Tuesday, 21 July 2015

[wanabidii] Kwanini ITV haitangazi habari za ACT Maendeleo?

Wadau,nimekuwa nikifatilia kwa karibu habari za kisiasa zinazoonyeshwa na vyombo vya habari ITV ikiwa ni miongoni mwao. Nilichobaini ni kuwa wanatangaza vizuri sana habari nzuri za CHADEMA na vyama vingine isipokuwa ACT Maendeleo.

Ukirejea hoja ya shirikisho la vyombo vya habari kuhusu kutetea uhuru wa vyombo vya habari likiongozwa na Mheshimiwa Dr. Mengi sioni uhalisia wa kuwepo huo uhuru hata sasa kwa wamiliki wa vyombo hivyo. Huenda ndio maana serikali inaona ni vema ikaweka regulator wa kusimamia utoaji wa habari kwani wamiliki wameshindwa kuvifanya vyombo vyao kuwa huru.

Kwa mfano ACT Wazalendo imefanya mikutano mingi mikoa mbalimbali Tanzania, vyombo vya habari mbalimbali vilitangaza, isipokuwa ITV.Machali jana kajiunga na ACT Wazalendo, vyombo vingine vimetangaza isipokuwa ITV.

Ndo kusema hii sio habari kwao.....????..Nafikiri ITV inaharibu reputation yake kwa wananchi waliokuwa wakikiamini chombo hiki.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment