Sunday 31 May 2015

[wanabidii] Enzi za uwendawazimu na Ujahilia, CHADEMA nilipotea, Namshukuru Jalia, Kwani ameniokoa, Loo! sasa najutia.


Enzi za Ujahilia,
CHADEMA nilipotea,
Namshukuru Jalia,
Kwani ameniokoa,
Loo! sasa najutia.

Enzi za ujahilia,

Nikikumbuka nalia,
Namshukuru Jalia,
Kwa aliyonitendea,
Hakika nilipotea.

Hakika nilipotea,
Njia niliyoiendea,
Kila nikifikiria,
Moyoni najisemea,
Rasini nilitimia?

Enyi mliobakia,
Dua ninawaombea,
Mpate kuiendea,
Njia ya kujitambua,
Nchi kuitumikia,

Babu anawatumia,
Yake yana muendea,
Yenu yana didimia,
Paka wana lialia,
Jikoni wamejilalia.

Paka wana lialia,
Jikoni wamejilalia,
Nchi ingejipatia,
Nguvu nilizojitolea,
Ajabu najionea.

Ajabu najionea,
Wachache wajijengea,
Ngome za kujilindia,
Viti walivyo kalia,
Mafurushi wajilia.


Mafurushi wajilia,
Bila haya nawambia,
Tena wanasingizia,
Gharama walizingia,
Risiti wa'zi chezea.

Hayo yakiendelea,
Kasheshe ipo Songea,
katibu ajionea,
Paka walio zoea,
Jikole kulichezea.

TIMU UZALENDO.


0 comments:

Post a Comment