Mtalika.
Hyu ndiye mgombea makini ambaye chama makini kilimuona hafai kuwa mgombea urais kupitia kwake. Tunakumbuka alivyotaka kuwabambikiza wana Monduli nani awe mbunge wao yeye 'atakapokuwa rais'. Naamini watu makini ndani ya Chadema akiwamo Dr. Slaa, Tundu lisu, Mnyika na wengine watakaa kimya wakisubiri uchaguzi uishe waanze kukijenga upya chama chao. Naamini wanaweza kupiga kampein za ubunge majimboni bila kumpigia Rais ikitokea akatangazwa huyo. lakini kingine ninachokitarajia ni Magufuli kukosa mpinzani wa Maana. Hii inawezekana kwa sababu nakumbuka kusikia kuwa Katiba ya Chadema inahitaji mtu kukaa miezi sita ili aweze kugombea uongozi wowote. Sasa hawa wanaohamia ikitokea mtu akaweka pingamizi likakubaliwa si hatari? Hata hivyo ushindi wa CCM juu ya CDM kama Lowasa anasimama ni dhahili
--------------------------------------------
On Wed, 7/29/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Lowassa na Majibu ya Hasira kwa Swali la Msingi
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, July 29, 2015, 10:22 AM
Wadau Habari; jana
ilikuwa siku ya kipekee sana kwa historia ya Tanzania ambayo
tuliahidiwa na
tuliisikia minong'ono mingi na tetesi za kila leo juu ya
kuhama chama kwa
aliyekuwa mgombea urais kwa tiket ya CCM ndugu, EL.
Binafsi nampongeza
kwa kuitumia haki yake ya kidemocrasia na kufanya maamuzi
magumu; kama
mtanzania nisiyefungamana na upande wowote nimestaajabishwa
sana na mambo
mawili makubwa.
Mosi ni juu ya
umiliki wake wa card ya CCM, EL inasemekana ana miliki card
namba 15 ya
Uwanachama ndani ya CCM, lakini siku ya jana alijivua
uwanachama na kupewa
rasmi card ya CDM, sasa bado najiuliza imekuaje kamanda huyu
amejiondoa CCM na
kwenda CDM lkn bado anamiliki card ya chama hicho? Maana
jana sikuona akiirudisha
card ya CCM ili ichanwe chanwe pale mbele ya macho
yetu.
Lakini kama hiyo
haitoshi bado najiuliza inawezekanaje Kiongozi mkubwa kama
yeye anathubutu
kutoa majibu ya hasira mbele ya Taifa hili juu ya swali la
msingi ambalo
lilimchafua yeye na baadhi ya Viongozi wa wizara
husika.
Kwa kusema kwamba
NANUKUU; "Nilipoitisha kikao cha "Government
negotiation team"
nikawauliza mbona nasikia huu mkataba una matatizo? mimi
nina uzoefu wa kuvunja
mikataba na huu tuuvunje! wakaomba ruhusa watoke nje kwa saa
moja, baada ya
hapo waliporudi wakasema wamepigiwa simu toka mamlaka ya juu
mkataba usivunjwe
"what else could I have done?" Mwisho wa KUNUKUU,
Sasa najiuliza hapa
inawezekanaje PM umeitisha kikao cha subordinates wako alafu
anatokea wa
kukuambia kuwa et nimewasiliana na wakuu wamekataa hilo,
nani basi mwenye
kupaswa kufanya consultation na Wakuu wenzake kati ya watu
hawa wawili EL kama
PM au Subordinates?
Lakini pia napata
shaka pale namna ambavyo swali la msingi lilivyojibiwa kwa
kusema kwamba,
NANUKUU; "Am sick of Richmond, mtu yoyote mwenye
ushahidi wa mimi kuhusika
na Richmond aende mahakamani, kama huna just shut up.
Nilichukua uamuzi kwa
niaba ya serikali.
Nimeondoka
madarakani miaka nane iliopita, mambo haya yameongezeka
yamepungua, mikono yangu
ni misafi na mtu mwenye ushahidi acha kupigapiga kelele,
peleka
mahakamani" mwisho wa KUNUKUU; Kwa uelewa wangu wa
kawaida kabisa unyeti
wa jambo hili haukutaka jibu la namna hii bali watanzania
tungeridhishwa zaidi
endapo tungepata majibu mazuri kwa kina na yenye
kujitosheleza badala ya kuwa
mkali kiasi ambacho inatuacha na maswali mengi kwamba ile ni
namna ya kututisha
na kutuziba midomo kama ambavyo ilitokea pale kwa wana
habari wenzangu au ni
nini hasa?
Kama hii haitoshi
bado najiuliza, Je na ile hoja ya Dr.Slaa kwamba ushahidi wa
jambo hili anao na
yupo tayari kwenda kuthibitisha mahakamani leo hii sisi
watanzania tunaibebaje
hii statement kuwa naye alikuwa anabwabwaja tu au namna
gani?
Lakini nathubutu
kwenda mbali zaidi kwa kujiuliza Dr.Slaa na wenzake
wanasimama vipi Jukwaani
kumnadi kwa kumtakasa mtu huyu ambaye wao walikuwa
wanachangia kumchafua?
Mambo haya
yananipa shida kuyapatia majibu basi nabaki kujiuliza bila
mafanikio naombeni
wadau mnisaidie kung'amua.
"Majibu ya hasira kwa swali la
Msingi"
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment