Saturday 30 May 2015

[wanabidii] URAIS 2015: Kuhusu Mapinduzi Kwenye Sekta ya Afya!

URAIS 2015: Kuhusu Mapinduzi Kwenye Sekta ya Afya!

Kama ambavyo nimekuwa nikibainisha hapa kwamba katika vipaumbele tutakavyoweka kwenye serikali ya awamu ijayo, cha kwanza kikiwa kuondoa umaskini na kukuza uchumi kwa malengo ya kuzalisha ajira za kutosha; cha pili kikiwa kutoa huduma bora kwa jamii; na cha tatu kudumisha utawala bora, leo nitachambua kwa ufupi nini kinapaswa kufanywa ili kuboresha huduma za afya kwa watu wote nchini.

Changamoto kubwa kwa serikali kwenye afya ni upatikanaji wa fedha. Ilivyo sasa, asilimia 65 ya bajeti yetu kwenye afya inalipwa na wafadhili, fedha za ndani ni asilimia 35 tu! Hili ni jambo la aibu. Na halikubaliki. Tumeshindwa kufikia malengo ya azimio la Abuja kuwa bajeti ya afya kwa nchi zilizoridhia na kusaini mkataba ule ni kuwa tutenge asilia 15 ya bajeti yetu kwenye afya. Tumekuwa tukirusha rusha miguu kwenye kati ya asilimia 8 na 12 tu, na tena kwa msaada mkubwa wa wafadhili. Hii imesababisha mdororo wa huduma za afya nchini: vituo kukosa madawa, vifaa tiba na vitendanishi; majengo kuwa machache; huduma za afya kuwa mbali na wananchi; na watumishi kwenye sekta hii kukosa motisha ya kazi kutokana na kulipwa mishahara midogo na kufanya kazi kubwa, ngumu, katika mazingira mabaya na magumu na kwa masaa ya ziada bila posho stahiki.

Kwenye afya mkakati ninaopendekeza unapaswa kuwa na mambo makubwa yafuatayo ya kufanya:

1. Kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na bima ya afya ya namna moja ama nyingine (Universal health insurance coverage).

2. Kuanza kuchaji malipo kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya (tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa watanzania wako tayari kulipia gharama za afya ili mradi tu ziwe na ubora stahiki - dawa na vipimo vipatikane, wahudumu wawe na staha na huruma kwa wateja na zipatikane kwa haraka) - hili litapaswa kwenda sambamba na kutengeneza mfumo wa ruzuku ambao utawalipia wazee, mama wajawazito, watoto, na watu wengine wasio na uwezo (siyo kusema huduma bure, naongelea makundi haya kukatiwa bima na pesa za ruzuku toka serikalini)

3. Kupeleka madaraka halisi ya umiliki na uendeshaji wa vituo vya kutolea huduma za afya kwenye mamlaka husika za kiutawala (fiscal decentralisation). Madaraka ya umiliki na uendeshaji wa vituo yatakuwa kwa wananchi wa eneo kituo kilipo, na yatakuwa madaraka kamili.

4. Kupeleka kampeni za kitaifa (kama za chanjo, lishe, uzazi wa mpango n.k.) kutoka juu sambamba na ruzuku za kutekelezea miradi hiyo. Pesa hizi za ruzuku zitapelekwa kwenye vituo kwa mfumo wa ushindani unaotokana na malengo mahsusi yaliyowekwa.

5. Kuweka mfumo wa ushindani ambao utatoa motisha kwa vituo ama maeneo ya utawala kwa kadri yanavyofikia malengo yaliyowekwa ya kiafya (pay-for-performance) siyo kupeleka bajeti kutoka juu kwa mazoea. kwa kuwa vituo vitakuwa chini ya mamlaka hizo, vikisimamiwa na bodi za afya zenye nguvu ya maamuzi yote yakiwemo kuajiri na kufukuza, kupanga bajeti na kufuatilia utendaji wa vituo hivyo, hakuna kituo kitazembea. Wafanyakazi watawajibishwa na bodi zilizochaguliwa na wananchi. Maana pia bodi zitawajibishwa na wananchi.

6. Serikali kuu itabaki na majukumu ya kuhakikisha vituo vya afya vinatoa huduma kwa viwango na ubora unaopaswa kwa kutunga sera, kutoa miongozo mbalimbali ya huduma, kusajili vituo na kuvifutia usajili, na kukagua ubora wake.

Kwa uchache, haya ni mapinduzi yanayopaswa kufanyika haraka ili tupate mabadiliko tunayoyataka kwenye ‪#‎TanzaniaTuitakayo‬. Ukitaka kusoma kwa kina mawazo haya yamo kwenye kitabu changu, ‪#‎Kigwanomics‬.

Wakatabahu,
Hamisi Kigwangalla, MD.


--
"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
                +255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment