Sunday, 31 May 2015

[wanabidii] FURSA YA KUGOMBEA URAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 2015

Ndugu Watanzania ,

Katika kipindi cha miongo miwili sasa ( ninataka kusema miaka 20 )  sasa Serikali ya Jamhuri ya Muungano imekuwa ikiongozwa na raia  kutoka upande wa Bara.  

Na kwa kipindi kirefu CCM imekuwa ikitueleza kuwa imeshaweka misingi bora ya kumuwezesha mwana - CCM kuweza kuongoza taifa letu.

Na tumekukwa tukisisitiziwa kuwa nje ya CCM hawezi kupatikana kiongozi aliye bora kusimamia maslahi mapana ya Tanzania.

Na hivi majuzi tumeshuhudia pia uibukaji wa matumizi yasiyo na kiasi ya fedha kwa baadhi ya wateule - binafsi kutaka kujenga ushawishi ili wateuliwe kuwa wagombea wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  

Na kwa bahati njema kabisa wateule-binafsi hawa wengi wanatoka pia upande wa Tanzania Bara;

Na katika kipindi hicho hicho kwa uzoefu tuliokuwa nao yawezakana pia kwa upande wa vyama vya upinzani kukawa na wateule-gombea wa nafasi ya kiti cha rais wa Jamhuri yetu tukufu kutoka Bara.

Na tunafahamu vema kabisa kuwa Watanzania wenye uwezo na umakini katika kutuvusha hapa tulipo wanapatikana pande zote za Jamhuri yetu. Tena  wasio na hila wala kuwezeshwa KIFEDHA ili kutangaza teule-binafsi  zao ;  

Na zaidi sana yafahamika pia kuwa kiuchumi au kibiashara fedha hutumika kama MTAJI. 

Na yafahamika pia , ikiwa biashara inasuasua katika kujiendesha basi huhitaji kupata MTAJI ama kama mkopo toka wa vyombo vya fedha ama kwa kutoa/kuuza hisa kwa watu wasio husika moja kwa moja katika uendeshaji BIASHARA hiyo; lakini hatima yake yaweza(kwa kutegemeana na asilimia ya mchango) kupelekea wasimamizi wa BIASHARA husika kupoteza uhuru wao wa kutoa maamuzi sahihi kwa maslahi mapana ya biashara na kulazimika kufuata miongozo au  MATAKWA ya waongeza MTAJI;

Na kwa kuwa tumethibitishiwa hapa na wateule-binafsi kuwa ili waweze kutanganza nia yao ya kutuomba fursa ya  'KUENDESHA BIASHARA yetu WATANZANIA' imewalazimu kupokea MTAJI toka kwa Wahisani hata kabla hatujawakabidhi uongozi wa yenyewe;

Na  kwa kuwa yafahamika wazi wazi kibepari kuwa mtaji huwezekezwa kwa dhumuni la kujipatia faida siku za usoni.  Hata kama siku hizo si kesho au kesho kutwa. Kwa wafanyabiashara kubwa kubwa kipindi cha matazamio huweza kuwa miaka takriban zaidi ya mitano !

Na kwa kuwa weteule-binafsi wetu wamejithibitisha kuwa na uwezo wa kutumia MTAJI wa wawekezaji katika kujinadi umahili wao wa kuliongoza taifa hili, wakati huo huo serikali hii hii wanayotaka kuiongoza haina MTAJI wa kusimamia 'BIASHARA' ya kuinua maisha ya Watanzania!

Na kwa kanuni za kibiashara, inapotokea BIASHARA fulani ikashindwa kujiendesha  kifaida kwa kukosa tija na ufanisi ( matumizi mabaya ya MTAJ kwa kukiuka masharti ya mtoa MTAJI, soko baya , misukosuko ya kiuchumi nk) basi wenye hisa ( kwa kuchangia fedha, ama kutoa vitendea kazi (ardhi, mashine, usafir) kwa matarajio ya faida) wataibuka na kuifilisi ili kufidia kile walichowekeza;

Na kwa kuwa tuna wateule-binafsi waliotueleza kuwa wamepewa 'MTAJI' wa kutangazia nia zao kutoka kwa ' Watafuta Faida '  kabla hata ya kupata nafasi ya kutuendeshea 'BIASHARA' wanayotaka kuisimamia ya kuinua maisha ya Watanzania;

Kwa haki ya kikatiba kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano bila kurejea ibara wala kifungu; naropoka kuwa ;

Wakati sasa umewadia wa kila chama cha siasa kuwapendekeza wagombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka upande wa Tanzania Visiwani.  


Lengo , nia na sababu ni kuwaepushia  Watanzania  adha ya hawa wateule-binafsi woote wenye kuchukua  MITAJI toka kwa "MARAFIKI"  kujinadi nayo.  
 
Hiyo MITAJI wakafungue makampuni ya uwekezaji.

Ukiona mtu anaenda dukani kukopa suti kwa ajira ya kubeba mkaa kwa mama ntilie kaa chonjo saa ni mbaya; Huyu hataki kazi anamtaka mama ntilie mwenye!

 

 


 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment