana wa kuahirisha oparesheni UKUTA .Mtu makini alipaswa aende kutangaza kuahirisha UKUTA basi lakini kajikuta Mara kawa Wakili  na msemaji wa Redio Magic FM, Redio Five zilizofungiwa mapema wiki hii zimefungiwa kwa uonevu kana kwamba Waziri wa Habari na TRCA hawana mamlaka ya kuzifungia na wamezifungia bila Sababu .Ujinga mtupu.

Mbowe akajikuta Jana Akizungumzia Kufungiwa kwa Gazeti la Mawio kana kwamba Waziri wa Habari Hana mamlaka hayo .Na amesahau wahariri wa Gazeti la Mawio ,mchapishaji  na Mtoa Habari iliyosababisha Gazeti Hilo lifungiwe Tundu Lissu Kesi hipo pale katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,bado haijatolewa maamuzi.

Mbowe Kuonyesha jinsi gani Utawala wa Magufuli unawatia kiwewe akajikuta akiropoka tu eti  JWTZ limekuwa likiwatisha Raia kwasababu inarushwa Ndege zake hewani wakati anasahau JWTZ kupitia Msemaji wake walishasema wao Septemba Mosi Mwaka huu,wanasherehekea siku ya majeshi kwa kufanya usafi nchi nzima na wananchi waendelee na shughuli zao kama kawaida .

Mbowe na wafuasi wako kama Nyie ni watu safi, na Operesheni UKUTA ilikuwa ni nzuri isingesababisha vurugu kwanini umefikia Hatua ya Kusema JWTZ inawatisha Raia na zile Ndege zao ?

Ni juavyo  Mimi  wahalifu ndiyo w anaogopa wanausalama wetu Kwasababu ya hofu ya Kukamatwa kwasababu wana Tenda matendo ya kihalifu hivyo ni sahihi Chadema na wewe Mbowe muogope Ndege hizo za JWTZ kwasababu maandamano ya UKUTA mliyokuwa mmepanga kuyafanya Leo ni batiri kisheria na Hakuna serikali yoyote ingeweza kuwaacha mfanye hayo maandamano yenu haramu ya UKUTA ambayo ni wazi yalikuwa yanataka kutuletea Mashaka makubwa Katika taifa letu lakini yamekufa kifo cha Mende .

Kwani  vyombo Vya Ulinzi za Usalama ikiwemo JWTZ Kazi yake ni kutisha Raia? 

JWTZ haipo kwaajili ya kutisha Raia,ipo kwaajili ya kulinda Raia na mipaka ya nchi na siyo kosa Kwa JWTZ  Ndege zao kufanya mazoezi Katika anga ya Tanzania na Mbona JWTZ ikikaribia kufanyika kwa sherehe mbalimbali za Kitaifa kama Sherehe za Uhuru, Muungano,Siku ya Majeshi ,sherehe za kuapishwa  rais mpya Ndege vita zina pita Angani zikifanya mazoezi raha mustarehe .

Kwanini  wewe Mbowe Jana usema eti kitendo cha Ndege za JWTZ kufanya mazoezi Angani ni kutishia Raia?Kwanza ni Raia wangapi wamekulalamikia Ndege hizo za JWTZ zimewatishia Usalama?Ebu acha kupandikiza Chuki kwa wananchi na Jeshi Lao la JWTZ ambao wanaliamini na kuliheshimu.

Mbowe na viongozi wenzake muache Uongo,muwe wa kweli kwa Watanzania kwamba mmeamua kusitisha maandamano yenu haramu ambayo yalikaaniwa Kila kona na wananchi Wengi walikataa kuyaunga mkono Kwamba serikali ya Magufuli ilijiapiza adharani Kuwa endapo Chadema mngeingia mtaani mngeshughulikiwa bila huruma.

Kwanini unawasingizia viongozi wa dini ?utakuja kulaaniwa ujue ?Na kwanza inawapasa mkatubu kwa Mungu wenu kwa tabia yenu chafu isiyo na msimamo Kwani mlijiapiza mtaandamana mkataka watu wa waunge mkono,baadhi ya makada wenu wakawaunga mkono Matokeo yake wamekamatwa wapo magerezani ,wengine wamefunguliwa Kesi Nyie mpo majumbani kwenu mnakula raha na familia Zenu na maandamano mmeyahairisha.Ipo siku Mungu atawaadhibu.


Hivi siku zote ham kufahamu viongozi wa dini wapo na wakishawishi kuhusu kuacha kufanya jambo Fulani mtaacha? Kama mlilijua Hilo kwanini hadi Agosti 30 Mwaka huu, mlikuwa mkisisitiza UKUTA uko pale pale Septemba Mosi?

Siku zote za mazungumzo na viongozi wa dini Huyo pepo mchafu aliyokuwa akiwatesa alikuwa hajawa toka amewatoka Agosti 31 Mwaka huu mchana ndiyo roho mtakatifu akawaingia mkatangaza kuhairisha UKUTA?

Mbowe umesema umehairisha UKUTA kwasababu ya kushawishiwa na viongozi wenu wa kidini lakini Mbona ulivyokuwa ukizungumza uonyeshi kabisa umepata Upako mtakatifu kutoka kwa watumishi hao wa Kimungu uongee maneno yenye busara na usiwe na kinyongo lakini kupitia hotuba yako ya Jana unaonyesha wazi wazi kabisa Una gazabu za serikali ya Rais Magufuli kwakile unachodai Ina minya Uhuru wa Habari,Demokrasia wakati kupitia hotuba yako ya Jana ni dhahiri serikali hii Ina Demokrasia ndiyo maana umezungumza mambo mengine ambayo ukitakiwa uthibitishe huwezi kuthibitisha?

Kwahiyo Chadema siyo Sheria za nchi wala maandiko ya vitabu Vya dini ha hamtayajii isipokuwa mmetii ushauri wa viongozi wa dini? Maana Mungu kupitia Kitabu cha Warumi 13:1-2 kinawataka mtii mamlaka na pia Sheria za nchi zinawataka mtii mamlaka lakini kwa mujibu wa hotuba yako huku sema Chama Chako kimehairisha maandamano kwa Sababu ya kutii mamlaka na Biblia isipokuwa mume watii viongozi wa dini.Ajabu sana. 

Kama mumewe za kupuuza Biblia ,Sheria za nchi ndiyo huo ujasiri wa kuwasikiliza viongozi wa kidini ambao siyo Sheria ,vitabu Vya dini mmeupata wapi?

Chadema kuweni wa  kweli tu Kuwa Operesheni yenu haramu ya UKUTA mliyoipanga muifanye leo ilikosa Waungwaji mkono kwasababu ilipingwa   kila upande,serikali ingewashughulika kikamilifu ?

Nalipongeza Jeshi la Polisi limeweza kufanya Kazi yake vizuri tu tangu Julai Mwaka huu,Chadema ilipotangaza kuzindua Operesheni UKUTA Kwani Jeshi la Polisi hili chini ya IGP- Ernest Mangu lilikwenda sambamba na wabunifu wa Sheria ambao ni baadhi ya wafuasi wa Chadema kwa kuwakamata bila huruma na kuwafikisha mahakamani Hali iliyosababisha Chadema kuingiwa na kiwewe .Hongereni sana Jeshi la Polisi kwa kuwatia adabu.

Rai yangu kwa vyombo Vya Ulinzi Usalama viwe macho sana na Chadema tena sana, kwasababu kadri Siku zinavyozidi kwenda Chama hiki kimeanza kujipambanua kupitia kauli za baadhi ya viongozi wake ni Chama kinachotamani siku Moja siku Moja Tanzania imwage Damu kwa vurugu kwakisingizio cha Kudai Demokrasia na siku zote Uhuru bila mipaka ni sawa na uwendawazimu maana iliposema maandamano ya UKUTA yatakuwa hayana kikomo maana yake ni vurugu Tayari zingetokea.

Chadema ni Chama kilichosajiliwa hapa nchini ,na kuna mazuri yamefanywa Chama hiki Napongeza ila kadri siku zinavyozidi kwenda Chama hiki kimeanza kuiga aina ya siasa zilizokuwa zikifanywa zamani Kati ya Mwaka 1995 -2005 na Chama Cha Wananchi CUF  za vurugu,Kupambana na Polisi na kutotii mamlaka ya serikali.

Lakini serikali ikifanikiwa kukomesha aina ile ya siasa za CUF hadi Leo hii CUF imeachana kwa kiasi kikubwa na siasa zile za kidhalimu sasa hivi sasa Chadema wanaanza kuiga siasa hizo hasa Kamwe zisipewe nafasi Katika nchi yetu kwasababu za ovyo ovyo tu.

Hivyo mbinu ile ile iliyomtumika kuua siasa za kidhalimu za CUF za Kipindi kile cha kila Ijumaa CUF ilikuwa inafanya maandamano haramu Uwanja wa Kidongo Chekundu Polisi ikawa I napambana nao hadi Misikitini   Ndiyo itumike kuisambaratisha fikra za baadhi ya viongozi wa Chadema ambao Kutwa wamekuwa wakiwaamasisha wanachama wao wasitii mamlaka na Sheria za nchi na kuhamasisha watu washiriki maandamano haramu yasiyonakikomo.

Chadema Mtambue Watanzania hawapendi vurugu,wanapenda Amani hivyo ili Chama chenu kiendelee Kupendwa na wanachama wenu ,Nyie viongozi wa juu hasa Mbowe acheni tabia ya kuhamasisha wafausi wenu kushiriki oparesheni Zenu kama UKUTA ambayo Tayari serikali ilishasema ni batiri .

Mbowe wewe na viongozi wenzako wa juu mnaona raha gani kusimama majukwaani kuwashawishi wafuasi wenu wasitii mamlaka na washiriki Katika matendo ya kuvunja Sheria kama maandamano haramu kama ya UKUTA ambayo umedai umeyasogeza mbele hadi Oktoba Mosi ?Mnalipwa na nani kwa udhalimu huo?

Ipo siku Mungu atawaadhibu hiyo dhambi ya kuwashawishi watoto wawatu watangulie Mbele waandamane ,washughulikiwe na vyombo Vya dola wewe unakaa pembeni.

Ieleweke wazi licha Chadema wamesogoza Mbele  Jana Operesheni UKUTA, Chadema imebaki na kovu lisilofutika Kuwa ni Chama ambacho viongozi wake wamekuwa wakiwaamasisha wafuasi wao wasitii Sheria na mamlaka na hii ni sifa Mbaya sana kwa Chama hiki ambayo Katika awamu ya serikali ya nne kilijizolea Umaarufu sana lakini kadri siku zinavyozidi kwenda Umaarufu wake unaporomoka kwasababu hivi sasa Hakina ajenda zaidi ya kuhamasisha wabunge wake wasusie vikao Vya Bunge lilopita,waamasishe wafausi wao waandamane matendo ambayo ni ya kihuni na yanawapaka matope.

Chadema na vyama vingine Vya upinzani Nawataka mzinduke mtoke Katika usingizi wa serikali ya awamu ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mtambue na kukubali hivi sasa mpo Katika serikali ya Rais Magufuli ambayo haijui kulea wavunja Sheria ,wahuni ,wazushi.

Ndiyo maana kule bungeni baadhi ya wabunge wa Chadema waliyozungumza uongo ,kufanya matendo ya utovu wa nidhamu ndani ya Bunge walishitakiwa Katika Kamati ya Bunge na walipatikana na hatia na wamefungiwa kuingia bungeni hadi wamalize Adhabu zao na wabunge wengine w ameshitakiwa Katika Mahakama za uraiani kwa makosa mbalimbali mfano Tundu Lissu anayekabiliwa na Kesi Tatu za uchochezi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea alishitakiwa Katika Mahakama ya Kisutu na a kapatikana na hatia ya kumtolea Lugha chafu Mkuu wa Mkoa  wa Dar Es Salaam, Paul Makonda.

Muda wa kubadili tabia na wakukubali kuwa Magufuli ndiyo rais wa nchi kwa sasa na Dk.Tulia Ackson ndiyo Naibu Spika wa Bunge nyie wabunge wa  Chadema bado mnao ,anzeni sasa .

Rudini bungeni kafanye ni Kazi mliyoitumwa na Wapiga kura wenu ,Acheni wazimu kwasababu Wapiga kura wenu hatujawatuma Msuse kuingia vikao Vya Bunge kisa eti hamtaki Dk.Tulia  tena bila Sababu za Msingi .Dk.Tulia yupo Kikatiba Bungeni kama hamtaki tumieni Katiba kumuondoa lakini siyo njia za kiuni mnazofanya Kumkataa Dk.Tulia.Mnajidhalilisha Mbele ya Jamii ya watu wanaofikiri sawa sawa.

Mwisho nawashauri wafuasi wa vyama Vya upinzani hasa Chadema Kuweni macho na maagizo mnayopewa na viongozi wenu maagizo mengine msikubali kuyatekeleza  kwasababu ni haramu kisheri na mkiyatekeleza mwisho wa siku vyombo Vya Sheria vitawashughulikia Nyie binafsi Huyo mtu anayeitwa Mbowe hamtokuwa nanyi selo ya Polisi, mahakamani na gerezani. Chadema Mmechafuka,Mjisafishe. Naomba kutoa hoja.

Mungu Ibariki Tanzania.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
1/9/2016.


Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment