Sent from my iPhone
Kusema kweli Mheshimiwa Lowasa anachekesha sana. Kusema kuwa tunatakiwa kuwa na kiongozi mwenye kufanya maamuzi magumu ana maana CCM haifanyi maamuzi magumu na viongozi wake hawafanyi maamuzi magumu na uthubutu. Yeye yuko wapi. Anasahau kama anamsema JK anasema chama chake na viongozi wake na anawapa wapinzani silaha ya kuishambulia CCM?--
CCM watamheshimu kwa kuhujumu chama anachoomba kimchague kuwa mgombea Urais. Sidhani.
Kusema kuwa angekuwa Waziri Mkuu eti hali ingekuwa tofauti anasahau kuwa Waziri Mkuu siye mtendaji nia msimamizi wa collective management? Anataka kusema kuwa Chama chke kimeshindwa kutekeleza majukumu yake. Sasa huku anakisema chama na viongozi wake huku anavaa magwanda yake na anakiomba chama kimteue/
Hivi ana akili sawa sawa au ndio mateke ya mfa maji?.
Kusema yeye anauchukia umaskini? Kwa vipi? Amewafanya wangapi kuwa matajiri kwa kutumia nguvu zake?
Kusema Yeye sio Tajiri bado anausaka utajiri? Anataka kukumbilia Ikulu akautafute huko huku mtaani hakumtoshi.
Watanzania tuchunge sana mtu huyu ni hatari na janga la taifa
Herment A. Mrema
Date: Sun, 31 May 2015 08:17:45 -0700
From: mairi.info@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] RE: SAFARI YA MATUMAINI NA EDWARD LOWASSA!SAFARI YA MATUMAINI NA EDWARD LOWASSA!
Mheshimiwa Edward Lowassa ametangaza nia akiomba kuteuliwa na Chama chake kuwa Mgombea Urais kwa mwaka 2015. Lakini zipo kasoro kadhaa zilizojitokeza kwenye sherehe ile, ambazo binafsi naomba zisahihishwe, zisijitokeze tena! Kasoro hizo ni pamoja na:
1. Matangazo kupitia ITV EATV na AZAM TWO kukatikakatika na wakati mwingine kuonesha mchelemchele.
2. Dj. hakuwa amechagua nyimbo mahususi kuendana na tukio na wakati husika pale alipotakiwa kucheza wimbo husika.
3. Mtangaza nia kumtaja Kiongozi wa Chama chake kuwa, huenda akatumia baadhi ya maneno kupata sababu ya kumwadhibu tena. Hii inajenga hisia ya msuguano ndani ya Chama.
4. Baba Askofu kutumia kutumia maneno machungu kuwa, wasiompenda Mtangaza nia wakale malimao. Mtumishi wa Mungu anapaswa kutumia maneno ya upako na ushawishi.
5. Mzee Kingunge kutumia mkutano wa kutangaza nia kuelezea ajenda ya katiba mpya, ambayo bado ina maswali mengi kwa watanzania, na hivyo kutumia muda mrefu kuhutubia kuliko hata mtangaza nia.
Nakubaliana na Mtangaza nia kwa mambo haya:
1. Nchi yetu inahitaji kiongozi mwenye uthubutu anayeweza kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya watanzania.
2. Nchi yetu inahitaji kiongozi atakayesimamia raslimali zetu kama vile madini, mafuta na gesi zisichukuliwe ovyo ovyo na wawekezaji uchwara.
NB: Huu ni mtizamo wangu binafsi, maana mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa hapa Tanzania, ila ni mpiga kura mzoefu, ambaye nimejiandaa kujiandikisha kwa mfumo wa BVR.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:
Post a Comment