Sunday, 31 May 2015

Re: [wanabidii] SIMPIGII KURA MGOMBEA MASKINI

Msameheni Yona alipoteza ufahamu toka oktoba 2010 hawezi kulikataa hili
SENT FROM ALCATEL ONETOUCH TABLET

'salumkango' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Sio watu ni Yona Maro. Kwa kweli ni hoja dhaifu mno. Na hata mifano aliyoitoa haiendani kabisa. Tatizo la Tanzania sio utajiri bali ni jinsi viongozi wetu wanavyoupata huo utajiri

Sent from my Samsung Galaxy smartphone.

-------- Original message --------
From: 'Mike Zunzu' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Date:31/05/2015 12:56 PM (GMT+03:00)
To: wanabidii@googlegroups.com
Cc:
Subject: Re: [wanabidii] SIMPIGII KURA MGOMBEA MASKINI

Kwa mtizamo huu, kwa hiyo watu mnaamini Rais akiwa masikini atawaogopa matajiriri, utumbo na udumaavu wa akili kufikiria hivyo, Kwa taarifa mtu aliyeleta habari hii jamvini hakuwaza kwamba hekina na uungwana wa kutaka kutenda haki kwa kila mmoja ni msingi wa uongozi bora.
Hizi ndizo sababu zinazotufanye tuchague watu wasiofaa matokeo yake mtu akiwa madarakani ndipo tunaanza kujuta. Uchaguzi unaofaatia tunafanya kosa hilo hilo, kama wazazi wanaotafuta kupata mtoto wa jinsia fulani lakini kila wakati wanapata mtuto wa jinsia ambayo tayari wana watoto wa njisia hiyo.
Ninachofahamu mleta habari hii wakati mwingine amekuwa akileta habari mbali mbali zingine zikiwa na mafunzo tele, ningelitegemea amesoma habari za viongozi mbali mbali duniani hata kama siyo wote, lakini kua viongozi waliofanya makuwa ka nchi zao je ni kwa sababu walikuwa na mali? Soma habari ya kiongozi aliyeileta Malaysia hapo ilipo leo, je alikuwa Tajiri?  Utamlinganisha Nyerere na waliomfuatia combined. Kuna kiongozi wa Bolivia na wengine wengi. 
 Kiongozi mzuri ni yule atakayetumia katiba kuingoza nchi ndiye atakayewezesha nchi kusonga mbele, siyo ku sign sheria kwa mbwembwe.

On Sunday, 31 May 2015, 9:20, Herment Mrema <hmrema11@hotmail.com> wrote:

Magafu,

Ogopa umaskini wa akili, umaskini wa roho na umaskini wa mfuko.  Ni hatari kuliko cancer kwani angalau ukiwa na cancer unajua pa kuanzia lakini ukiwa na umaskini wote wa aina tatu utaanzia wapi?.

Pole Watanzania maskini wenzangu kwani tumeliwa na tumefanywa maskini ili waendelee kututawala watakavyo.  Nalililia Tanzania yetu

Cheers

Herment

Date: Sun, 31 May 2015 11:09:22 +0700
Subject: Re: [wanabidii] SIMPIGII KURA MGOMBEA MASKINI
From: gmdmagafu@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Hoja hafifu sana. Unajaribu kutushawishi Watanzania ambao wengi wetu ni maskini tuikane haki yetu ya kuchaguliwa, siyo? Usitushawishi Watanzania kuwapigia kura wagombea ambao wametajirika kupitia ufisadi. Kuvumilia wizi na kuwaita wezi eti "wajanja" kunaharibu nchi yetu. Sisi sote ni Watanzania. Mishahara ya Watanzania tunaijua vizuri kwa sababu ndio hiyo tunayopekea sisi pia. Utajiri mwingine hauelezeki hata kwa mshahara wa juu kabisa wa mfanyakazi wa serikali ya Tanzania. Watanzania tuko zaidi ya mil 45. Najua wajinga ni wengi watakaokuunga mkono lakini hatuwezi wote kuwa wajinga hivyo.

Na kwa hakika Nyerere mwaka 1995 alikuwa mmoja wa wale ambao hawakuwa wajinga hivyo. Nyerere alijua hatari ya kuwaruhusu wagombea wenye kutumia ushawishi wa pesa kupigiwa kura. Kwa hiyo aliwatupilia mbali kabisa hata wasifike katika hatua ya kupigiwa kura. Wapigakura wana njaa sana. Na njaa tayari imeanza kuonekana - kwenye CCM yenyewe, mitaani, vyuo vyetu, nk. CCM watatunza heshima yao kama watawaondoa wagombea wenye kutegemea ushawishi wa pesa wasifike kwenye hatua ya kuigiwa kura chamani kama Nyerere alivyofanya 1995. Wakiruhusiwa kupigiwa kura, basi lazima pesa ishinde. Na kila mwekezaji hutegemea faida. Pesa zao lazima wazirudishe wakiwa Ikulu (+faida).  

Wagombea wa Bara katika CCM wana vurugu na uchu sana (huku wakidai kuwa Wapinzani ndio wana uchu wa madaraka). CCM wawatupe hawa wagombea wa Bara kwa kuwapa Wazanzibari nafasi ya kugombea safari hii. Isitoshe Zanzibar inaonekana kuwa na watu wenye sifa zaidi kuliko Bara. Kuna Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar mwenye uzoefu wa uongozi wa juu ambao hakuna mtu yoyote wa Bara mwenye ku-match.

2015-05-30 23:54 GMT+07:00 Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>:
SIMPIGII KURA MGOMBEA MASKINI

Rais wa Kenya ,Uhuru Kenyatta ni mmoja wa matajiri wakubwa wa Afrika , inasemekana Aliachiwa urithi wa ardhi kubwa sana na baba yake ambaye alikuwa rais wa kwanza wa Kenya , Mzee Jomo Kenyatta .

Toka ameingia madarakani amefanya mabadiliko mengi na kuwajibisha wengi ya karibuni zaidi ni kuwajibisha wakuu wa mashirika ya umma zaidi ya 20 kutokana na tuhuma za rushwa .

Prof Peter Mutharika ambaye ni rais wa Malawi wa sasa alitangaza mali zake alipoingia madarakani ambazo ni dola milioni 4 za kimarekani pamoja na vitega uchumi vingine alivyonavyo na hisa .

John Kerry , Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wakati alipotakangaza kugombea urais wa Marekani alitangaza mali zake ambazo zilikuwa zaidi ya dola milioni 30 za marekani hapo ni nyumba zake , hisa zake na jinsi anavyolipa kodi .

George Bush Mkubwa na Mdogo wote walikuwa marais wa Marekani , wote ni wamiliki wa moja ya kampuni kubwa kuliko zote za mafuta na Gesi ulimwenguni utajiri wake hausemekani lakini wote waliwahi kuwa marais wa marekani .

Rais wa Sasa wa Marekani , Barak Obama alitangaza mali zake kabla ya kuukwaa urais ambazo zilifikia dola milioni 5 atakapomaliza muhula wake wa 2 atatangaza tena mali zake na mengine mengi ambayo yatakuwa wameshakaguliwa na chama cha wahasibu wa marekani pamoja na taasisi nyingine za serikali .

Kwahiyo wewe unasema si Tajiri , lakini umekuwa waziri kwa miaka 10 , tunajua safari zako zote za nje unalipwa posho kiasi gani na msururu wa watu unaoenda nao kwa kipindi hicho cha miaka 10 , bado wewe ni mbunge unavyoenda bungeni unalipwa posho .

Ukiacha hili la uwaziri tunajua ulikuwa unafanya shuguli nyingine kama ni za serikali au binafsi kabla hujawa mbunge wala waziri huku kote ulikuwa unatengeneza maisha yako na ya familia yako na kama una mke hata mkeo nae ni mfanyakazi kwahiyo kipato chenu kwa pamoja kilikuwa kikubwa kiasi Fulani iweje leo utuambie wewe ni maskini ?

Hapa Kwetu inaonyesha mtu kuwa na hela au kuwa tajiri basi huyo hatakiwi kugombea urais au ubunge tunataka wale maskini wanaojionyesha kwamba wana hela chache na milolongo mengine mingi sana .

Kuna baadhi ya wagombea wanajinasibu masikini saa hizi lakini hawako radhi kuonyesha mapato na matumizi yao toka wameingia serikalini kwenye ngazi ya ubunge na uwaziri kwa kipindi chote .

Nikiambiwa nipige kura kati ya mgombea tajiri na maskini nitampa tajiri ambaye ameweka utajiri wake hadharani na ambao umekaguliwa na vyombo kama TRA na vingine nchini kuthibitika kwamba hazina utata wowote .

Kiongozi tajiri anatupa funzo moja kuu kwamba yeye ameongoza kampuni yake kwa mafanikio kwa kipindi Fulani kabla ya kuamua kugombea urais , anajua mambo ya mikataba , makubaliano , mikopo na masuala mengi yanayohusu biashara na maisha kwa ujumla kuliko baadhi ya wagombea .

Nchi yetu inaingia kwenye kipindi cha Uzalishaji wa Gesi , mafuta , Urani na maliasili nyingine nyingi hii inahitaji mtu mwenye uwezo huo wa biashara , maelewano , mikataba , mikopo na maendeleo si mtu yoyote tu .

Lengo la makala hii sio kumpigia kampeni Fulani , ni kusema ukweli uliopo tu ili tuweze kuwa huru .

YONA FARES MARO
0786 806028

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment