Kwenu ndugu zangu mnaonithamini, napenda kuwataarifuni kuwa nitagombea ubunge Mufindi kaskazini ili hatimaye niliongoze jimbo hilo kwa kipindi cha 2015 -2020....nitagombea ubunge huo kwa ticket ya Chama cha Mapinduzi( CCM). Kinachonisukuma haswa kugombea ni kuwa naona wananchi wa jimbo hilo tunastahili mema zaidi ya ukiwa mbaya tulionao...Lakini pia mambo mengi katika mustakhabali wa uongozi wa nchi yetu huwa yananisumbua sana...na nafikiri ni muda mwafaka wa mimi kujitosa huko kwa mapenzi mema ya nchi yangu. Nakumbuka Askofu Wa jimbo la Iringa..mhashamu Ngalalekumtwa aliwahi kusema...ukiona mtu anafundisha wakati wewe ukimsikiliza...halafu ukajisikia moyoni na akilini kuwa unaweza kufundisha vizuri zaidi yake....basi hiyo ni dalili nzuri ya kuwa wewe kipaji chako ni UALIMU...jimbo la Mufindi kusini liliwahi kuongozwa na Josef Mungai na kwa sasa mbunge wake ni Mahamud Mgimwa, ambaye pia ni naibu waziri wa maliasili na utalii..Zipo habari kuwa jimbo hilo litakuwa majimbo mawili...yaani jimbo la Mafinga na Mufindi kaskazini...mimi nitagombea Mufindi kaskazini.... elimu yangu ni Bsc: Chuo kikuu cha Dar es salaam, Msc of Aquatic ecology, chuo kikuu cha Bremen Germany, Msc of fish farming, chuo kikuu cha Bergen Norway..Kikazi nipo Tanzania Fisheries Research institute (TAFIRI) kama senior research scientist...Nilizaliwa 1974...nina mke na watoto watatu...Dini ni mkristo hai...value zangu : Napenda heshima na kuthaminiana..naamini uongozi ni kazi maalumu..hivyo basi inastahili watu maalumu..nafikiri ni muda mwafaka sasa kwa nchi yetu kulitazama hilo na kuiponya nchi...Naombeni maombi yenu...muda si mrefu tutapita katika mchujo wa chama...sio kazi rahisi, rafu ni nyingi lkn naamini nitashinda...Ngupula.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment