1. Siupendi umasikini lakini nauchukia zaidi utajiri unaopatikana katika mazingira haram, bora niwe masikini kuliko kuwa na utajiri uliopatikana kwa njia ya rushwa na ufisadi.
2. Bora kuwa masikini kuliko kuwa tajiri kwa utajiri ambao umepatikana kwa kuingia mikataba mibovu isiyokuwa na maendeleo kwa wananchi wenzangu ambao waliniamini kwa kunipa dhamana ya uongozi.
3. Bora niwe masikini kuliko kuwa tajiri halafu nautumia vibaya utajiri wangu kwa kuwashawishi watu wanaishiwishi hali ya kuwa uhalisia naujua kuwa naungwa mkono kutokana mfuko wangu na si utendaji wangu.
4. Bora niwe masikini kuliko kutumiwa na matajiri, ambao nakuwa na mikataba nao ya siri nyuma ya pazia ambayo itakuja kuwanyonya na kuwakandamiza wanyonge.
5. Bora niwe masikini kuliko kuwa na utajiri, ambao nawatesa wenzangu kwa utajiri wangu ikiwemo kufumbia macho maovu ya ufisadi na mafisadi kwa kuwa tu nanufaika nao.
6. Bora niwe masikini kuliko kutumia utajiri wangu kwa kudharau jamii nyingine kwa kupitisha mifugo kwenye mashamba ya masikini nikijua kuwa nitatumia pesa zangu kutoa rushwa na hakuna chombo cha dola kitakachonisumbua iwe mahakama au polisi kwa pesa zangu.
7. Bora niwe marafiki masikini kuliko kuwa na marafiki matajiri, amabao kila siku wanafikiria kufanya hujuma dhidi ya wasionacho na wazalendo wakweli katika jamii.
8. Bora ni niwe masikini kuwa kuwa tajiri halafu nawadhihaki masikini kwa kununua ushawishi wao na kura zao.
9. Bora niwe masikini kuliko kuwa tajiri anayesaka urais kwa bilau na viburudisho pamoja na burudani amabazo hazimsaidii mpiga kura na zenye lengo la kumghiribu mpiga kura ambaye hajui akitoka hapo atakula nini?
1. bora kuwa maskini unayeishi kwa amani kuliko kuwa tajiri unayewagawa Watanzania kwa matamanio ya kutaka urais.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment