Sunday 31 May 2015

Re: [wanabidii] LOWASSA UACHE UONGO

Tatizo kambi lowassa mme lost mbaya . hata kwa dodoki la chuma hasafishiki huyo . you are wasting your time . Mtu alishindwa hata kushika mic ataweza kufanya kazi gani ?
Kuweni makini na mnayemnadi . Anapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa . wait you will see . Jiandaeni kupata vitanda hospitalini kwa pressure . Penye kosa mkubali kukosolewa . 

On Sunday, May 31, 2015 at 12:05:53 PM UTC+3, Mike Zunzu wrote:
Natamani dada huyu angelipewa nafasiu ya juu kwenye tume ya uchaguzi.



On Sunday, 31 May 2015, 0:00, 'lesian mollel' via Wanabidii <wana...@googlegroups.com> wrote:


wee katabazi mwandishi gani bana usiejua hata kiswahili, dada ni hadhara si adhara, nshaandika sana magazeti ya kimombo na mimi ni mmasai lakini kiswahili nakijua na siwez andika hv, adhara halafu unajiita makini, unapendaga kujisifia na kuwaponda watu tuuuuu as if ur perfect while ur fake in every work u put the public
Lowasa si mjinga wa kijibu ujinga, anatangaza nia na nia maana yake atasimamia nini hajaja kujisafisha na watanzania wamesema  liwalo na liwe hata kama mtakomaa na richmond wao wanamtaka hvo alivyooooo, polen na agenda yenu chafuu mtashindwa hadi mkome
Hes smart ndo maana si mtu wa kujisifu ni mtu wa matendo hawez kuanza kuzungumzia past while anatakiwa kuwaambia watanzania kua atawaondoaje hapa alipo ndio maana ya safar ya matumaini elimu, elimu, elimu....leo kakabiziwa mzigo na mzee nyerer aliebakia mwl  wa itikadi, mwl wa kivukoni elimu ya siasa mel kingunge ngombale mwiru kasema mzigo huu akabidhiwe mnyamwezi lowasaaaaaaaaaa. lowasa oye...who else...mti weny matunda matamu ndio unaorushiwa mijiwe
Hua  nashangaaa kina Gamba, kina Makamba jr na Kigwa vijana wq3nzangu badala ya kunadi sera zao wamekua wanajibu na kumponda mgombea mwenzao sawa na wazee kina Membe kina Mwigulu, mkibisha ,,,,angalieni kuanzia kesho
sasa najiuliza huo si uogaaa, au kutojitambua, nadi sera zako na si kuanza kumponda mgombea mwenzako na je akija shinda itakaujeeeeeeee, sawa na huyu mdada mpondaji anaejiita kukaa kwenye media 15 yrs while bado anaandika rubbbish
mollel
Kambi Lowasa


From: 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wana...@googlegroups.com>
To: WANABIDII <wana...@googlegroups.com>
Sent: Saturday, May 30, 2015 12:06 PM
Subject: [wanabidii] LOWASSA UACHE UONGO

LOWASSA UACHE UONGO

Na Happiness Katabazi

NIMEMTAZAMA kupitia Televisheni ya ITV ,Mzee Edward Lowassa na kuisoma neno kwa neno hotuba yake ya kutangaza nia leo katika Uwanja wa Sheikh Abeid Mkoani Arusha ya kugombea urais wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimebaini uongo wazi katika aya ya kwanza.

Haya hiyo katika hotuba hiyo inasomeka hivi; HOTUBA YA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KWA AJILI YA KUTANGAZA NIA YA KUOMBA KUTEULIWA KUWA MGOMBEA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) KWA NAFASI YA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA).

Ukisoma kichwa hicho cha habari cha hotuba yake kimesema ( Hotuba ya Mheshimiwa Edward Lowassa kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari......).

Sehemu ya hiyo aya Lowassa amedanganya umma kuwa eti leo amezungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza nia.

Ukweli ni kwamba Lowassa leo ametangaza nia mbele ya wafuasi wake katika mkutano wa adhara ambao wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya,wasanii wa Kimasai wakiwa na mishale na silaha za jadi na mwanamuziki wa muziki wa Taarabu Hadija Kopa walitumbuiza.

Binafsi ni mwandishi wa habari kwa zaidi ya miaka 15 sasa,nimeisha shiriki mikutano mbalimbali ya waandishi wa habari na vyanzo vya habari(source) yaani (Press Conference).

Kitaaluma mkutano wa waandishi wa habari uhusisha waandishi wa habari na wale wanamsindikiza mtoa habari na mkutano na waandishi wa habari katika eneo la mkutano.

Mkutano na waandishi wa habari haunaga mbwembwe ,kualika makundi ya watu mbalimbali, wasanii,vibweka kama tulivyovishuhudia leo katika mkutano huo ,wafuasi wako kupaza sauti kusema Lowassa Rais,wanasiasa kupanda majukwaani kumnadi mtoa habari(Lowassa), kama ulivyoshuhudia leo katika mkutano ile jinsi Kingunge Ngombale Mwilu, Kangi Lugola, Mtumishi wa Mungu Josephat Gwajima, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha,Onesmo Ole Nangolo walivyokuwa wakimpigia debe Lowassa.

Kimsingi tukubaliane Lowassa kupitia aya hiyo ya hotuba yako ya leo amedanganya umma na amejidanganya yeye mwenyewe na kujionyesha asivyo makini katika baadhi ya mambo.

Hata kama hiyo hotuba uliandaliwa na waandishi wako wa hotuba unaowaamini,kama kweli wewe ni kiongozi makini na unayetaka kuwa rais wa nchi hii kwa kila njia, ulipaswa uisome kwanza hotuba hiyo neno na kwa dosari hii imedhirisha na wewe siyo makini.

Hadi ulikubali kuisoma hiyo hotuba mbele ya adhara ina maana ulikubaliana na mambo yote yaliyoandikwa kwenye hiyo hotuba ambapo baada ya wewe kuisoma jukwaani leo sisi wafuatiliaji wa mambo ndani ya muda mchache tumeibaini ina kasoro hiyo ya wazi kabisa tena kwenye kichwa cha habari.

Sasa hao waandishi wa hotuba yako utawachukulia maamuzi magumu? Maana umekuwa ukijinasibu wewe ni kiongozi unayeweza kuchukua maamuzi magumu kwa haraka.

Nakushauri anza kutoa maamuzi magumu kwa hao waandishi wa hotuba yako hii ambayo ni hotuba ya kihistoria kwani hotuba hii ni ishara ya wewe kuanza safari ya matumaini kwenda Ikulu lakini tayari nimeibaini ina dosari hiyo.

Nyie waandishi wa hotuba ya Mzee Lowassa kuweni makini na kazi yenu, au kama mmetumwa kumuandikia ujinga huo mzee Lowassa katika hotuba zake ili atolewe kasoro kuwa sio makini,mseme maana waandishi wengi hivi sasa hamuaminiki mmekuwa kama wanawake Malaya wanaouza mihili yao ambao wana mabwana wengi ili mradi wapate fedha upitia mihili yao.

Na hili linawezekana maana aingii akili mwandishi wa habari amuandalie hotuba mtu anayemuunga mkono afanye kosa la kiufundi kama hili tena katika kichwa cha habari.

Niitimishe kwa kumtaka Lowassa aache uongo.Ule ni mkutano wa adhara aliohutubia leo wakati akitangaza nia na siyo mkutano wake na waandishi wa habari kama alivyodai katika hotuba yake. Hongera sana Mzee Lowassa kwa mkutano wako huo uliofurika watu wengi.Ila ukumbuke msemo usemao ' Kuzikwa na watu wengi sio kwenda Mbinguni.

Kila la kheri katika hiyo safari yako
Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Mei 30 mwaka 2015..
--
Send Emails to wana...@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wana...@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment