By Lizabon
Wadau amani iwe kwenu.
Kama mnavyojua kwa sasa vyama vya siasa nchini vipo kwenye pilika za kusaka wagombea wa kuwakilisha vyama vyao kwenye nafasi ya urais, ubunge na udiwani. CCM tayari imekamilisha zoezi la kumpata mgombea urais na mchakato kwa ajili ya kuwapata wagombea ubunge na udiwani unaendelea.
CHADEMA, CUF, NCCR na NLD walikubaliana kusimamisha wagombea wa pamoja kwenye nafasi zote hizo. Awali ilionekana kuwa wanaweza kufanikiwa lengo lao hilo hasa kwa vile walitoka wakiwa wamoja kwenye Bunge Maalum la Katiba na waliendelea kuwa pamoja kwa muda mrefu. Hata hivyo wamekuja kuvurugana katika hatua za mwisho kipindi ambacho tulitaraji wangezidisha mshikamano wao.
Nikirudi kwenye mada, ni dhahiri shahiri kwamba baada ya Oktoba 2015, vyama vya CUF na NCCR vitapotea kabisa kwenye ushawishi wa siasa za Tanzania Bara. Zipo sababu nyingi zitakazopelekea hali hiyo kutokea. Miongoni mwa sababu hizo ni;
1. Hila mbaya, uchoyo na ubinafsi wa CHADEMA ambao ni washirika wenza wa UKAWA. CHADEMA hawapendi kuwa chini ya mtu au chama kingine. Hoja wanayojenga ni kwamba chama hicho ni kikubwa sasa na kina uwezo wa kusimamisha wagombea kwa kila jimbo na kata. Ni kutokana na hili, ndo maana CHADEMA wamesimamisha wagombea kwa zaidi ya majimbo asilimia 70 na asilimia 30 zilizobaki wamepewa vyama vingine. Aidha, mkakati mwingine wa siri wanaofanya CHADEMA ni kuwaandaa kwa siri wagombea katika majimbo ambayo waliwaachia vyama vingine na kwamba mwanzoni mwa au wiki ya pili ya mwezi Agosti UKAWA utavunjika na kwamba CHADEMA hawatapoteza kitu na yale majina waliyoyaandaa yatawasilishwa kwenye NEC. Huu ni mkakati wa siri sana na ni wachache tu tunaoujua. Kwa hali hiyo, vyama vya CUF na NCCR ambavyo vilibweteka kwa kujiegamia kwa CHADEMA vitakuwa vimepoteza.
2. Vyama vya CUF na NCCR vinakabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha. Mpaka sasa, vyama hivi havina uhakika wa kupata fedha watakazotumia kwa ajili ya uchaguzi Mkuu. Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad amemueleza mwenyekiti wake Ibrahim Lipumba kuwa CUF hawana fedha kwa ajili ya uchaguzi Mkuu na kwamba ikiwa Lipumba anataka kugombea nafasi ya Urais, atafute fedha za kutosha kutoka kwenye vyanzo vyake. Maalim amemueleza Lipumba kuwa fedha shilingi milioni 600 walizopata na CHADEMA na shilingi bilioni 2 walizopata kutoka kwa washirika wao wa nchi za Kiarabu zimetumika kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar ambako wana uhakika wa kuibuka washindi. Kauli hii ya Maalim Seif ni dhahiri kwamba CUF Tanzania Bara itakuwa na wakati mgumu sana katika kipindi cha kuelekea Oktoba 2015.
3. Ujio wa ACT unaimaliza kabisa NCCR Mkoani Kigoma. ACT inaonekana kujiimarisha zaidi mkoani humo kuliko maeneo mengine ya nchi. Katika kuonesha kuwa wamedhamiria kuuteka mkoa huo, tayari wamemchukua mbunge wa Kasulu Mjini Moses Machali. Aidha, inadaiwa kuwa wabunge wengine kama David Kafulila na Felix Mkosamali wamekalia kuti kavu kwenye majimbo yao. Ikiwa ACT itafanikiwa kuteka majimbo yaliyokuwa chini ya NCCR, ni dhahiri kuwa chama hicho kitapotea kabisa hasa ikizingatiwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia hana uwezo wa kushinda Jimbo la Vunjo analotaka kugombea.
4. Wabunge wa CUF, Salum Halfan Barwani wa Lindi Mjini na Suleiman Ally Bungara aka ----- ambao walipata kura za huruma na za hasira kutoka kwa wana CCM hawana uhakika wa kutetea majimbo yao. Hii ni dhahiri kwamba majimbo yao yatarejea CCM na CUF itabaki mikono mitupu.
Wadau, nayasema haya sasa na nawaomba muweke kwenye kumbukumbu zenu. Baada ya Oktoba 2015, CUF na NCCR Mageuzi vitakuwa historia kwa siasa za Tanzania Bara na ni CHADEMA pekee ndiyo itakayokuwa chama cha upinzani. Time will tell.
chanzo Jf
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment