Sunday 31 May 2015

[wanabidii] URAI 2015: Mapinduzi Kwenye Sekta ya Elimu!

URAIS 2015: Mapinduzi Kwenye Sekta ya Elimu!

 

Kwenye awamu ya nne tumeshuhudia Serikali ya CCM ikijenga shule nyingi na kuzalisha na kuajiri walimu wengi kuliko kipindi chochote kile katika historia ya nchi yetu. Tumeshuhudia vyuo vingi vya elimu ya kati vikipanda hadhi na kuwa vya elimu ya juu, na tumeshuhudia idadi ya wahitimu wenye elimu ya chuo kikuu wakiongezeka mwaka hadi mwaka. Sambamba na jitihada hizi, tumeshuhudia wahitimu wakifanya usaili wa mchujo wa awali kwa ajili ya nafasi za kazi kwenye uwanja wa Taifa. Tumeshuhudia baadhi ya taasisi zikilalamikiwa kwa kutoa ajira kwa undugunaizesheni. Hii inatanabaisha kuwa tuna tatizo si tu la kukosa elimu yenye kutoa ujuzi wa kujiajiri bali pia tuna wasomi wengi wenye elimu ya juu kushinda mahitaji ya soko la ajira. Tumeshuhudia shule za kata zikitoa wahitimu wenye ubora ambao wamekuwa wakisonga mbele zaidi kwenye masomo yao, huku wengine wengi wakifeli . Ni lazima tufanye paradigm shift.

 

Ni wazi kwamba hatupaswi kuendelea kuwekeza kwenye kusomesha watu wetu kwenye elimu ya juu kwa kipindi hiki, pengine tujikite zaidi kuwekeza kwenye kuongeza ubora na kwenye utafiti na teknolojia.

 

Nini tunahitaji kwenye elimu sasa?

 

Tunahitaji:

 

(1.)         Kuongeza ubora wa shule zetu kwa kujenga maabara, maktaba, mabweni, viwanja vya michezo, karakana (zinapohitajika) na nyumba za walimu. Pia kuhakikisha shule zote nchini zinakuwa na umeme, maji na mtandao mzuri wa mawasiliano ili kuongeza ari ya walimu kuishi kwenye maeneo yote bila kuchagua (retention scheme).

 

(2.)         Kuboresha mitaala ili kuifanya elimu yetu iwape wanafunzi si tu elimu ya ufahamu bali pia ya ujuzi na uvumbuzi; na zaidi component ya elimu ya ujasiriamali na communication skills ni lazima.

 

(3.)         Tuanzishe mfumo wa motisha kwa walimu wetu kulingana na jiografia na mazingira wanapofanyia kazi (differential incentives scheme). Walimu wanaofundisha maeneo ya mbali na makao makuu ya wilaya na wanaofundisha kwenye maeneo yasiyo na huduma mbalimbali muhimu ni lazima walipwe posho maalum zaidi ya wenzao wanaofundisha maeneo ya mijini.

 

(4.)         Kuwa na mpango wa dharura wa kuanzisha shule za VETA kwa kuamua kuzigeuza baadhi ya shule za sekondari kuwa za VETA na kuziwezesha zipate vifaa na wakufunzi wenye ujuzi ili zianze mara moja kutoa mafunzo kwa vijana waliohitimu darasa la saba na hawakupata fursa ya kusonga mbele, na kwa wale waliohitimu kidato cha nne na hawakupata fursa ya kusonga mbele, na hivyo hivyo kwa waliohitimu kidato cha sita. Mpango huu utatoa fursa ya kupata vijana wengi wenye ujuzi kwa haraka kwa ajili ya kujenga vijiji na miji yetu (mafundi uashi, ubunifu wa mavazi, ushonaji nguo, useremala, mafundi bomba, umeme, madereva, mafundi mitambo, mabwana shamba vijijini n.k.). Shule za VETA zitatoa fursa kwa vijana waliopoteza matumaini, zitawapa ujuzi wa kujiajiri, lakini pia wahitimu wa VETA wanahitajika sana kwenye ajira za sekta binafsi.

 

(5.)         Kurekebisha mfumo wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa kuweka mfumo ambao unatoa usawa (equity) kwa mwanafunzi kulingana na hali ya uchumi wa familia yake na si kigezo cha kozi anayosoma pekee (mfano mwanafunzi mtoto wa mbunge ama wa waziri analipiwa gharama zote bure wakati mtoto wa maskini anayesomea biashara anatakiwa kujilipia aidha ada yote ama sehemu ya ada hiyo).

 

 

--
"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
                +255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment