Thursday, 23 July 2015

Re: [wanabidii] Re: LOWASSA UMEPIGWA KWENZI NA DOLA LA CCM,BONYEA

Kuamia ni kufukuza ndege shambani na kuhamia ni kitoka makazi fulani uliyoyazoea Australia mazingira fulani uliyoyazoea na kwenda kwenye mazingira mengine  kama mkoa mtaa nyumba nk

On Jul 21, 2015 8:27 PM, "'Mike Zunzu' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Assignments huwa zina viwango wa maneno, najaribu kuwaza mwenzetu anavyohangaika kupata points wakaka wa ku analyse. Watu wamemwambia sana lakini wapi haelewi, hakujifunza kusoma habari, kisha unaandika habari hiyo hiyo kwa kifupi bala kupoteza maana ya habari? Kama alikuwa mroro basi, ni kosa lake.



On Tuesday, 21 July 2015, 10:41, Augustine Rukoma <arukoma66@gmail.com> wrote:


makala ndefu lakini point mpaka utumie darubini kuipata
On Monday, July 20, 2015 at 8:25:58 AM UTC+3, Happiness Katabazi wrote:


LOWASSA UMEPIGWA KWENZI NA DOLA  LA CCM ,BONYEA

Na Happiness Katabazi

KWA zaidi ya wiki Moja sasa kumekuwa na taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na mhusika ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM),Edward Lowassa kuwa anakusudia kuamia  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA).

Taarifa hizo zimekuja ikiwa ni siku Chache tu tangu CCM imalize mchakato wake Julai 12 mwaka huu, wa kumpata  mgombea urais ambapo Lowassa wenzake kushindwa kufikia hatua ya tano bora hali iliyosababisha wafuasi wake akiwemo Mbunge wa Songea Mjini,Dk.John Nchimbi,Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kujitokeza hadharani kupinga mchakato ule na Kudai  Kanuni za CCM zilivunjwa na wengine wameamua kuamia  Chadema.

CCM waliitimisha mchakato wao kwa kumpata Mbunge wa Chato,John Pombe Magufuli Kuwa mgombea wao wa urais na mgombea mwenza  ni Samia Suluhu Hassan.

Kwanza nataka Ieleweke wazi kuwa kila Mtu ana Haki ya kujiunga na Chama chochote za siasa  na haki hiyo umewekwa Katika Ibara  ya 20 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 , inasomeka hivi; 

"Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo."

Hivyo basi Kama taarifa hizo zinaukweli basi Lowassa atakuwa anatumia haki yake hiyo ya Kikatiba ya kujiunga na Chama cha siasa anachokitaka.

Waswahili wanamsemo usemao lisemwalo lipo Kama halipo linakuja na Dalili za Mvua ni mawingu,Dalili hizo Tumeanza kuziona kwa Mbali .

Ushauri wangu kwa Mzee Lowassa Kuwa Kama kweli anawazo hilo la kuama CCM kwenda Chadema kwasababu CCM haijapitisha Jina lake Kuwa mgombea  urais ,aliache  wazo Hilo Mara Moja Kwani halitakuwa na manufaa kwake  binafsi na familia yake .

Halitakuwa na manufaa kwake  kwasababu wewe Lowassa amekaa ndani ya serikali,CCM kwa muda mrefu sana, anafahamu  jinsi hivyo vyombo viwili vinavyofanyakazi zake .

Kama utaamua kuama CCM kwenda upinzani ujiandae kukabiliana na Changamoto zifuatazo Kesi mbalimbali na karaha mbalimbali.Je upo Tayari Katika Hilo? Na Je Una ubavu wa kuvumilia vibweka hivyo?

Lowassa usisikitike sana jina Lako kutopitishwa na CCM, bali kaa chini utafakari ni kwanini Hilo lilitokea. 

Je ulikidhi  vigezo? Na Kama  Kanuni zilipindishwa ,kwanini basi  Mungu alishindwa Kuzuia uhuni huo usitendeke na Kanuni zisivunjwe?

Kwa wanasiasa ninavyowajua wanasiasa wa nchi hii walivyotawaliwa na mizengwe tena wakati wa uchaguzi hata kama mlikuwa ni marafiki uwa manageukana utafikiri hamjawahi kufahamiana na kushughulikiana Kavu Kavu.

Hivyo kwa Kuwa wewe Lowassa na genge lako la kampeni mlikuwa mkianza vitendo Vya kuvunja Kanuni wakati mwingine hali iliyosabisha Kuzua mjadala Katika Jamii,uenda basi Ndio maana viongozi wako wa CCM nao wakaamua kutumia kile kinachodaiwa na wafuasi wako 'uhuni ' kukata jina lako  maana wakati mwingine mtu mwenye mamlaka unaweza kutumia njia za kihuni kutoa maamuzi dhidi ya Mtu mhuni idi mradi tu nchi Inakuwa salama.


Mapema kabisa nilikushauri kupitia makala zangu Kadhaa zilizokuwa na kichwa Cha Habari ( LOWASSA UWEND URAIS UTAUSIKIA REDIO TBC1) na (MADA SITA CCM  HAMMO KWENYE URAIS),hukuta kunisikia hadi yaks kufika yaliyokufika ambayo yamekusababishia majeraha moyoni.


Lowassa je uoni  hayo yaliyokufika ni malipo ya Mwenyezi Mungu kwako?Maana Kama Mungu angetaka CCM ipitishe jina Lako CCM ingelipitisha.

Kwa tunaofuatilia siasa za nchi hii kwa wazi na Siri Minasema yaliyomkuta Lowassa kule CCM alistahili .

Tujikumbushe Wimbo iliotungwa na mwanamuziki wa Muziki wa Dansi nchini,Ally Choki ' Mzee wa Farasi' usemao Mtenda kanitendewa .Baadhi ya maneno yaliyomo  ndani ya wimbo huo ni ;

" Mtenda akitendewa uisi kaonewa Yale yote aliyofanya uwa yanamrudia ....mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu unauma...aliyoyatenda yeye yote kasahau...malipo ni hapa hapa Duniani Eeeh,usimzalau Mkunga na uzazi ungalipoo Aaah...."

Mzee Lowassa Maudhui ya Wimbo hayo yatafakari sana naninaomba yakurejeshe Mwaka 2005 Katika Kipindi cha mchakato wa kumsaka mgombea urais CCM, wewe Lowassa na genge la wahuni maarufu la Wanamtandao mlishiriki kikamilifu wakati mwingine kuwachezea rafu baadhi ya wagombea wa CCM akiwemo Dk.Salim Hamed Salim,Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye na Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara,John Malecela kuwachafua chafua kupitia baadhi ya waandishi wa habari mliokuwa mmewaweka mfukoni  kupitia vyombo Vya Habari .

Hali iliyosabisha Dk,Salim ,Malecela,Sumaye kunuka kwa uzushi tu ambao ulikuwa ukienezwa na genge la wahuni la wanamtandao ambao wewe Lowassa ulikuwa Mfuasi Mtiifu wa genge Hilo ambalo hivi sasa genge Hilo limesambaratika na wafuasi wa genge Hilo wamekorofishana wamekuwa ni maadui wa kuitisha na wanalaluana wao Kwao.

Dk.Salim aliizushiwa siyo Raia wa Tanzania na alikuwa Mwanachama wa Chama Kimoja kule Zanzibar ambacho kilikuwa kinapingana na serikali iliyokuwa madarakani ,wakati Sumaye aliizushiwa kajilimbikizia mashamba na amepora mashamba ya wananchi Mkoani Morogoro ,na pia ameficha Sh.Tilioi  Tatu Kwenye Akaunti yake.

Hali iliyosababisha Dk.Salim ,Sumaye Kufungua kesi Katika Mahakama Kuu Kulishitaki Gazeti la Mwananchi na Tanzania Leo kwa kuchapisha Habari hizo za uongo na viongozi Hao walishinda Kesi hizo .

Na Hakuna kitu kilichonifurahisha hapa nchini Kama genge Hilo la wahuni maarufu Kama Wanamtandao liliposambaratika na hivi sasa Ndio limekufa kabisa Kwani endapo genge hili lisingesambaratika hivi sasa Kama taifa tungekuwa  Katika Hali Mbaya Kwani liliumiza watu ambao wengine walikuwa hawana hatia kwasababu ya Sababu zao kijinga na kihunihuni tu .

Sasa kwa mazingira hayo ya Kuwa Kwenye kundi liloshiriki kuwashuhudia wenzao uzushi na uongo, kwanini Isifike mahali Mungu nae akalipa kisasi kwaniaba ya Hao walioumizwa na kundi la wanamtandao Mwaka 2005 kwako  wewe Bwana Lowassa Katika mchakato wa CCM 2015?

Minakushauri Lowassa ukae chini utulize akili zako vizuri ,ujielewe Kuwa wewe ulishawahi Kuwa Waziri Mkuu,waziri ,mbunge na Mwana CCM wa muda mrefu Na hii siyo Mara yako ya kwanza jina Lako kuenguliwa na CCM Katika mchakato wa Kugombea urais .Mara ya kwanza ilikuwa Katika uchaguzi wa CCM Mwaka 1995 jina Lako lilikatwa ulipogombea urais CCM ulitulia.

Na hadi sasa bado unapata Stahili zako toka serikalini na utambue wewe pia ni mfanyabiashara ,unamke,watoto na Una ndugu na Jamaa wanakutegemea na bado wanakuitaji ili uwa saidie  wakiwemo baadhi ya wabunge waliokuwa Kwenye kambi yako kufa na kupona ila hawafiiki kichinichini wewe kuamia Chadema wanasema Katika Hilo hawatakuwa pamoja na wewe.

Lowassa utambue Kuwa huna nguvu ya asili ya kukubarika na ndani na nje ya Chama  Kama aliyokuwaga nayo Mwenyekiti wa Chama CHA NCCR - Mageuzi enzi hizo, Augustine Mrema ambaye alikuwa akipendwa na watu Wengi tena bila kutoa Fedha wala kutoa ahadi za kuwapa watu vyeo wala kuzungukwa na watu wanaosaka madaraka na wale waganga wa serikali ya awamu ya nne Kama ulivyozungukwa wewe na watu wa aina hiyo.

Lowassa Kama kweli unataka kuamia Chadema, ukumbuke ni Katibu wa Chadema, Dk.Wilbroad Slaa Katika Viwanja Vya Mwembeyanga Temeke Dar Es Salaam, na Katika maeneo mengine amenukuliwa akikuita wewe Lowassa ni fisadi wa mali za umma.

Na siyo peke yake ,pia baadhi ya wafuasi wa Chadema nao wamekuwa wakikuita wewe ni fisadi uliopindukia, sasa eti ghafla CCM imekata jina Lako Leo hii wafuasi wa Chadema tena wengine ni viongozi wa juu wa Chama hicho n marafiki zangu wanajitapa kwakukusifu Lowassa ni mtu safi na wanamsubiri Chadema.

Minimewauliza hao baadhi ya viongozi wa Chadema wanawazimu kichwani au wanamatege ya akili?

Nimelazimika Kuwauliza maswali hayo kwasababu hadi sasa Hakuna mahala  popote panapoonyesha  Chadema imekusafisha  Lowassa Kuwa ni Mtu safi na siyo fisadi tena Kama walivyokuwa wakimuita awali.

Lowassa Kama kweli unataka kuamia Chadema, jiulize kwanini Leo Chadema wanaokuona ni Mtu safi,una sifa za kiongozi bora?

Je kwakuwa wameona una wafuasi Wengi ndani ya CCM na una wafadhili Wengi wenye Fedha wanaokufadhili Katika siasa zako Ndio maana Chadema hivi sasa Ndio wanakutaka uamie Katika Chama chao?

Tumewasikia hao Madiwani na wana CCM   waliojiunga na CHADEMA wiki iliyopita wamesema wameamua kuama CCM kwasababu eti Lowassa amekutwa jina lake.

Swali langu Je ikitokea kweli ukaamia Chadema nako huko Chadema wasipopitisha jina Lako ,wewe na hao wafausi wako Mtaama Chadema kwenda Chama gani kingine?

Minaisi hawa wanaojiita ni wafuasi wako uwenda sio wazima katika vichwa vyao.

Najiuliza hivi CCM walijiunga kwaajili tu Lowassa lazima apitishwe jina lake na lisipopitishwa Ndio wanaama Chama ?

 Basi hao wafuasi wako ni madikteta ambao wanataka uamuzi wao tu na wala hawaheshimu uamuzi wa mamlaka ya Chama chao Cha CCM na Kama ni hivyo basi hawana nidhamu?

Mzee Kingunge Yule pale amepinga mchakato uliompata mgombea urais CCM lakini hatujamshuhudia akihama CCM.

Siwezi kumbeza kirahisi rahisi  Mzee Kingunge kwasababu naamini Kingunge ni mtu mzima Anaujua mazuri na Mabaya yote  yanayofanywa  na CCM wakati wa uchaguzi ,hivyo Mzee Kingunge uwenda anajua kilichofanyika Katika mchakato uliompata mgombea urais CCM Mwaka 2015 ambao Mimi na wengine hatuji Je ni kweli Kanuni zilivunjwa au laa Kwani ukweli wanaujua wao wenyewe.

Hata hivyo mapema kabisa Kabla ya CCM kupitisha jina la mgombea Kingunge ambaye yeye alitangaza na kusema anamuunga mkono Lowassa na  alitahadharisha  Kuwa kuna Dalili chafu za CCM kupitisha jina la mtu asiye kubalika na Wengi na kukata Majina ya watu wanakubalika Hali ambayo itasababisha vurugu.

Na ndivyo ilivyokuwa CCM ilitumia vigezo vyao ikampitisha Magufuli mgombea ambaye watu walikuwa hawampi uwezekano mkubwa wa kushinda Kama Lowassa,Membe na hivyo kufanya Lowassa ,Membe ambao walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushindwa na Kuwa na wafuasi Wengi kutopitishwa na CCM  .

Hali iliyosababisha watu wanaodaiwa ni wafuasi wa Lowassa kufanya fujo na Jeshi la Polisi kuweka Ulinzi mkali  katika  Mji wa Dodoma wakati vikao hivyo Vya CCM vikiendelea na Katika Kikao cha NEC baadhi ya wajumbe wakati Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete akiingia Katika mkutano ule walikuwa wakiimba   Wimbo wa ' Tunaimani na Lowassa" Hali iliyosababisha Kikwete akiri Kuwa Hali hiyo haijawahi kutokea.

Hata hivyo mchakato ulimalizika salama Magufuli amekubalika na watu Wengi kwasababu Hana rekodi chafu na anauzika kwa wananchi vizuri tu na kwakuwa Watanzania Wengi ni Kama tuna ubongo wa Ndezi tumeishasahau vibweka vilivyotokea Dodoma  Katika kumpata mgombea urais wa CCM ,tu naendelea na mambo mengine ila baadhi ya watu wacheche bado wanavinyongo.

Sasa hiyo kambi ya Lowassa iache nongwa Kama ndugu wa mume,ikubali Matokeo yaliyotokea na iache kumjaza Ujinga Mzee Lowassa wa kuama CCM kwenda Chadema.

Kwasababu ushauri wa kuama CCM ni  wa Kikatiba ila siyo mzuri kwa Lowassa Mwenyewe Kwani mwisho wa siku atakayekuja kuumia Moja kwa Moja ni Mzee Lowassa na siyo wapambe wake. 

Wapambe wake mwisho mwisho wa siku  watamkimbia Kama baadhi ya wapambe wake walivyoonza kumkimbia hivi sasa.
...
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment