Thursday, 8 September 2016

Re: [wanabidii] Kumbe Mbowe msaliti wa nguvu ya umma?

Kosa la kuchanganya mtu na taasisi katika sakata hili lilianza pale Mbowe aliposema NHC imefanya hivyo kwa kuwa yeye ni M'kiti wa chadema. Hapo ndipo ilipoanzia kujadili deni hilo na uongozi wa chama
--------------------------------------------
On Thu, 9/8/16, 'misangocharles' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Kumbe Mbowe msaliti wa nguvu ya umma?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, September 8, 2016, 8:11 AM

Nadhani tuweke pembeni wakati
mwingine ushabiki wenye makengeza. Kumchanganya mtu na
taasisi sidhani kama ni sahihi. Huwezi kushutumu watu kwa
ujumla wake kwa kosa la mtu mmoja. Deni lake lielekezwe
kwake na sio kwa taasisi.
Hivi hamkumbuki, kuna kada na kiongozi maarufu wa CCM
alituhumiwa kusambaza arv feki na akajipatia fedha lukuki.
Huyu aliyeua watu kwa dawa feki kwa nini hakuhusishwa na CCM
na mbona povu halikututoka kiasi hiki? Sina maana ya
kumtetea Mbowe maana hanisaidii kwa lolote na niseme wazi
niliacha kazi kwake kwa sababu sikukubaliana na mambo fulani
yasiyo sawa kwangu.
Lkn hii hainifanyi nisiseme ninapoona tunachanganya hoja ya
msingi kwa kuchafua na wasiohusika

Sent from my Huawei Mobile

'mpombe mtalika' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:


SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limefanya uamuzi mgumu
dhidi ya
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Freeman
Mbowe. Uamuzi wa kumshinikiza alipe malimbikizo ya deni lake
la kodi kwa
shirika hilo la taifa, deni la zaidi ya shilingi bilioni
moja. Mbele ya NHC, Mbowe kupitia kampuni yake ya Mbowe Hotels
Ltd ni mdaiwa
sugu na hili limethibitishwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC,
Nehemia Mchechu
katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam, Agosti
24, mwaka huu.


Pengine si tu mbele ya NHC bali hata mbele ya Watanzania
wengi, Mbowe
ni mdaiwa sugu kwa kurejea takwimu hizo rasmi za NHC, ambalo
ni shirika
mali ya wananchi linalojiendesha kibiashara ili hatimaye
kutoa gawiwo
kwa serikali kuu na kuboresha hali za makazi ya wananchi
nchini.Kwa
hiyo na kwa vyovyote vile, hujuma yoyote dhidi ya shirika la
umma
ikiwamo hii ya kutolipa kodi ni sawa na hujuma dhidi ya umma
ambao chama
anachokiongoza Mbowe kimekuwa kikijinadi kupitia salamu
yake ya "nguvu
ya umma."


Tayari Mbowe amekwishafanya utetezi dhidi ya tuhuma hizi za
kuitwa
mdaiwa sugu wa NHC. Kwa bahati mbaya, utetezi wake umebeba
siasa,
pengine kwa sababu tu ya kutafuta kichaka na kuficha aibu ya
kihistoria
ya kuwa miongoni mwa wadaiwa vinara na sugu wa NHC.Katika utetezi wake wa Agosti 24, mwaka huu,
baada ya Mkurugenzi Mkuu
wa NHC kutangaza kuwa mwanasiasa huyo ni mdaiwa sugu, Mbowe
alitoa
taarifa kwa umma akijitetea kwa kupiga porojo za kisiasa,
kwanza akikiri
kuwapo deni ama mgogoro wa kibiashara wa miaka mingi baina
ya kampuni
yake na NHC."Kumekuwepo
na ukakasi wa muda mrefu kuhusiana na mkataba wetu wa
umiliki, uendelezaji na uendeshaji wa jengo hili
unaochagizwa na msimamo
wangu wa kisiasa," anasema Mbowe na kuendelea; "Haki na
Uhuru wetu wa
kufanya biashara kama raia wengine umekuwa ukiingiliwa mara
kwa mara
katika mazingira yanayoambatana na vitisho kiasi ambacho
maamuzi kadhaa
hayafanyiki kwa hofu ya kisiasa kwamba itakuwa kumwongezea
nguvu
mpinzani."Anasisitiza
akitaka Watanzania waelewe kuwa hadaiwi. Bado anapiga siasa
akisema; "Sitafungwa fikra, sitafungwa mdomo na sitaacha
kuutetea
ukweli, haki na demokrasia katika nchi hii kwa misingi ya
kulinda
kinachodhaniwa ni maslahi yangu ya kibiashara." Anasema
wafanyabiashara
wengi wamekuwa wakifungwa fikra na midomo ndani ya nchi hii
kwa kuogopa
hila na ghiliba za watawala.Anasema;
"Ni heri kufa masikini nikiwa nimesimamia ukweli, kuliko
kuishi tajiri niliyetawaliwa na ubinafsi, woga, hofu na
ubatili."


Lakini pamoja na kauli hiyo ya kukanusha kudaiwa katikati
ya hoja za
kisiasa, NHC kwa niaba ya Watanzania, uongozi wake umesimama
imara kudai
haki ya umma. Unaweza kujiuliza Mbowe ni mtu wa namna gani
pale maslahi
yake yanapokinzana na umma? Je, yuko tayari kwa kiasi gani
kulinda
maslahi yake bila kujali athari kwa umma? Mbowe anapaswa
kufahamu haya.NHC
kudai wadaiwa si siasa


Pengine historia ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
imemkalia kando
Mbowe huyu wa Chadema. Nitamkumbusha jambo ili afute hoja
zake nyepesi
kwamba kitendo cha NHC kudai wadaiwa sugu ni ajenda ya
kisiasa.Takriban
miaka 44 iliyopita, yaani mwaka 1972, Freeman Mbowe akiwa na

umri wa miaka 11 tu kwani alizaliwa Septemba 14, 1961,
Shirika la Nyumba
la Taifa lilifanya uamuzi mzito wa kudai wadaiwa wake sugu.Katika
kutangaza uamuzi wake huo, Ofisa Uhusiano wa NHC kwa wakati
huo,
E. Musabalala, aliutangazia umma namna shirika hilo la umma

litakavyolinda maslahi ya umma. Akasema shirika limefanya
uamuzi wa
kuunda kamati maalumu nchini ili hatimaye kuwafukuza
wapangaji ambao ni
wadaiwa sugu, waliolimbikiza kodi za shirika hilo.Kwa kumkumbusha tu Mbowe ni kwamba, kamati ya
kwanza kuundwa ilikuwa na
watu 14 na ilifanya uchambuzi kwa wapangaji sugu katika
nyumba za
shirika hilo la umma maeneo ya Ilala, Upanga, Ukonga na
Barabara ya
Morogoro, mjini Dar es Salaam. Kazi hiyo ilianza Oktoba,
mwaka 1972.Na uamuzi huo wa kuuda kamati ulikuwa wa
mwendelezo tu kwa sababu
tayari uamuzi wa shirika kuwafukuza wapangaji wadaiwa sugu
ulikwishaanza
mwezi Mei, mwaka huo wa 1972.Kwa
hiyo, Mbowe asilete siasa kwamba anakandamizwa kwa sababu
eti ni
mwanasiasa wa upinzani. Ajue tu kwamba rekodi zinaonesha
uamuzi wa NHC
kushughulika na wadaiwa sugu kama yeye, wenye kufanya hila
za hapa na
pale, ulianza zamani tena akiwa na umri wa miaka 11.
Asimuonee
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Mchechu, ajue shughuli hii ni pevu,
uamuzi wa
busara kwake ni kulipa fedha za umma, asiishie tu kutamka
jukwaani ….
Peopleees … power, bali ajue nguvu ya umma sasa inadai
chake kupitia
NHC.Si wa
kwanza kutupiwa virago


Katika utetezi wake, Mbowe anasema ametupiwa virago na
kwamba
utekelezaji wa uamuzi wa NHC kupitia dalali wake ni wa
uonevu kwake,
watu wake wanadai hata taasisi mbalimbali za serikali
zinadaiwa lakini
kwa nini hazikutupiwa virago kama yeye. Anahoji, iweje yeye
pekee na
anahitimisha kwamba anapigwa siasa.Hapa niweke wazi kwamba kuna tatizo la
kumbukumbu kuhusu NHC kufanya
uamuzi mgumu kwa wateja wake ambao wadaiwa sugu, wadaiwa
wanaohujumu
umma. Nitajadili mambo mawili muhimu hapa.Mosi,
Mbowe akumbuke kuhusu kile kilichoandikwa katika gazeti
linalomilikiwa na familia yake la Tanzania Daima la Oktoba
12, mwaka
2013, habari iliyoandikwa na mwandishi na mpiga picha wa
gazeti hilo,
Joseph Senga (Mungu amrehemu).


Habari ile ilieleza uamuzi mgumu wa NHC kuwatupia virago
madaktari
wawili wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa sababu mwajiri
wao, yaani
Muhimbili kulimbikiza deni.Madaktari
hao wawili ni Dk. Wambura Chacha na mwenzake bingwa wa
upasuaji katika Kitengo cha Mifupa (MOI), Profesa Joseph
Kahamba. Hawa
wanaweza kuwa mashahidi kwamba NHC haifanyi siasa, bali
inadai fedha za
umma.Madaktari
hao, kwa mujibu wa habari hiyo ya Tanzania Daima walikuwa
wakiishi katika nyumba namba 355 mali ya NHC, Mtaa wa Umoja
wa Mataifa
jijini Dar es Salaam. Mwajiri wao alikuwa amelimbikiza deni
la miezi 15
lililokuwa limefikia Sh 9,738,000. Sasa itakuwa Mbowe mwenye
deni la
bilioni takriban 1.2? Halafu unadai eti siasa!Operesheni hiyo ya wakati ule ya kudai fedha za
umma kutoka kwa wadaiwa
sugu kama Mbowe iliendeshwa na Meneja wa Kitengo cha
Kukusanya Madeni
wa NHC, Japhet Mwanasenga. Kwa wakati ule wa operesheni hiyo
Muhimbili
ilikuwa ikidaiwa Sh milioni 135.6, yakiwa ni malimbikizo ya
malipo ya
pango kwa vipindi tofauti.Kwa
hiyo ya Mbowe na wenzake kwamba anaonewa kwa kutupiwa virago
wakati
serikali na taasisi zake ni wadaiwa sugu haina ukweli, bali
ni porojo
za kusaka huruma ya kisiasa. Kama ataweka kumbukumbu zake
vizuri,
atakumbuka pia kwamba hata Wizara ya Habari, Utamaduni na
Michezo wakati
huo ikiongozwa na

Waziri Dk. Emmanuel Nchimbi, ilitupiwa virago na
NHC.
Asilete ndoto za mchana.


Pili, kuna jambo analopaswa kulielewa Mbowe. Kwamba
serikali na taasisi
zake zinaweza kufanya mawasiliano ambayo Mbowe kama mmoja
wa wadaiwa
sugu si lazima apewe taarifa za namna wadaiwa wenzake
walivyojipanga
kulipa madeni yao. Serikali inayo bajeti yake na hili Mbowe
anapaswa
kulijua vizuri kwa sababu ni kiongozi wa kambi rasmi ya
upinzani
bungeni, na ajue yeye kama mtu binafsi au kampuni zake
bajeti yake ni
siri yake.Kwa
hiyo si sahihi kudai kuwa umetupiwa virago na wenzake
hawajatupiwa.
Usahihi kuwa, na kwa kweli kwa mtu makini anapaswa kutambua
kuwa jambo
la msingi ni kulipa deni, tena deni linalohusu fedha za umma
si
kujitetea kuhusu muda wa kulipa kwa wadaiwa wenzako. Kila
mdaiwa anaweza
kuwa na makubaliano tofauti na anayedai.Haenei
katika ubepari, ujamaa


Chadema, ambacho Mbowe ni mwenyekiti wake kinajinadi kuwa
na mrengo wa
kibepari. Ni kweli ubepari unahusu kutumikisha watu ili
bepari anufaike
zaidi lakini katika huo huo ubepari, hasa kwa mabepari wa
kweli ni
lazima unayemtumikisha aendelee kula, kubaki katika afya
njema ili
endelee kuishi na uendelee kumtumikia. Hili inaonekana
halimo kichwani
mwa Mbowe, wale anaojinadi nao kuwa ni nguvu ya umma sasa
hao hao ndio
wanaomdai kodi aliyolimbikiza kupitia shirika lao la umma
– NHC.Tazama,
utu wa mabepari wa kale kwa kurejea kijiji Saltaire, kule
Shipley, kijiji ambacho ni sehemu ya Jiji la Bradford, pale
Yorkshire ya
Magharibi, England, miaka 163 iliyopita, yaani mwaka 1853
au kijiji cha
Port Sunlight kule Merseyside, England, mwaka 1888, miaka
128
iliyopita. Hoja ni kwamba mabepari hawa wa kale walisaidia
umma wao
karne zaidi ya moja lakini Mbowe, Mwenyekiti wa chama cha
kibepari,
anadaiwa kodi ya umma na bado anakuwa mbishi. Ni kama vile
hafafani hata
na ubepari wa kale enzi za kikoloni, achilia mbali upebari
wa kisasa.Wakoloni
ambao mwaka 1885, baada ya ripoti ya Tume ya Kifalme England

walianzisha, kwa mara ya kwanza, mpango wa makazi kwa
wafanyakazi
kupitia sheria iliyoitwa Housing of the Working Classes Act
ya mwaka
1885. Sasa Mbowe hajui kwamba lengo la NHC kudai kodi ya
umma ni
kusaidia wafanyakazi wa nchi hii katika suala la makazi,
wafanyakazi
ambao Rais John Magufuli aliahidi kuboresha maslahi yao,
maslahi ambayo
bila shaka ni pamoja na makazi bora kwa kadiri
inavyowezekana.Mbowe kalipe deni lako, usikwaze umma. Umma
unahitaji kufaidika na
jengo ulilohodhi kwa kulimbikiza kodi, lile jengo lililopo
makutano ya
mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi, katikati ya jiji la Dar es
Salaam.
Hima hima Mbowe, jitahidi kuheshimu na kutunza haki ya kiapo
ya uadilifu
na maadili ya utumishi wa umma, kwa nafasi yako kama
mbunge, kiongozi
wa kambi ya upinzani bungeni na zaidi ya hapo, mwenyekiti wa
chama kikuu
cha upinzani nchini. Lipa deni kuleta utulivu ndani ya umma
wa
Watanzania, uamuzi wa kulipa unaweza kusaidia kuepusha
mpasuko kitaifa
na kifamilia.

Raia Mwema
--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment