Monday, 12 September 2016

Re: [wanabidii] CHADEMA wanamaanisha au wanatania?

Mbowe ndiye yuko Objective sana,,, au nao ni utani mwingine?!?
--------------------------------------------
On Mon, 9/12/16, Joseph Ludovick <josephludovick@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] CHADEMA wanamaanisha au wanatania?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, September 12, 2016, 8:41 PM

Tangu
alipokataa kubadili gia angani. Ila Jana amemkosoa RAIS!
Yule yuko objective sana!
On 12 Sep 2016 17:30,
"Emmanuel Muganda" <emuganda@gmail.com>
wrote:
Nimeacha kumsoma Mwanakijiji muda mrefu
sana.em
2016-09-12 4:15 GMT-04:00
'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Na. M. M. MwanakijijiSIYO kila utani unachekesha; utani mwingine unaitwa utani
mbaya kwani
unaweza kumfanya mtu akasirike na wakati mwingine unaweza
hata
kusababisha ugomvi.Ninachoogopa ni kuwa ndugu zetu wapinzani inawezekana
wanapenda sana
utani; tena ule utani mbaya. Kama hawatanii basi inawezekana

wanamaanisha wanavyovisema na kama hawavimaanishi basi
wanatutania na ni
utani ambao haupaswi kuwepo kwani mambo tunayoyazungumzia
ni makubwa
sana na yana matokeo ya kudumu katika maisha ya mamilioni ya
Watanzania.Tuchukulie kwamba CHADEMA wanamaanisha wanayoyasema. Kwamba,
kwa mfano
wanamaanisha kabisa kuwa Magufuli ni "dikteta uchwara"
na kuwa anasigina
Katiba na kuwa anatawala bila kufuata sheria.Kama madai haya ni ya kweli kabisa basi kuna baadhi ya mambo
wasingeweza
kuyaachilia hewani hasa kama wanajua wanasimamia
walichoamini.Baada ya kuliweka taifa katika hali ya wasiwasi ya mgongano
viongozi wa
CHADEMA waliamua kurudi na kuahirisha wakisema kuwa
wameombwa na
viongozi wa dini na watu wengine 'wazito' kuwa wasifanye
maandamano yale
ambayo yalikuwa yenye lengo la kuionesha dunia kuwa
Magufuli ameleta
utawala wa kidikteta.Hili linanikumbusha jambo ambalo kiongozi wa wapigania haki
za weusi wa
Marekani Martin Luther King Jr alikutana nalo wakati wa
harakati zake
mwanzoni mwa miaka ya sitini.Martin Luther King alikuwa akiongoza maandamano na kukaa
chini katika
kupinga vitendo mbalimbali vya kibaguzi katika mji wa
Birmingham, Jimbo
la Alabama.Mikutano na maandamano hayo ambayo yalikuwa yanafanyika kila
mahali
yakasababisha mahakama kutoa zuio la maandamano hayo
likipiga marufuku
mikutano ya kila aina; hata kunyanyua bango kupinga
ilizuiwa. King na
wenzake waliamua kupuuzia amri hiyo ya mahakama akiamini
kuwa kutii amri
ovu ni kuendeleza uovu.Kutokana na kukaidi amri hiyo King na wenzake kadhaa
wakaswekwa ndani
katika Jela ya Mji wa Birmingham. Akiwa jela, kundi la
viongozi wa
kidini – hasa weupe – wakimchukulia yeye kama mchungaji
mwenzao
waliandika barua kali ya kumkosoa mbinu zake na taratibu
zake za
kuupinga utawala muovu. Jambo hili lilimuuma na kumuudhi
King na akaamua
kuandika majibu ya hoja za wachungaji hao.Kama kuna mwanaharakati yeyote ambaye hajawahi kusoma barua
hii (unaweza
kuipata kwa kuigoogle) nashauri watu wasome kwani ni
kiongozi mzuri
sana. Katika hili King anasema mojawapo ya mistari maarufu
sana kuwa
"dhulma mahali popote, ni dhulma mahali pote"
(Injustice anywhere, is injustice everywhere).Akijibu hoja kuwa maandamano waliyokuwa wanafanya kinyume na
agizo la
sheria ni uvunjaji mkubwa wa sheria King alijenga mojawapo
ya hoja nzito
sana zilizowasaidia kuwasimamisha wanaharakati wengi baada
yake.Alisema kuwa "naomba kuwakilisha kuwa mtu anayevunja
sheria ambayo
dhamira yake inamtuma kuamini ni ya kidhulma, na yuko tayari
kukabiliana
na adhabu ya kosa hilo ili kuamsha dhamira ya jumuiya juu
dhulma yake,
kiukweli kabisa anaonesha utii mkubwa zaidi wa sheria!"Sasa ndugu zetu CHADEMA wamesema jambo kubwa sana; jambo
lenye matokeo
na jambo ambalo walitaka taifa zima liamini kuwa ni kweli
– kwamba
Tanzania inakabiliwa na udikteta na kuwa nikinukuu maneno
yake ya juzi
wakati wa kutangaza kuahirishwa kwa maandamano "Na wote
tu-mashahidi wa
jinsi ambavyo viongozi wa ngazi zote wa CHADEMA na wanachama
wa kawaida
wamekamatwa, kuteswa na kufunguliwa mashtaka ya uonevu kwa
sababu tu ya
kutetea au kutekeleza haki na uhuru wao kwa mujibu wa Katiba
yetu.Madai yote aliyoyatoa ni mazito. Sasa kutuambia kuwa
wameombwa na
viongozi sijui wa dini na watu gani wengine ndio wameona
umuhimu wa
kuahirisha maandamano ya UKUTA hawajitendei haki wao wenyewe
na
hawalitendei haki taifa.Hawajitendei haki kwa sababu sasa hivi sijui ni jambo gani
zito
wanaloweza kumtuhumu Rais na serikali yake ambalo watu
wataona kweli
linawauma hasa tukizingatia kauli kali na maonyo ya mikwara
ya kila
namna kuelekea ile Septemba Mosi. Mara kadhaa walinukuliwa
kuwa tarehe
ile iko pale pale na hakuna kurudi nyuma.Hawajalitendea haki taifa kwa sababu baada ya kuahirishwa
UKUTA baadhi
ya ndugu zetu hawa wameanza kuhoji "gharama"
zilizotumika na vyombo vya
dola na serikali kudhibiti UKUTA. Kwamba, hata kama
maandamano
hayakufanyika lakini Serikali imepata hasara na wametumia
hela nyingi
kwa wanajeshi na nyenzo mbalimbali.Sasa kama lengo la UKUTA lilikuwa ni kuibebesha serikali na
walipa kodi
mzigo zaidi wa gharama basi lengo hili limefanikiwa. Lakini
kama
wanafurahia kuwa mpango wao umesababisha matumizi
"makubwa" ya fedha
nalo ni jambo la kuhoji kama wanamtakia mema Mtanzania wa
kawaida.Lakini kama wanachosema – na ipo mifano mingine mingi –
siyo mambo
ambayo wanaamini hasa bali wanachukulia kama utani; kama
namna ya
kujipatia au kujiongezea ujiko wa kisiasa (political clout)
basi
wananchi nao watawachukulia kiutani utani na mwisho itakuwa
ni kama
simulizi la yule mtoto aliyelia "mbwa mwitu" akitania
kwa sababu tu
hakutaka kuchunga na siku mbwa mwitu wa kweli alipokuja
alipoita na
kuita hakuna aliyejitokeza. Utani mwingine mbaya.Lakini kama hii tarehe mpya ya Oktoba Mosi ni ya kweli na
wanaamini
kabisa kuwa wanamaanisha, nina ushauri mdogo sana lakini
utaendana na
dhima ya Martin Luther King Jr. Viongozi wa CHADEMA na
viongozi wengine
wa upinzani ambao wameamua kukabiliana na hicho wanachokiita
"udikteta
uchwara" basi maandamano yajayo yawe kwanza kabisa ya
viongozi wa
upinzani nchini.Watangaze kuwa maanamdano hayo ni ya viongozi. Nina uhakika
wakifanya
hivyo, hata jeshi la polisi na vyombo vya usalama vitakuwa
tayari kuwapa
ulinzi viongozi hawa watakapoandamana kutetea kile
wanachokiamini.
Lakini kama wanatania…

Chanzo Rai
 --

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegr
oups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegr
oups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/op
tout.


--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/
optout.

--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment